acha fikra mgando mkuu, Pep kumuondoa Toure Barca na Man City hakuna mahusiano na ubaguzi, ni kua simple jamaa haendani na mfumo wake. Hapo hapo ndani ya Barca walikuepo akina Abidal na Keita mbona wao hakuwaondosha? Abidal aliendelea kuwa first choice wa pep licha ya uwepo wa mchezaji kama Maxuel mwenye uwezo mkubwa Zaidi wa skills kuliko Abidal.
Pep pia aliwaondosha Deco, Zlatan, wachezaji wenye hadhi zaidi ya huyo Toure mbona hamsemi kama ni ubaguzi? au kwa kuwa wao ni weupe hakuna tatizo kuondoshwa lakini akiwa mweusi ndio ubaguzi?
Mchezaji mweusi akiwekwa bench au akiuzwa munaanza kulalamika ni ubaguzi achene kulalamika kipuuzi.