Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
NILIKUWAPO ZANZIBAR KIBANDA MAITI, JAWS NA KIJIWENI MALINDI MIAKA 30 ILIYOPITA
Kitabu hiki, "Cade" cha James Hadley Chase nimekisoma miaka mingi sana iliyopita niko sekondari umri wangu kiasi miaka15 hivi.
Sasa mimi ni mzee lakini nakumbuka ufunguzi wa mwandishi alipoanza kueleza hadithi ya Cade mpiga picha wa magazeti bingwa.
Anamweleza Cade yuko ndani ya ndege inakaribia kutua kwenye mji fulani Amerika ambako kunatarajiwa kufanyika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi.
Cade anategemewa awepo kwenye maandamano haya ili jicho la camera yake lishuhudie yote yatakayotokea siku ile na camera ile picha zake zionekana dunia nzima na dunia ishuhudie wanachokipigania jamii ya watu weusi wa mji ule.
Ufunguzi huu wa kalamu ya James Hadley Chase unajifungua kichwani kwangu nikiwa nimekaa mgahawa maarufu wa "Passing Show," Zanzibar nikitazama maandamano makubwa ya ACT Wazalendo wanapita Malindi wanatokea bandarini kumpokea kiongozi wao maarufu kwa jina la OMO mgombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu unaokuja.
Niko "Passing Show," nakunywa chai kwani ndiyo kwanza nimeingia na boti ya mapema kutoka Dar es Salaam iliyomchukua OMO na msafara wake.
Nimeshuhudia heka heka za ACT ndani ya chombo na halikadhalika nimeshuhudia umma wa wanachama wa ACT waliofika bandarini kumpokea OMO kama mgombea urais wa Zanzibar.
Sauti za matarumbeta na ngoma zinahanikiza pale nilipokaa nayaona maandamano yakipita.
Hakika niko "Passing Show," nikitazama passing show.
Lakini pana ujumbe katika maandamano haya mbali na nyimbo zinazoimbwa.
Waingereza wanasema, "Show of strength."
Waandamanaji wanaonesha nguvu ya chama chao.
Ubongo unafungua ukurasa wa pili.
Miaka 30 iliyopita nilikaa mahali hapa hapa siku ya pili baada ya Wazanzibari kupiga kura Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995, uchaguzi uliokuwa na upinzani mkubwa kati ya Komando Salmin Amour na Maalim Seif Shariff.
Naikumbuka siku hii kama jana.
Zanzibar iliamka baada ya kupiga kura kukiwa na tetesi kuwa Maalim kambwaga Komando.
Nimekaa kijiweni kwangu nje ya 'Passing Show" asubuhi naishuhudia Zanzibar ikisisimka.
Hakuna mazungumzo ila ushindi wa CUF dhidi ya CCM.
Leo CUF haipo.
Maalim hayupo.
Lipumba yupo na CUF halikadhalika ipo ingawa naiona CUF katika ACT Wazalendo.
Miaka imeruka.
Miaka imepeperuka.
Nayatazama maandamano na akili yangu inaniambia kuwa hao jicho langu linachoangalia wanaandamana ni CUF kwani CUF haikuondoka kwa maneno, "Shusha tanga pandisha tanga."
Hakikubadilika kitu.
Watu ni wale wale na mambo ni yale yale.
Lakini akili yangu inaniambia kuwa CUF ipo na itashiriki uchaguzi Zanzibar.
''A shadow of it's former self,'' Waingereza watasema.
Umri ni muhimu katika chama cha siasa kwani umri ndiyo unaokuza chama cha siasa kama vile umri unavyomkuza binadamu.
Chama si sare mpya na jina jipya la chama.
Akili ina hulka ya kusema na kujijibu yenyewe.
Nikakumbuka hotuba ya Prof. Lipumba Kibanda Maiti kufunga kampeni na siku ya pili inapigwa kura kuchagua Rais wa Zanzibar.
Miaka 30 imepita.
Siasa za Zanzibar siku zote zina mengi ya mtu kujifunza ila kitu kimoja hiki lazima ukikubali.
Zanzibar ni nchi ya vyama viwili tu na hii ndiyo sababu CUF haionekani ukitaka kuitafuta utaiona katika ACT Wazalendo kama mimi nilivyoiona nikiwa nakunywa chai ''Passing Show.''