Uchaguzi 2020 Nilikuwepo kwenye mkutano, sijapenda kuchangishwa fedha kinguvu

Uchaguzi 2020 Nilikuwepo kwenye mkutano, sijapenda kuchangishwa fedha kinguvu

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Leo kama kawaida niliwahi mapema sana kwenye mkutano kusikiliza sera za mgombea wetu.

Mengi ameeleza vizuri sana japo kuna ambayo ameyarudia rudia sana.

Kingine nilichopenda ni muda wa mgombea umekuwa mrefu sana kapata karibu saa nzima tofauti na 2015 kipindi cha Lowassa ambae alikuwa anaongea dakika 3 tu.

Ila katika yote kubwa ni hili la kutaka kuchangishwa fedha kilazima/kinguvu. Mgombea wetu anatuambia "haya toeni hizo simu zenu za mchina, bonyeza *150*00# kisha chagua namba 4 kisha..."

Baadhi tuliokuwa hapo tukajiuliza kajuaje tuna pesa kwenye simu? Kwa kuzuga tukamjibu hakuna network, akasikia.

HATUJAPENDA HII, WEKENI NAMBA AU ACCOUNT KWA MUDA MTU ATAOTAKA KUCHANGA ATAWACHANGIA.
 
Katuambia toa simu yako kisha bonyeza. Hapo hukuona kama tumelazimishwa?
Mbona unakuwa muongo hivyo. Nilikuwepo kwa nini sijaona wakikabwa mashati kuchangia.
We utakuwa mchawi tu, si bure!
 
Nimesikia kuwa baada ya kuona watu wanachangia, mkakata mtandao!! CCM waoga sana...
 
Mbona unakuwa muongo hivyo. Nilikuwepo kwa nini sijaona wakikabwa mashati kuchangia.
We utakuwa mchawi tu, si bure!
Huyo Lumumba anaona wivu watu walivyochanga kwa moyo bila kujiuliza
 
Back
Top Bottom