Habari za sasa hivi ndugu wana jf, leo pia ni siku nzuri katika jiji la dsm kwa kuwa kuna kampeni za mgombea wetu wa uraisi pale Tanganyika Packers.
Hapa nilipo(kimara) nipo na jamaa zangu kama 20 hivi tunajiandaa kwenda huko kwa ajili ya kusikiliza sera mbadala na nzuri kabisa kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu.
Jana haikuwa siku nzuri kwa kuwa tulighafirika kwa kitendo cha kuombwa pesa kinguvu kutoka kwa mgombea wetu wa uraisi.
Kwa kuwa bado tunapenda sera mbadala, leo tutaenda pia ila angalizo "HATUTAKI KUOMBWA PESA".
Leo hatutasingizia network, bali tutaamua kuondoka mkutanoni.
Wanasiasa mtuonee huruma, chama kilikuwa na wabunge zaidi ya 50 ambao ukichukua kiinua mgongo chao cha zaidi ya mil 200 ukizididha mara 50 unapata bilioni 10 na zaidi.
Billioni 10 ni pesa nyingi sana, kwa nini chama kisiwaombe wabunge wao wastaafu wachangie kila mmoja mil 100(nusu ya walichopata) , ili kupata atleast billion 5 ambazo naamini zinatosha sana.
Kutuchangisha kinguvu sisi ambao hata elfu 5(5000) kuipata kwa siku ni kazi, hiyo ni dhambi kubwa sana.
Mwananchi wa kawaida naipambania elfu 5 kwa siku alafu unataka nikuchangie wewe ambae juzi tu umelipwa kiinua mgongo cha zaidi ya mil 200, hii HAIWEZEKANI NA HAIKUBALIKI.
Wote tunafahamu jinsi mtaani palivyo pagumu na pesa hakuna na ajira hakuna, sasa za kuwapa nyie tunatoa wapi?
TUTAENDA ILA HATUTACHANGA