Nililinyamazia WhatsApp group la Sekondari kutokana na kuchoshwa na vizinga

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Kwa nia njema ya kujumuika tena na wanangu wa sekondari. Safari hii ilikuwa kupitia WhatsApp group.

Halikuwa tofauti sana na magroup mengine, mambo yalikuwa ni yaleyale tu, kusaidiana kwenye shida na raha. Tuliweka mkakati mzuri wa kusaidiana kwenye misiba na ugonjwa.

Kosa nililofanya ni kuwa kinara wa kuchangia. Niliona ni sehemu nzuri ya kuwasaidia washkaji ambao wengi wao hawakuendelea na masomo. Kwa hiyo ikawa kama members watachanga laki basi mimi naongeza laki nyingine ili mchango ukasaidie mwenye changamoto.

Hili lilikuwa ni kosa, badala ya wadau kunichukulia kama mwenye moyo wa kutoa wao wakaona kama ninazo za kugawa tu. Sms za kuombana hela zikawa nyingi. Bahati nzuri mimi ni mtu niliyenyooka mara nyingi nilijibu sina. Wale wasumbufu sana nikawa sipokei simu zao.

Mwisho nikachoka, nikapiga kimya nikawa sichangii chochote kwenye charting za group.

My Take
Tupunguze mizinga kwenye group. Tunawakimbiza watu wazuri
 
Kutoa ni moyo na ni faida kwako zaidi ila kosa ulilofanya ni kuruhusu Ego yako ikutawale na kufanya uhukumu hali na vipato vya wenzako..

Nakubaliana na wewe kusema hauna ila mizinga haiwezi kupungua sababu ya umasikini uliotengenezwa na serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 60.

Shukuru sana kama una uwezo na kipato ila jitahidi usiwaangalie chini hali zao wenzako wasioweza kuchangia.
 
Kwa nia njema ya kujumuika tena na wanangu wa sekondari. Safari hii ilikuwa kupitia WhatsApp group.

Halikuwa tofauti sana na magroup mengine, mambo yalikuwa ni yaleyale tu, kusaidiana kwenye shida na raha. Tuliweka mkakati mzuri wa kusaidiana kwenye misiba na ugonjwa.

Kosa nililofanya ni kuwa kinara wa kuchangia. Niliona ni sehemu nzuri ya kuwasaidia washkaji ambao wengi wao hawakuendelea na masomo. Kwa hiyo ikawa kama members watachanga laki basi mimi naongeza laki nyingine ili mchango ukasaidie mwenye changamoto.

Hili lilikuwa ni kosa, badala ya wadau kunichukulia kama mwenye moyo wa kutoa wao wakaona kama ninazo za kugawa tu. Sms za kuombana hela zikawa nyingi. Bahati nzuri mimi ni mtu niliyenyooka mara nyingi nilijibu sina. Wale wasumbufu sana nikawa sipokei simu zao.

Mwisho nikachoka, nikapiga kimya nikawa sichangii chochote kwenye charting za group.

My Take
Tupunguze mizinga kwenye group. Tunawakimbiza watu wazuri
Waingereza wanasema "No good deed goes unpunished".
 
Wewe siyo Abubakar Msambata Masojo?,Kwahiyo kumbe ulitukimbia mwanangu halafu unakuja kutusimanga huku?

Ngoja niwashitue wadau waje waone ulivyo Mkuda!

Kununua hako gari tu sikuhizi unanata kinoma!

Aisee sikutegemea kama hili suala utalileta humu!
 
Kumeanza kufuka Moshi.

Nausubiri moto 😎
 
Mimi mpaka namba ya simu kama na mfahamu nampa ya simu ambayo sitaki kuwasiliana.

Kuna watu wanataka kuishi kukufanya daraja.
 
Wewe siyo Abubakar Msambata Masojo?,Kwahiyo kumbe ulitukimbia mwanangu halafu unakuja kutusimanga huku?

Ngoja niwashitue wadau waje waone ulivyo Mkuda!

Kununua hako gari tu sikuhizi unanata kinoma!

Aisee sikutegemea kama hili suala utalileta humu!
Itakuwa yeye maana maelezo yana fanana na shiti zake
 
Kwa nia njema ya kujumuika tena na wanangu wa sekondari. Safari hii ilikuwa kupitia WhatsApp group.

Halikuwa tofauti sana na magroup mengine, mambo yalikuwa ni yaleyale tu, kusaidiana kwenye shida na raha. Tuliweka mkakati mzuri wa kusaidiana kwenye misiba na ugonjwa.

Kosa nililofanya ni kuwa kinara wa kuchangia. Niliona ni sehemu nzuri ya kuwasaidia washkaji ambao wengi wao hawakuendelea na masomo. Kwa hiyo ikawa kama members watachanga laki basi mimi naongeza laki nyingine ili mchango ukasaidie mwenye changamoto.

Hili lilikuwa ni kosa, badala ya wadau kunichukulia kama mwenye moyo wa kutoa wao wakaona kama ninazo za kugawa tu. Sms za kuombana hela zikawa nyingi. Bahati nzuri mimi ni mtu niliyenyooka mara nyingi nilijibu sina. Wale wasumbufu sana nikawa sipokei simu zao.

Mwisho nikachoka, nikapiga kimya nikawa sichangii chochote kwenye charting za group.

My Take
Tupunguze mizinga kwenye group. Tunawakimbiza watu wazuri
Sawa tajiri
 
Jivunie kuwa katika nafasi ya kutoa kuliko kupokea
Hii statement imekaa kitapeli sana.

Hao wanao pokea, kwa nini na wao wasitoe?

Kwamba kwenye hii Dunia, kuna ambao wao ni kupokea tu?

Wao kutoa, haiwahusu.

Huu utapeli upo sana kwenye dini, unaambiwa, ni heri zaidi kutoa, kuliko kupokea.

Ulaghai huu. Wakuibia wajinga.
 
Me nimelivungia group la wajukuu mablaza wana vizinga sio powa, mtu mzima na watoto wake watatu ananipiga kizinga bachela.

Mwendo wa sina tu.
 
Wewe siyo Abubakar Msambata Masojo?,Kwahiyo kumbe ulitukimbia mwanangu halafu unakuja kutusimanga huku?

Ngoja niwashitue wadau waje waone ulivyo Mkuda!

Kununua hako gari tu sikuhizi unanata kinoma!

Aisee sikutegemea kama hili suala utalileta humu!
Abuu kazingua kinoma..😂😂
 
Back
Top Bottom