Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Inawezekana ni huyo huyo alienda kutafuta mawindo
Duuh...! Pole sana mkuu. JKT ya mbeya uyole unaifahamu kweli ilipo?. Mbona sio maeneo yenye kufikiwa na maji?. Halafu ni katikati kiasi kwamba chatu alitokea upande gani mkuu?. Maana ni kama hamna poli. Labda ungesema nyuma ya sec ya mbeya day kuna mto kule na vichaka pembeni ya mto. Isitoshe kule tuliwahi kusikia kuna chatu anapita maeneo yale

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaisahau elnino ya mwaka tajwa hapo juu, mvua zilikuwa kubwa sana kule maeneo ya Mbeya bila kujua nikaingia kwenye mtego wa chatu, alinidondosha.

Pona yangu sikuamka, na ukilala chali chatu hakuwezi alinitambaa sana mwilini ili anivingirishe ila nilijikaza na ile ngozi yake laini ilivyokuwa inanitambaa mwilini.

Nilijikaza lakini alibahatisha kunimeza mguu wote; alishindwa kunimalizia kwasababu nilikuwa nimetanua mguu wa kulia hivyo sikupita mdomoni mwake. Niliokolewa baada ya masaa matatu ila mguu uliungua sana.

Huwezi amini tulikuwa tunaangaliana jicho kwa jicho huku nimelala, ujasiri huu niliupata baada ya kulewa sana pombe ya Kiroba ilikuwa maarufu sana kule Mbeya inaitwa Double Punch.

Chatu msikie tu. Yupo kama jini au shetani, yale macho yake mkitazamana kwa karibu.
mmh we jamaa story yk ni ngumu kuiamini maana hujaelezea chanzo kwa ninavyojua nyoka chatu akurupukii kitoweo tena kikubwa km binadamu huwa anafanya maandalizi mapema sio chini ya 3 days akikufuatilia anakutathmini ndio maana ni ngumu sana chatu akiattack mnyama kutokea makosa..

binafsi nilishaona jamaa mmoja akipambana na chatu ana kwa ana bila silaha yoyote na chatu alinawa mikono jamaa akaenda kumuuza kwa watu wa maonesho ila mtiti wake haukuwa mdogo yule mtu alikuwa ameshiba kwelikweli na chatu ni km alifanyiwa ambush tu akajitetea ila wapi nguvu zilimwisha akawa mdogo km pritoni.

ilianza km masihara chatu ameonekana kwenye pori moja kubwa jamaa mmoja aliyeshiba akaitwa chatu alifukuzwa huku anakimbilia upande mwingine km mara mbili tatu mara chatu aliamua kujitetea isee alimgeukia jamaa wakawa wanaangaliana face to face watu wote walitawanyika wakakimbia mbali yule mtu alikuwa jasiri sijaona maana chatu alimvaa jamaa akajivingilisha kwenye kiuno ili kumtisha jamaa wapi anamzungulusha kumtoa kila chatu akijivingirisha jamaa anamkujua picha ilichezwa km nusu saa hivi yule chatu akawa amechoka kabisa ngumu hana na jamaa nae jasho zinamtoka balaa..mwisho wa siku chatu aliku mpole..
 
Unataja simu za mwanzo kuwa n camera unaitaja tecno? Tangu lini hiyo kampuni ikagundua teknolojia mpya. Mimi simu ya kwanza ya camera niliiona kwa brother mmoja alitoka Dubai, 2008 ilikuwa.
Simu ya kwanza ya kamera kuiona ilikuwa ni nokia nayo niliiona 2003 kwa shangazi yangu aliyekuwa bandari
 
Sitaisahau elnino ya mwaka tajwa hapo juu, mvua zilikuwa kubwa sana kule maeneo ya Mbeya bila kujua nikaingia kwenye mtego wa chatu, alinidondosha.

Pona yangu sikuamka, na ukilala chali chatu hakuwezi alinitambaa sana mwilini ili anivingirishe ila nilijikaza na ile ngozi yake laini ilivyokuwa inanitambaa mwilini.

Nilijikaza lakini alibahatisha kunimeza mguu wote; alishindwa kunimalizia kwasababu nilikuwa nimetanua mguu wa kulia hivyo sikupita mdomoni mwake. Niliokolewa baada ya masaa matatu ila mguu uliungua sana.

Huwezi amini tulikuwa tunaangaliana jicho kwa jicho huku nimelala, ujasiri huu niliupata baada ya kulewa sana pombe ya Kiroba ilikuwa maarufu sana kule Mbeya inaitwa Double Punch.

Chatu msikie tu. Yupo kama jini au shetani, yale macho yake mkitazamana kwa karibu.

Wewe Muongo, kamwe huwezi kunusurika kwa chatu, akishindwa kukumeza mguu mmoja anarudia kichwani, na mara zote humeza mawindo yake baada ya kuyaua kwa kujiviringa na kuhakikisha kwamba yamekufa ndipo huanzia kumeza toka kichwani.
 
Mbeya karibu na reli ya tazara maeneo ya kambi ya jkt mbeya walikuwa na huo mtindo zamani wanapiga picha matukio halafu wanauza picha
We ulikuwa unaota ndoto maana unasema ulilewa, afu kwa maeneo ya jeshini sidhani kama wanajeshi wamgeshindwa kukuokoa, hao waliokuwa wanakupiga picha walitumia vifaa gani au sio utaratibu wa wana mbeya upatwe na tatizo afu waanze kukuangalia tu. Kingine kama ulilewa ulikuwa na ujasiri gani wa kujilaza kumzuia chatu asikuviringe ili kukuvunja. Bila hizo picha mimi nikiwa mwana mbeya hapa nakuona MUONGO sana aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili jama linaonekana punguani uki fatilia threads zake. Kuna nyingine limepost sjui chupi nyeupe imefanyaje sjui hili haliko sawa kichwani kwakweli
 
Back
Top Bottom