Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Sitaisahau elnino ya mwaka tajwa hapo juu, mvua zilikuwa kubwa sana kule maeneo ya Mbeya bila kujua nikaingia kwenye mtego wa chatu, alinidondosha.

Pona yangu sikuamka, na ukilala chali chatu hakuwezi alinitambaa sana mwilini ili anivingirishe ila nilijikaza na ile ngozi yake laini ilivyokuwa inanitambaa mwilini.

Nilijikaza lakini alibahatisha kunimeza mguu wote; alishindwa kunimalizia kwasababu nilikuwa nimetanua mguu wa kulia hivyo sikupita mdomoni mwake. Niliokolewa baada ya masaa matatu ila mguu uliungua sana.

Huwezi amini tulikuwa tunaangaliana jicho kwa jicho huku nimelala, ujasiri huu niliupata baada ya kulewa sana pombe ya Kiroba ilikuwa maarufu sana kule Mbeya inaitwa Double Punch.

Chatu msikie tu. Yupo kama jini au shetani, yale macho yake mkitazamana kwa karibu.
Mkuu nasikia ukimezwa na chatu ukaokolewa hua kuna majira ya mwaka yakifika hali ya mwili inabadilika, je kwa mguu wako uliomezwa na huyo chatu hakuna kipindi cha mwaka kikifika mguu unabadilika?
 
Mkuu nasikia ukimezwa na chatu ukaokolewa hua kuna majira ya mwaka yakifika hali ya mwili inabadilika, je kwa mguu wako uliomezwa na huyo chatu hakuna kipindi cha mwaka kikifika mguu unabadilika?
Unabadilika mguu unakuwaje??🙄🙄😲😲
 
Back
Top Bottom