Mwalimuwavichaa
Member
- Nov 9, 2021
- 17
- 33
Nawasalimu JF kwa salamu ya Hi Five...GOOD!
Niende kwenye point.
Ninaweza kusema naongozwa sana na hisia zang tu (Emotion), hata akili natumia pia., na kwa bahati mbaya sana sikuwa mshabiki kindaki ndaki wa mpira. Ila kutokana na ushawishi wa rafiki yangu nilijikuta naipenda simba na kuimba nyimbo za Pira Biriani, pira sambusa, WIDA N.K. Kitendo cha Manara kufanyiwa figisu na kuhamia Yanga basi na mimi nikamfata.
Ndio najua na leo Namungo wametupa kichapo ila bado ntabaki huku. Huyu mtu niliona ana kipaji kikubwa sana cha ushawishi mpaka akanifanya mimi nikapenda Mpira. Mechi ya simba ilipokuwa ikicheza nilikuwa napata kinywaji changu kwa furaha iliyopita kifani mana mwisho wa siku ubingwa ulikuwa kwa simba tu.
Nilimfata baada ya kuona kuna binti kavamia utawala ilihali uwezo hawezi kuwa nao kama wa Manara. So nilipokutana na clip za Manara kulia kwenye mitandao kwa kufanyiwa hujuma, ikaniuma sana nami nikamfata alipo sasa. Najua kuna povu hapa. Kila mtu na afate hisia zake bwana[emoji41]. Twende kwa Diamond Plutnum na Harmonize..
Nilimkubali sana Diamond kutokana na historia yake chungu sana aliyopitia katika maisha. Hata nyimbo zake zilionyesha kuwa jamaa alikutana na ugumu wa maisha ikampelekea kufanya biashara za kawaida sana ili kujikimu kimaisha.
Ugumu wa maisha haukumzuia moyo wake kupenda wale aliohisi wanaweza kuwa pamoja. Matokea yake walimkimbia kwa kuwa hakuwa na hadhi ya kuwa nao kwa kipindi hicho. Kwa kifupi Diamondi Mungu kampa kipaji kikubwa sana hapa Duniani.
Ila sasa kwa hiki kilichotokea kwa Harmonize kimeanza kunirudisha nyuma mpaka nianze kufikiria ule uhusiano wa Diamondi na Baba yake........
Itaendelea