Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Mwaka 2020 kuna kiongozi WA chama kikubwa hapa nchini ambaye ni Rafiki yangu na ninayemheshimu Sana. Wakati tunapiga Stori mbili tatu akanishauri nijiunge na chama chao lakini nilimkatalia na kumwambia kuwa sitawatendea Haki yeye na chama chake na watu wengine ikiwa nitajiunga na chama chao.
Nilimwambia, nataka niwe mkweli, nisione uzito pale ninapohitaji kusema Ukweli na mchango wangu unapohitajika. Kama ni kupongeza ni pongeze Kwa dhati na sio kupendelea. Na kama ni kukosoa nikosoe bila kuumauma.
Akaniambia, kwani ukiwa ndani ya chama huwezi kutenda HAKI. Nikamwambia, ninahisi kitu kama hicho ingawaje sina uhakika Kutokana na kuwa sijawahi kuwa na chama. Akaniambia, huo ni wasiwasi wangu tuu. Chama chao kinatoa nafasi na Uhuru Kwa Watu wa karba yangu. Nikasema, anipe muda nitafikiri. Hasa nitakapoona Watu wa aina yangu ndani ya chama chao.
Jana alinigusia na kunikumbushia Jambo lilelile ikiwa ni Baada ya miaka mitatu sasa kupita.
Napenda kusema Ukweli, na kutenda haki kama nitakuwa katika nafasi ya kutakiwa kufanya hivyo. Bila kujali nimesimama Mbele ya nani.
Sipendi kuwa chawa na kiberenge cha kukubali hata mambo yasiyofaa kisa anayefanya ni Boss wangu.
Ukiwa boss wangu ukitaka ukweli ambao wengine wanaogopa kukuambia Sisi ndio tupo Kwa kazi hizo. Bila kujali utakasirika au utafurahi. Au utatufukuza kazi. Ingawaje heshima na hadhi yako nitailinda( Kwa sababu hiyo ni Haki yako) lakini ukweli utapewa tuu.
Kama hutaki ukweli au utaona maneno yangu yatakukwaza usiniite. Ita wale ambao husema kile unachopenda kusikia. Lakini Sisi tutasema kile ambacho unapaswa kukisikia.
Mzee WA chama, najua utasoma hapa, niwie radhi. Nilikuambia nikipewa uanachama haitaisha miezi mitatu nitafukuzwa😂😂 au sitaruhusiwa kuingia kwenye vikao🏃🏃
Pumzika sasa.