NILIMPA FIGO YANGU
Kila ninapokumbuka, moyo wangu unauma,
Nilimpenda Rebeka, ni binti wa Kimanyema,
Chuoni nilipofika, kwa pamoja tulisoma,
Nilimpa figo yangu, la mbele sikutambua.
Tangu afike chuoni, Rebeka nilimpenda,
Kimtazama usoni, utakutoka udenda,
Ni shombe shombe makini, lizaliwa huko Ndanda,

Hakika aliumbika, ukweli shime tuseme,
Nyuma kulitikisika, pitapo kwa wanaume,
Libaki kiweweseka, kithubutu ainame,

Mwaka wa kwanza chuoni, ule muhula wa pili,
Mimi linipa idhini, niwe wake wa ukweli,
Nilifurahi jamani, bila jali yangu hali,

Ahadi tukaiweka, chuo tukishahitimu,
Ya kumuoa Rebeka, mwanamama shamushamu,
Kwetu akatambulika, kama wifi ama shemu,

Mwaka wa tatu chuoni, alianza kuugua,
Kule hosipatalini, ugonjwa waligundua,
Figo ikasumbueni, miguu imevimbia,

Tumbo akavimba sana, mithili mjamzito,
Daktari akanena, maneno hayo mazito,
Rebeka aweza pona, ukifwatwa huu wito,

Abadilishwe nyingine, figo moja imeoza,
Ndugu wote muitane, jambo hili mtaweza,
Ila aliye mnene, changa figo nakataza,

Ndugu wote likataa, wa kumtolea figo,
Wote walitokomea, kwa kugeuza visogo,
Mie nikajitolea, Rebeka apate figo,

Haliye ikawa nzuri, mithili kule zamani,
Rebeka wangu mzuri, tukahitimu chuoni,
Ndipo likaanza shari, aliporudi nyumbani,

Simuni hapatikani, kwenye mitandao pia,
Lienda kwao nyumbani, kioja lijionea,
Ameshakuwa ndoani, mke wa pili mekua,

Nililia mimi sana, machozi yakanitoka,
Hata lakufanya sina, ananiuma Rebeka,
Ninamuomba Rabana, amuadhibu Rebeka,

Denny Jeremias Kitumbika
Mufindi Tanzania
19.10.2024