Jamani mwezi wa pili nilitoa uzi kuhusu kutafuta babe, wakaja wengi wazuri. Loh, kumbe ni lichawi! Visa nilivyovipata mpaka niliamua kwenda kwenye maombi.
Akikupigia mkapigana usiku, unamuota kashika fimbo meaning anakuuliza, utanisamehe au hii fimbo inakuishia yote? Nasema nimekusamehe, nisipomsamehe ananichapa haswa au akipiga sijapokea ananiambia, unadhani sijakuona? Nimekuona umevaa hivi na hivi, walahi anakupa ishara fulani unajua alikuwepo.
Mara nyingine hadi na makofi anakupatia na yupo Dodoma mie Arusha, alifanya vitimbi hadi nikaona hapa ni maombi, nikaenda kwa msaada zaidi na mpaka sasa ameniacha.
Humu kuna watu ma Free Mason, nakumbuka alivyonikata tumbo nilipokataa kuonana naye ili tupate watoto, nikamjibu fuata utaratibu, si ndiyo lengo letu? Akadai utaona, we mida ya kumi na mbili kamili jioni nikaona kitu shaaa tumboni, mara uwazi tumboni, weh damu zote chini, kupelekwa hospitali ilikuwa inshu nyingine.
Waliona wakashona ila haiponi, kwenda hospitali nyingine ndiyo hivyo. Nikaona mzee wa ukoo anisaidie kwa hili nikapona.
Ila nilikwenda maombi, sasa hivi humu mie hapana!