Nilimruhusu msaidizi auze bidhaa zake ndogo ila zinamlipa kuzidi mshahara wake. Je, nifanye maamuzi gani?

Yani we jamaa, ni kama ikitokea umejenga fremu za biashara, then ukaona wapangaji wako wanapiga hela kuzidi kodi unayopata, utawafukuza ili hiyo biashara ufanye wewe, huwezi toboa namna hiyo mkuu maisha hayapo hivyo. Kwanza umesema biashara yake haifanani na yako, pia ulivyomkubalia, hamkukubaliana kwamba hatakiwi kufanikiwa sana. Unaumiaje roho mwingine kufanikiwa mkuu? Sio kwamba hii ndo itasababisha asikuibie?
Kama vipi mpe kiwango akuchangie kodi kila mwezi upunguze makali ya kodi ya fremu.
 
Ibn Unuq found this usefull
 
naingiza faida ya laki 3 hadi 4, Kabla biashara haijashuka ilikuwa ni Laki 8+
Biashara ilianza kushuka baada au kabla ya kumruhusu? Tuanzie hapa kwanza. Kama ni kabla, kumpunguzia kipato huyo jamaa hakutakuongezea wewe. Na kama ni baada, basi huenda biashara yake inahujumu biashara yako kwa namna moja au nyingine.

Sasa tukikuuliza maswali utujibie ili tuendelee kushauri. Au tuishie hapo? Kuna nondo kibao sijashusha bado.
 
Kuna jamaa yangu alikua mfanyakaazi wakiwanda Cha kutengeneza cosmetics akiwa na cheo kikubwa tu akawa na access yakuona formula zote zinazotumika kutengeneza cosmetics. Baada ya muda wa miaka 4 nae akaanzisha kampuni ya kuuza Chemical na kusaidia kuboresha cosmetics za watu wengine wanazotaka kutengeneza zilizo Bora. Boss alivyogundua alimfukuza kazi. Hali yakua mfanyakaz kasomea hayo mambo.
 
Hapa ni chura kapigwa teke, huwezi kuzuia watu kukua, kikubwa accept challenge, boresha mbinu so as to stay at the top of the game, wa kwanza ni wa kwanza siku zote.
 
Msaidizi wa kuuza bidhaa zako dukani unataka akuze biashara yako ?; Nadhani watu manachukulia biashara poa...., Kumbuka hii ni bongo ya madalali na wachuuzi, it's not rocket science (If she/he can do outstanding abaki hapo kwako anafanya nini..., unaongelea anakaa kama picha...., wewe picha za kwenu zinafanya mauzo.... au unalimpa pesa ya marketing na sales ?

In short kama ningekuwa na uwezo wa kuweka wauzaji kila kuna na wakaleta faida kwangu hata ya elfu hamsini ningewakusanya as many as possible wakanipatia hata hizo laki laki (leverage)...; ila hizo ni theory na biashara za kwenye vijarida ukija ground 90 percent ya biashara Bongo ni Debt trap ya watu kudumbukia kwenye madeni ya vikoba...., thus ukipata mtu ambaye bado anakuletea profit tena kwa wewe kumlipa pesa ndogo, that is an asset....; ukiona vipi unaweza kufukuza (Ila ndio hapo sijui utaacha unachofanya ili ukae mwenyewe au ujigawe mara mbili)
 
Mawazo ya watu humu hayatakusaidia zaidi wataona una roho mbaya.
Siku zote jipe muda na katika muda huo muombe Mungu akuongoze kufanya maamuzi huwezi jua unasaidia wangapi kupitia huyo uliyemuajiri, huwezi jua labda ni jaribu lako na Mungu anampango wakukupa kikubwa ili usaidie wengine.
Otherwise kama unauhakika 100% anatengeneza faida unaweza kumcharge % fulani kwa utakavyoona na wala sio dhambi maana hata kwenye dini kuna Zaka, Sadaka na fungu la kumi na nia mjinga atakayesema Mungu anawivu na roho mbaya kwa kuwwka sheria za matoleo
Kila la kheri
 
Ukiwa na scarcity mindset.. ni ngumu sana kutoboa..
Ni rahisi kuamini mwenzako wa karibu yako akipata wewe utakosa..
 
Kunjua roho mkuu,muache nae apate riziki kama hajaharibu kazi yako.
Ninadhani si kwa ubaya. Kumbuka hakuna biashara inayoingiza faida tu. Ni vema huyo mhudumu pia alipie gharama fulani,mfano,kodi na gharama nyingine ili kusaidiana eneo na biashara zao zidumu. Lengo lilikuwa zuri,kumsogeza ili na yeye abadili maisha. Kama biashara imekaa vizuri,si vibaya ikarudisha kiasi fulani kwenye fremu. Wala huyo tajiri asifikirie kuila au kumfilisi,wakae mezani wayajenge.

Tena dogo angekuwa muungwana anapaswa mwenyewe ajiongeze. Atazame kipi anaweza kukicover kwenye gharama za uendeshaji.
 
Mimi ninadhani awali ulikuwa na malengo mazuri na hata sasa bado una malengo mazuri. Ni uungwana unachofanya kutafuta namna bora ambayo haitamuumiza dogo.

Hakuna biashara inayofanywa na kuingiza faida tu. Kama umejiridhisha dogo anaingiza faida nzuri, basi biashara yake nayo iwajibike. Aone hapo dukani kipi atachangia katika gharama za uendeshaji. Anaweza kuchangia umeme,maji au sehemu ya kodi.

Hiyo inahitaji umakini ili pande zote msiumie. Ukilazimisha biashara zenu zitakufa.

Hapo sasa mtakuwa wote ni kama wamiliki,kila mtu atakuwa na uchungu wa kulinda hiyo mali.
 
Wale wale, halafu nyie wote ni wanawake!
 
So ww ulitegemea afanye biashara itakayomuingizia hasara au ni nini kinakusumbua sasa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…