Nilimshinda kwa hoja afisa usalama akaondoka kwa aibu

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Alhamisi mapema nikiwa job tukiwa tumepata taarifa ya msiba wa Rais Magufuli,tukiwa hatujui pa kushika au pakuachia alikuja afisa mmoja wa usalama kikazi.

Nikampokea nikasalimiana naye vizuri as usual. Ila siku hii hakuchangamka sana kutokana na taharuki ya msiba.

Nikamwambia kila kitu kitaenda vizuri kwani mama Samia yupo na ndiye atatawazwa kuwa Rais.

Akaniuliza , je, ataweza kuvaa viatu vya Magufuli?

Nami nikamjibu kwa kumuuliza maswali mafupi?

Nikamuuliza:
Je, akiapishwa si atakuwa Rais kamili?

Rais Magufuli alivaa viatu vya Kikwete?

Je, kuna ulazima wa Rais aliyeko madarakani kuiga au kuvaa viatu vya Rais aliyepita?.

Kama Kila Rais aliyeko madarakani ataiga mienendo ya Rais aliyepita huoni kuwa tutarudi miaka ya 1963 kipindi Nyerere anatawala?

Alikosa majibu akasema Magufuli aliweka nchi mbele. Nikamuuliza Samia ataweka nini mbele?.

Daaahhh sijui atakwenda kunichomekea huko aendako.

Atajua mwenyewe.
 
MATAGA wanaamini hii nchi haiwezi kwenda bila jiwe. Ni zamu yao kuteseka na kuweweseka. Kuna watu walijimwambafai kuwa wao ni watetezi wa jiwe, sasa kiko wapi?

Miaka 5 nimeteseka bila hata kuonewa huruma, hata kama aliyekuja hatabadili chochote ila kumbukumbu atakuwa nazo kwamba KARMA IS REAL AND IT PAY.
 
MATAGA wanaamini hii nchi haiwezi kwenda bila jiwe. Ni zamu yao kuteseka na kuweweseka. Kuna watu walijimwambafai kuwa wao ni watetezi wa jiwe, sasa kiko wapi?...
As long as ni CCM yetu ileile na sio lile genge la upinzani,kila kitu kitakuwa sawa tu maana sisi hatukuathirika moja kwa moja na utawala wa Magufuli.

Furaha yetu ni kuona kwamba kwanamna yoyote ile wapinzani hawakamati kabisa hii nchi, na hilo wazo linabaki kuwa ndoto kwao.

Kitakacho fanyika ni kuswitch upande tu Ili tuhamie kwa huyu aliyepo sasa.Tunawapa nafasi ya kujipendekeza kwasasa ila baadae najua mtarudi kwenye default mode.[emoji28]
 
Alhamisi mapema nikiwa job tukiwa tumepata taarifa ya msiba wa Rais Magufuli,tukiwa hatujui pa kushika au pakuachia alikuja afisa mmoja wa usalama kikazi...
Hata Magufuli hakuvaa "viatu vya Magufuli".

Kuna hadithi tu kwamba alivaa "viatu vya Magufuli".

Ukiichunguza sana hii hadithi utaona ina uongo mwingi zaidi ya ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…