Alhamisi mapema nikiwa job tukiwa tumepata taarifa ya msiba wa Rais Magufuli,tukiwa hatujui pa kushika au pakuachia alikuja afisa mmoja wa usalama kikazi.
Nikampokea nikasalimiana naye vizuri as usual. Ila siku hii hakuchangamka sana kutokana na taharuki ya msiba.
Nikamwambia kila kitu kitaenda vizuri kwani mama Samia yupo na ndiye atatawazwa kuwa Rais.
Akaniuliza , je, ataweza kuvaa viatu vya Magufuli?
Nami nikamjibu kwa kumuuliza maswali mafupi?
Nikamuuliza:
Je, akiapishwa si atakuwa Rais kamili?
Rais Magufuli alivaa viatu vya Kikwete?
Je, kuna ulazima wa Rais aliyeko madarakani kuiga au kuvaa viatu vya Rais aliyepita?.
Kama Kila Rais aliyeko madarakani ataiga mienendo ya Rais aliyepita huoni kuwa tutarudi miaka ya 1963 kipindi Nyerere anatawala?
Alikosa majibu akasema Magufuli aliweka nchi mbele. Nikamuuliza Samia ataweka nini mbele?.
Daaahhh sijui atakwenda kunichomekea huko aendako.
Atajua mwenyewe.