Nilimshirikisha mama yangu mafanikio yangu nikadhani amefurahi, baada ya muda kila nikiwasiliana naye ananiambia isijekuwa naenda kwa waganga

Bora wamekuhisi mchawi unaweza kuwaelewesha hata kwa kwenda kuombewa kudhibitisha.

Siku hizi watu wakikuona una mafanikio wanasema unaliwa kinyewo. Sasa namna ya kuwadhibitishia huliwi ndio shida yenyewe....
Ukionekana na washkaji zako wanakuambia ndio mabasha wake.

Ila pole sana.
 
Acha tu ndugu yangu hii nchi inanukaa laana ya mafanikio ukipata kidogo tayari mchawi
 
Nakuelewa unayopitia kiongozi,niseme POLE..jaribu kumshirikisha kiongozi wa Kiroho,mueleze ulichokifanya upande wako,kauli za mama ,na unavyojisikia...

Mama ataitwa na utapata wasaa mpya wakumuelewesha, na kiongozi wa kiroho atamuonya mama kwa hayo akuneneayo,na naamini mama atabadilika
 
Kwakweli umenishauri jambo kubwa sana mkuu natafanya hivyo
 
Asante sana mkuu, imebidi nionane na ile kampuni ya betting tumekaa chini tukaongea sana kwakweli wamesikitika sana wakanambia sina bahati ya mama, nimezaliwa familia mbaya
Mchukue Mama yako mpeleke Mwenye hiyo Kampuni aonane na maofsa wa hapo wamueleweshe. Usichukie na wala usdharau wasiwasi wa Mama yako, yeye kama mzazi ana wajibu huo
 
Mchukue Mama yako mpeleke Mwenye hiyo Kampuni aonane na maofsa wa hapo wamueleweshe. Usichukie na wala usdharau wasiwasi wa Mama yako, yeye kama mzazi ana wajibu huo
Sitampeleka namsubiri atapike maneno yote machafu ili nijue nina mama wa aina gani kisha badae nifunge kitabu kwa kuthibitisha na kumpa mgongo ili Mungu amlipe, haiwezekani mimi naishi maisha ya kumcha Mungu leo nalipwa kuitwa mtoa kafara
 
Mama hana makosa....ni wewe kichwa maji umeshindwa kuwaaminish chanzo cha pesa zako

Unavyosema una mama mbaya unazidi kumkosea Muumba....angekuwa hakupendi angekuminya kwenye mapaja siku anakuzaa...

utalaanika wewe
 
Yawezekana kweli umeanza mambo ya manyoka,maana ingekua umeshinda kwa betting si evidence zipo na ungewaonyesha naamini ata JF usingeandika
Ni sahihi fanilia kuwa hofu maana umefanya ghafla na wanajua wewe ni kapuku inawezekana huna chanzo kizuri cha kipato ndio maana wameanza kupata hofu
 
Mama yako hakupendi wakati amekukuza mpaka ukawa mkubwa ? Au unadhani zamani abortion hazikuepo? 😂😂

Huyu jamaa anatafuta kuonewa huruma tu au anatafuta attention sasa mzazi wako kuwa na hofu na chanzo chako cha mapato kuna ubaya gani ? We mwanao wa darasa la tano akienda shule akarudi baiskeli utamwelewa ?

Ndo hawa wazazi mtoto anarudi nyumbani anasema ameshiba au ashakula na wewe unamchekea!

Sema chanzo chako cha mapato usiseme ulibet , sema ulicheza kamali ndo watakuelewa kirahisi 😂😂
 
Exactly
 
✍️Nilipokea simu Dr am 4 real PhD naomba nisaidie Kodi japo ya mwezi mmoja @35,000

Pale buguruni uswaz ndani ndani wanapokea Kodi za mwezi mwezi Ni ndugu zangu wawili na nilikua na access ya kuwapa lakini nikawakazia nikaona wamezidi KUOMBA omba...

Aisee mungu sio athumani there after jamaa mwaka ulio fuata jamaa akapata connection za biashara now ana ginnery, analima mashamba makubwa makubwa kwa trekta, anamiliki magari Zaid ya kumi ana nyumba za maana kwenye majiji yote muhimu..

Hana Elimu yoyote ya maana Wala professional yeyote Ila ana akili ya pesa na pesa imejaa anaitwa Freemasons wallah mzee izo Mambo Ni real..

Mungu akiamua kuku bless hakuandikii barua..
 
Wewe umeamuaje?, ukiwa mjinga utarudi kwenye zero waache na ujinga wao betting haikupi pesa kila mara uenda ndo bahati yako kilichobaki tafuta pesa ya Kula na kuvaa wewe sio kama wengine wasio na hata Banda la kulala kila siku wanakimbia Kodi ya chumba. Umeipata mwanzo mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…