Nilimshirikisha mama yangu mafanikio yangu nikadhani amefurahi, baada ya muda kila nikiwasiliana naye ananiambia isijekuwa naenda kwa waganga

Basi naomba odds 5 za haraka mkuu
Ilitokea tu kama bahati lakini siri ya kifanikiwa ni kudeal na timu zenye historia ya kueleweka sio kila mechi ya kuweka dau, angalia mechi ambazo hata ww mwenyewe akili inakwambia mchezo utaendaje, usifanye kwa ulevi zingatia sio kila mechi ya kuweka dau, soma historia ya team na wachezaji wake kuhusu ufungaji wao ukoje kwenye mechi zao
 
Kama Kaka yako anasali kwa Gwaji boy,huyo ndiyo kamumpa sumu mama yako,wengi wanaosali pale wananapoteza uwezo wa kufikiria,nikama wapo gizani nina mifano kadhaa
 
Ila wee jamaa ni mchawi yaan umemkula muhindi mpk umeshusha mjengo ulikua na odds ngapi masta
Mkuu siyo uchawi,nina jamaa yangu amemjengea nyumba mama yake Dodoma na nyingine anapangisha kwasababu ya betting........anamtaji timu tatu anaweka Laki siku akila anakula mzigo hasa,akiliwa analiwa kweli kweli,so kupanga ni kuchagua
 
Kama Kaka yako anasali kwa Gwaji boy,huyo ndiyo kamumpa sumu mama yako,wengi wanaosali pale wananapoteza uwezo wa kufikiria,nikama wapo gizani nina mifano kadhaa
Hakuna wanachofundishwa pale zaidi ya kuzimu na uchawi familia zote nyingi za walokole wa pale zimesambaratika kwa maneno yake
 
Mkuu siyo uchawi,nina jamaa yangu amemjengea nyumba mama yake Dodoma na nyingine anapangisha kwasababu ya betting........anamtaji timu tatu anaweka Laki siku akila anakula mzigo hasa,akiliwa analiwa kweli kweli,so kupanga ni kuchagua
Na huyo inamana amekula pesa nyingi wala simfikii hata kidogo watu wamefanikiwa sana na betting ninwatu tu hawajui
 
Pole Sana mkuu.....
 
Wewe na wewe ni dalali wa betting. Kwamba watu wakitaka pesa waende kubet jambo ambalo kwa kweli ni kubahatisha na mara nyingi uwezo ni kufilisiwa na wachezeshaji wa betting. Mama yako kukuita mchawi ni sawa maana mambo ya kucheza kamari hayana mwisho mzuri. na ndio maana hata vitabu vyote vya dini yamekatazwa.
 
Niliyemweleza ni mama yangu, kwanza kabisa kitendo cha yeye kuthubutu kunipakazia maneno ya laana kama haya tayari nina mama mbaya
Je amekuelewa ulichomueleza?
 
Baada ya kupata ile hela sikurudia tena ndo mana nikawashauri vijana wenzangu wawe na kiasi, wasicheze kwa ulevi
 
Kwenye mambo nyeti ni marufuku kumwambia ndugu wewe uliamua iwe siri ukawashwa kuwaambia ndo malipo yake hayo

Mama yako inawezekana hakutegemea kufanikiwa kwako kabla ya ndugu yako, hii kwenye familia huwa inaleta shida sana wazazi kubagua watoto kuna yule anaeonekana anastahili mafanikio na mazuri yote na kuna kina kabwela sasa ikitokea kabwela akapata huibua migogoro mikubwa hata kupelekea kuvunja familia
 
Sasa hivi kaelewa aliyekuwa akimfundisha ni kaka mlokole na ndiye aliyeharibu ile familia kwa habari za uchawi
Nilijua tu kaona ulokole wake haujampa miujiza, wivu tu heri rafiki kuliko ndugu aisee
 
Nilijifunza kitu, lakini nilifanikiwa kuwapiga marufuku kwa kuwawekea mpaka na nikawapa onyo wasinisogelee na ujinga wao, kama wanataka kuwa rafiki yangu waache upuuzi kinyume na hapo wasinisogelee
 
Hakuna mzazi atafurahi kuona ghafla bila kufanya kazi yoyote, kijana wake ana majumba, hakuna hakuna, you should involved her earlier!
 
Shida ni wewe wala si wao. Wanakufahamu vema, wanajua gharama za ujenzi, lilikuwa jukumu lako kuwaeleza kila kitu kuhusu hizo fedha. Wanakujali sana tofauti na ulivyo chukulia
 
Shida ni wewe wala si wao. Wanakufahamu vema, wanajua gharama za ujenzi, lilikuwa jukumu lako kuwaeleza kila kitu kuhusu hizo fedha. Wanakujali sana tofauti na ulivyo chukulia
Kama ningeanza kuwambia nimeshida sio ajabu wangesema niwagawie, nashkuru nimezifaidi mwenyewe mana hawajawahi kunijali hapo awali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…