Nilimsomesha mpaka chuo lakini bado wakataka kunimaliza yeye na mama yake

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
Wakati mimi namlipia ada ya chuo, kuna mwingine alikuwa anamsaidia kujenga kwao. Kumbuka, nilishajitambulisha kwa mama yake, ambaye alikuwa anajua kila kitu – kwamba binti yake hana kazi yoyote, lakini alikuwa anahudumia familia na kusomesha wadogo zake.

Mimi sikuwa nikijua hilo mpaka alipomaliza chuo, nikawa nataka kumuoa kumuoa. Akaanza kunizungusha kwa kisingizio cha kwanza apate kazi, mara anataka kusaidia ndugu zake, na mambo mengine mengi. Mwanzoni nilimuelewa, kwa sababu kama unatoka katika familia za kimaskini ni kawaida kusaidia ndugu zako.

Lakini baadaye niliona kama kuna kitu hakiko sawa. Nilipoanza kufuatilia, ndipo niligundua kwamba mahali aliponipeleka na kuniambia ni kwao, kumbe ni kwa mama yake mdogo. Hakunipeleka kwao kabisa, kwa sababu alikuwa anajengewa na huyo mwanaume hakutaka nione hiyo nyumba.

Pia, mama yake alikuwa anajua yote haya na alikuwa ananipanga. Wakati mwingine alikuwa ananipigia simu kuniomba hela, huku akijua tabia za mtoto wake. Mama yake alifurahia hali hiyo, na ndiye aliyekuwa anamshauri kuhusu kutokufunga ndoa nami.

Nilipogundua hili, nilimuuliza, ndipo akaanza kunijibu vibaya, akanitukana, na kunifanyia vituko. Aliniambia: "Kama Vipi? Tuchane! Hela gani umenipa?" Mimi nikaendelea kubembeleza kulinda penzi, lakini baadaye mwanamke alikataa kabisa. Nikaamua kutafuta rafiki zangu wawili na kwenda kwao na barua ya kishika uchumba, nikisema nataka kumuoa.

Nilikuwa tayari kusamehe kila kitu ili awe mke wangu. Siku hiyo, hakuna rangi niliyoacha kuona. Mama yake alinitukana sana na kuniambia maneno ya ajabu. Alinitisha maisha, akisema: "kaa mbali na binti yangu, utamharibia maisha!" Nilifukuzwa kama mwizi. Mama alikuwa mkali sana. Niliondoka pale nikilia, kwa sababu kwa binti huyo niliwekeza sana.

Hata yule binti mwenyewe aliniambia hanitaki tena, kwa sababu nimesababisha aibu, na mama yake alikuwa amemwambia asiwahi kuwa na mawasiliano nami tena. Rafiki zangu walinishauri niachane naye kabisa, na hivyo nikaamua kuendelea na maisha yangu.

Baada ya miezi miwili, nikiwa najua mambo yameisha, nilikuwa zangu nyumbani na sikutegemea chochote. Ghafla, nilisikia mlango unagongwa. Nilipoenda kufungua, nilipig*wa na kitu kizito kichwani. Baada ya hapo, sikumbuki kilichoendelea mpaka nilipozinduka hospitalini baada ya siku tano, nikiwa nimelazwa.

Kila mtu alidhani nimeshaku*fa. Walinip*iga sana, hadi kunivunja mbavu na mguu. Nilikaa hospitalini kwa miezi miwili. hawakuchukua chochote. Hata hivyo, nilianza kujiuliza ni kwa nini walinivamia wakati sina mali nyingi wala hela ya maana.

Niliporudi nyumbani, siku moja nilipokea simu kutoka kwa Kaka wa aliyekuwa mpenzi wangu. Alinisalimia vizuri na kuniuliza hali yangu. Aliponisikia, akaamua kunipa taarifa: "Ondoka Tanga! Hivi kilichotokea si wizi, bali ni mama na dada walipanga kila kitu. Mama alimwambia dada kwamba hela ulizotoa huwezi kumuacha kimya, utaharibu penzi lake. Kwa hiyo, lazima wakuon*doe. Najua hujamfanyia kitu kibaya, lakini mama yangu ndiye anayemwendesha dada. Ondoka mbali nao, kwa sababu wanapanga kuku*ua."

Alimaliza kwa kusema: "Nikikwambia haya, usinitaje ukilalamika polisi. Nikitajwa, nitakukataa, siwezi kwenda kinyume na mama yangu." Nilichukulia maneno haya kwa utani, lakini baada ya wiki moja, mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, akisema anataka kuniona na kuuliza hali yangu. Nilimuambia niko sawa na namshukuru Mungu.

Hata hivyo, kwa sababu nilishuku nia yake, nilimdanganya kwamba bado niko Tanga, mahali nilipovamiwa. Usiku huohuo, chumba changu cha zamani kilivunjwa, lakini kwa bahati nzuri hakukuwa na mtu ndani. Wakati huo, ndipo nilijua wazi kwamba aliyepanga haya yote ni yeye pamoja na familia yake.

Nilihama kabisa na nikaacha kazi yangu, kwa sababu kampuni yenyewe ilikuwa binafsi. Mpaka leo, hajui niko wapi. Lakini akiona ujumbe huu, atajua kwamba najua kila kitu alichonifanyia, najaua nakusoma kwani mara nyingi namuona kikoment kujifanya mtu mwema nimeamua kuandika kwakua nimeshasamehe na nina Aman
 
Pole kwa majanga mkuu, lakini humu jukwaani kila siku wadau wanasema wanaume msisomeshe wanawake ambao amjazaliwa tumbo moja lakini wakulungwa amtaki kusikia kabisa jamani wanaume wenzangu embu tubadilike tafadhali.
 
WE JAMAA NI MJINGA SANA NA HUJA HAJA YA KUONEWA HURUMA, USHAAMBIWA HAKUNA KUSOMESHA MWANAMKE ASIE MKEO TATIZO LA BINADAMU HUWA TUNAAMINI YANAYOWATOKEWA WALIOTOA USHUHUDA WEWE HAYAWEZI KUKUKUTA, HAWA WANAWAKE ALMOST WOTE NI WALEWALE.

Bwana mdogo mwanamke kama hakutaki achana nae ,na bora wangekuvunja mguu akili ikukae sawa
 
Bazinkulu m.ke hasomeshwi wacha wazazi wake wapambne wanavojua
 
Back
Top Bottom