Niliokoka nikiwa peke yangu chumbani usiku tena ugenini

Ilikuwaje Mtumishi?

Ilikuwaje Mtumishi?
Siku ya tatu kulikuwa na harusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo, naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, β€œHawana divai!” Yesu akamjibu, β€œMama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado.” Hapo mama yake akawaambia watumishi, β€œLolote atakalowaambieni, fanyeni.” Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha. Yesu akawaambia, β€œIjazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu. Kisha akawaambia, β€œSasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.” Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi, akamwambia, β€œKila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!” Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya
 
Hongera sana brother, neema ya wokovu iendelee kuwa juu yako, endelea kusambaza nuru uliyoipokea.
 
Nimeliwaza sana hili akikujibu nitag tafadhali.
Kuna wakati nilifanya ujasusi wa kuwafahamu haters wangu hapa JF.. Nilikutana na baadhi yao bila wenyewe kujua.. Wote walikuwa ni watu waliopigika hasa kimaisha na wenye kila aina ya mahangaiko.. Niliishia kuwaonea huruma sana
 
Asante kwa andiko lenye mafunzo mengi
 
Kuna mada flani unasema uliingia kanisani ukapigwa vibration, lilikuwa kanisa gani na ulifanya nini?Huo "uumbaji" unaosema uliutesa ni kwa namna gani na ulikikosea nini, na hatma yao ikoje baada ya wewe kuuza kilinge?

(Once a witch, always a witch)
 
Kuna mada flani unasema uliingia kanisani ukapigwa vibration, lilikuwa kabisa gani na ukifanya nini?Huo "uumnaji" unaosema uliutesa Ni kwa namna gani na ulikikosea nini, na hatma yao ikoje baada ya wewe kuuza kilinge?

(Once a witch, always a witch)
Tazama ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya.. Bwana wa majeshi asema.. Ijapo dhambi zako zitakuwa nyekundu Kama bendera yeye atazisafisha ziwe nyeupe Kama theluji.. Tunaokolewa na kukombolewa kwa neema tuu
 
Tazama ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya.. Bwana wa majeshi asema.. Ijapo dhambi zako zitakuwa nyekundu Kama bendera yeye atazisafisha ziwe nyeupe Kama theluji.. Tunaokolewa na kukombolewa kwa neema tuu
Kufafanua mabaya uliyotenda ni sehemu ya kujitakasa, watu waone ubaya wa shetani na uzuri wa Yesu, kufichaficha ni ishara mbaya

Sio kila uchawi unasamehewa. Uchawi unaendana na makufuru mabaya yanayoambatana na ukatili wa kunywa damu za watu, pia unaingia mkataba na shetani wa kumuuzia roho yako ili yeye akupe nguvu na mali, halafu simply unasema umeokoka, unamdanganya nani

Au unataka kuanzisha kanisa la miujiza ya kichawi
 
Kuna wakati nilifanya ujasusi wa kuwafahamu haters wangu hapa JF.. Nilikutana na baadhi yao bila wenyewe kujua.. Wote walikuwa ni watu waliopigika hasa kimaisha na wenye kila aina ya mahangaiko.. Niliishia kuwaonea huruma sana
ulimtembelea Kiranga na Nyani Ngabu ? kuna post niilisoma somewhere wanakwambia kama kuna uchawi wamekuruhusu uwaloge uko walipo ukashindwa it's true?
 
Nilishatubu kwa Mungu wangu hata nikisimulia hapa haina maana yoyote. Kwakuwa nawasilimulia watenda dhambi na pengine wabaya na wachafu kiroho kunizidi nilivyokuwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…