Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Niseme wazi. Mimi ni mhanga wa mabadiliko yaliyotokea pale Raisi Magufuli alipoingia madarakani. Nilikuwa nikifanya kazi nje ya nchi kama mtaalamu katika sekta fulani. Nikaambiwa taasisi fulani ya serikali hapa nchini ilihitaji watu kama mimi. Nikaomba nafasi hiyo ili nirudi nchini kutumikia nchi yangu.
Hiki kikawa kipindi cha uchaguzi. Na katika mchakato wa kuajiriwa nafasi niliyoomba, nikatokea kushika nafasi ya kwanza. Ikawa majina yapelekwe Ikulu kwa uteuzi rasmi, na yakasubiri Raisi Magufuli afanye huo uteuzi baada ya kuapishwa.
Kuna viongozi walionifahamu, baada ya kuona Raisi Magufuli amekuwa raisi, walinisihi sana nisirudi nchini na niendelee na kazi yangu huko nje ya nchi. Wakati huo sikuwaelewa kabisa, nikawa mbishi kwamba mie nitarudi nchini kutumikia taifa langu. Wakaniambia utajuta, kwa kuwa tunakufahamu silka yako, na Magufuli hawezi kuwa na mtu kama wewe mwenye kusema mambo waziwazi bila kuogopa.
Na ni kweli nisingemuogopa Magufuli bali kumheshimu, kwa kuwa katika kazi yangu nimekutana na maraisi wa kila aina kwa ukaribu kabisa, kwa hiyo huwa nawaheshimu, sio kuwaogopa, na kwangu spedi inabaki kuwa spedi.
Hata hiyo, labda kama kinachoitwa baraka zilizojifricha (blessing in disguise), Magufuli alipopewa yale majina matatu afanye uteuzi, aliyatupilia mbali yote. Aliamuru recruitment agent alipwe na yeye ndie atafanya uteuzi. Akaamua kuweka mtu wake kutoka kanda fulani katika taasisi hiyo bila hata kufuata uratatibu wa kuajiri kulingana na Act iliyounda shirika hilo. Huyo mtu amekuja kuondolewa baada ya raisi Samia kuwa raisi.