Niliona ni ujinga kwa mtumishi kutokuwa na "savings" sasa yamenikuta ya niliokuwa nawatukana

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,647
Reaction score
9,604
Wakati nipo mtaani nasaka ajira naona washakaji na watu wengine na kazi zao nzuri tuu ila wana madeni sana. Wapo ambao wakipatwa na shida tuu utasikia wanalalamika hawana hela ya akiba kutatua shida zao. Kila siku kukopa tuu.

Sasa nimeajiriwa mwaka wa nne sasa maisha yananipeleka puta balaa napata mshahara unapukutika hata siuelewi. Changamoto za hapa na pale kama misiba, kuuguliwa, kodi, ada, kutunza wazazi, matunzo ya familia yaani mshahara ukitoka sina amani. Nikiweka akiba ikifika kiasi fulani napata dharura inanikalia kooni inatumika yote nabaki kwenye 0.

Sijawahi lala njaa kwa sababu ni mkopaji mzuri na narejesha kwa wakati marejesho naogopa madeni, nikisema nitalipa tarehe fulani hiyo ni uhakika sina longo longo.

Wife nimemfungulia biashara kidogo ahangaike naye ila bado haijakaa sawa japo ni mhangaikaji sema hali ya biashara haijawa poa.

Saving sio mchezo na ukiona mtu ana madeni usidhani kuwa ni mzembe sana. Saving ni mbinu na commitment ya hali ya juu.

2021 nimebuni mbinu I hope nitasimama.
 
Kabla ya kuanza saving jitahidi utengeneze bajeti ya matumizi yako yaani mfano kwa mwezi kadiria hauzidi elfu moja simamia hilo usizidi elfu moja fanya hivyo kwa miezi 10 hapo utakua umefanikiwa.
 
Watu maskini ndio wanaongoza kwa kuwa na huruma na ndio maana wanabaki pale pale.


Fanya commitment ya ku-save kidogo then nyingi.
 
Dogo wewe Jikite kwenye kufanya kazi
 
muda mwingine jifunze kuwa bahili, sio kila kitu unanunua au ukiambiwa tu unatoa hela

Limit baadhi ya matumizi yako hasa yasiyo ya lazima
Ubahili nacho ni kipaji ...na kwa zama za yule bwana ...inabidi kuachana na unnecessary spending...,Inashangaza Sana mtu katoka kula anaagiza juice na maji at the same time ...ni kitu kidogo ila impact ni kubwa ..na kwa hawa watumishi mambo ya kutoana sijui lunch huko ndo pesa zinapotea Bila taarifa unastukia ...huna saving unaanza kuishi Kama mnyama
 
Ndio mkuu
 
Fanya ufanyavyo lakini jitahid u save hata kidogo mkuu haya maisha hayatabiriki jitahidi sana nakusihi mkuu
Ushauri mzuri, ila nyongeza, jitahidi ubuni kitu cha kukuingizia kipato kuboost salary yako..utafika mahala kipato kitazizi matumizi ya lazima. Kinachozidi, ndicho usave. Na unachosave,ndicho ukitumie kupanua zaidi kipato. At the end of the day, ndo Ubakheresa tiyari!
 
Ukiwa umeajiriwa na una mshahara chini ya 1m inabidi uwe makini mnoo kwenye matumizi coz ...Ajira nje ya serikali ...hazitabiriki siku hz makampuni kibao yanapunguza wafanyakazi kwa kisingizio cha corona ..Yan kama Sio mtu wa budget kufanikiwa itakua ndoto tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…