Niliona ni ujinga kwa mtumishi kutokuwa na "savings" sasa yamenikuta ya niliokuwa nawatukana

Niliona ni ujinga kwa mtumishi kutokuwa na "savings" sasa yamenikuta ya niliokuwa nawatukana

Kwenye madeni hapo umenifurahisha mwaka Jana nilikuwa na madeni mpaka napauka sura.
 
Ubahili nacho ni kipaji ...na kwa zama za yule bwana ...inabidi kuachana na unnecessary spending...,Inashangaza Sana mtu katoka kula anaagiza juice na maji at the same time ...ni kitu kidogo ila impact ni kubwa ..na kwa hawa watumishi mambo ya kutoana sijui lunch huko ndo pesa zinapotea Bila taarifa unastukia ...huna saving unaanza kuishi Kama mnyama
Mkuu usiwashitue watumishi ndo wateja wetu tutakosa pa kuwapigia.
 
Wakati nipo mtaani nasaka ajira naona washakaji na watu wengine na kazi zao nzuri tuu ila wana madeni sana. Wapo ambao wakipatwa na shida tuu utasikia wanalalamika hawana hela ya akiba kutatua shida zao. Kila siku kukopa tuu.

Sasa nimeajiriwa mwaka wa nne sasa maisha yananipeleka puta balaa napata mshahara unapukutika hata siuelewi. Changamoto za hapa na pale kama misiba, kuuguliwa, kodi, ada, kutunza wazazi, matunzo ya familia yaani mshahara ukitoka sina amani. Nikiweka akiba ikifika kiasi fulani napata dharura inanikalia kooni inatumika yote nabaki kwenye 0.

Sijawahi lala njaa kwa sababu ni mkopaji mzuri na narejesha kwa wakati marejesho naogopa madeni, nikisema nitalipa tarehe fulani hiyo ni uhakika sina longo longo.

Wife nimemfungulia biashara kidogo ahangaike naye ila bado haijakaa sawa japo ni mhangaikaji sema hali ya biashara haijawa poa.

Saving sio mchezo na ukiona mtu ana madeni usidhani kuwa ni mzembe sana. Saving ni mbinu na commitment ya hali ya juu.

2021 nimebuni mbinu I hope nitasimama.
Rich dad,poor Dad
 
Back
Top Bottom