Nilionya mapema hapa JF asianze Kipa 'mbovu' Aishi Manula, naona 'Mnanipuuza' hivyo leo tusilaumiane kwa 'Kipigo' akidaka Yeye

Mimi nafikiri mechi ya leo inamhusu zaidi Ali Salim. Ayoub kwa mechi chache alizocheza amefanya makosa mengi kiufundi kiasi angekutana na timu zenye washambuliaji hatari nafikiri Simba mwaka huu ingeyasikia makundi kwenye redio. Manula naye kukosa mechi za mashindano mfululizo ni hatari kucheza mechi ya leo na hasa ukizingatia ametoka kuwa majeruhi na kama benchi la ufundi likiamua kuanza naye basi hiyo wameamua wao kiroho safi kucheza kamari/kubet. Na wote tunajua na hata benchi la ufundi linajua vizuri sana kwenye kamari/kubet kuna aidha kula au kuliwa.

Ni mtizamo tu
 
Ayoub hata ukimleta Kayengeyenge FC yetu nakuhakikishia hapati namba,

Yule aendelee kula mshahara wa Bure TU na kugawana na walio mleta kakini hakuna kipa pale.
 
Ayoub hata ukimleta Kayengeyenge FC yetu nakuhakikishia hapati namba,

Yule aendelee kula mshahara wa Bure TU na kugawana na walio mleta kakini hakuna kipa pale.
Anaejua ufit wa mchezaji ni kocha wa makipa na kocha Mkuu ambao sikuzote wapo pamoja mazoezini. Hii mihemko yetu ya kishabiki. Inatusumbua bila sababu. Golini akipangwa Kipa yeyote ni sawa tu. Popoma Dua za waarabu zishamvuruga
 
Simba wakianza kufunga dakika zamwanzo kabla ya 20..al ahly hawawez kurudisha hadi mpira unaisha.
Wapambane vizuri tu madunduka.
 
Umeanza kuweweseka. Unatafuta sababu mapemaaa za jinsi ya kujitetea..!!
 
Sasa mnataka adake nani? Wote mlisema hawafai...... kama vp nenda kadake ww.
 
Popoma una mpangia kocha cha kufanya hapo ulipo hata leseni ya ukocha hauna wew kweli imbecile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…