Mimi nafikiri mechi ya leo inamhusu zaidi Ali Salim. Ayoub kwa mechi chache alizocheza amefanya makosa mengi kiufundi kiasi angekutana na timu zenye washambuliaji hatari nafikiri Simba mwaka huu ingeyasikia makundi kwenye redio. Manula naye kukosa mechi za mashindano mfululizo ni hatari kucheza mechi ya leo na hasa ukizingatia ametoka kuwa majeruhi na kama benchi la ufundi likiamua kuanza naye basi hiyo wameamua wao kiroho safi kucheza kamari/kubet. Na wote tunajua na hata benchi la ufundi linajua vizuri sana kwenye kamari/kubet kuna aidha kula au kuliwa.
Ni mtizamo tu
Ni mtizamo tu