Mkuu,
Kwanza, pole sana kwa changamoto yako. Vizuri umetambua kuwa afya yako ni muhimu na hutorudia kuparamia. Chukua tahadhari.
Pili, Alcef na powercef zote ni dawa moja. Kiambata kilichopo ni Ceftriaxone. Daktari wako wa pili sikuona haja ya kukuandikia tena powecef endapo tu ulishadungwa alcef. Ila kwa kuwa haina athari, basi si mjadala wa maana. Au pengine, kwa kuwa ulitumia muda mrefu kidogo, akaona vema akuandikie.
Tatu, umesema dawa umetumia Jumanne. Maana yake leo ndiyo siku ya tatu. Unataka matokeo ya haraka mno ndugu. Ufanisi wa dawa kuleta matokeo ya haraka hutegemea sana ukali wa kimelea, reaction ya mwili kwa dawa na usugu wa kimelea chako.
Siku tatu ni chache sana kukata tamaa juu ya ufanisi wa dawa. Kama husikii maumivu, kilichobaki ni usaha tu basi kuwa na subra Mkuu. Mategemeo siku 5 na kuendelea.
Nne, kama una wasiwasi sana inakupasa urudi kufanya kipimo upya. Ijulikane aina ya bakteria na sensitivity yao. Ili kuweza kujua dawa gani italeta matokeo kwa haraka.
Tano, kuwa mtulivu. Kama umeshaenda kupata dawa basi tulia tumia dozi vizuri ukisubiri matokeo. Usiwe na pupa ya kurukia kila dawa. Hapo pengine unapanga kwenda kwa mtaalam mwingine. Hebu vuta muda ukisubiri kidogo.
Nakutakia uponyaji mwema.