NILIPOKUA Mkoa X nikapatiwa Dawa ya Maajabu kwa ajili ya Matibabu ya Haraka, Nikapona

NILIPOKUA Mkoa X nikapatiwa Dawa ya Maajabu kwa ajili ya Matibabu ya Haraka, Nikapona

Nilipokua Mkoa X Mwaka Z, ghafla tu nikaanza kuumwa ugonjwa fulani siuelewi ulipotokea mpaka nikaanza kuhisi labda nishapigwa kipapai au namna gani vile maana ule Mkoa unasifika kwa hayo masuala ya kuroganarogana tu, usiku hakulaliki mchana hakukaliki na haakutembeleki baridi sio baridi joto sio joto.

Hangaika za hapa na pale huku na kule, doh nikajiona kwamba kweli nilivyo mimi siamini habari za kwenda hospital sana maana nilishawahi kutibiwa tofauti na ninavyotaka mimi nikazunguka hospital zote zaidi ya 5 hawaoni ugonjwa wala hawaelewi naumwa nini mwisho wakaniambia nikapigwe CT Scan eti wauchunguze mwili wangu una tatizo gani kumbe hata haihusiani na nilichokua naumwa, kuanzia hapo nikazima data huniambii kitu kuhusu habari za kwemda hospital naziamini sana pharmacy zaidi kuliko hospital.

Basi huku na huku chukua dawa hii ya kifua toka pharmacy hii changanya na dawa ile ya mafua kutoka pharmacy ile meza subiri labda utapona aah wapi dawa zimekataa imegoma kufanya kazi, nikitegemea hali itakaa sawa ila waaapi mambo yakawa yanzidi kua magumu, siku ya 2 mpaka ya siku 5 nikawa sasa tayari mgonjwa totally on bed nipo hoi bin taaban kitandani mbele sioni wala kutembea ni kwa tabu kizunguzungu muda wote mdomo mchungu pua ni za moto macho yanawaka moto kuona vizuri siwezi nipo kitandani tu najihisi kufakufa, sasa hapo ndio nikawasha taa nyekundu, nimesha-surrender mikono juu km nimekamatwa mateka yaan nataka kukabidhi ubingwa nikaomba ndugu wanipelekwe hospital hata kwa kubebwa juu ya machela itafahamika huko huko nisipotibiwa basi nifie huko huko kuliko kufia nyumbani kizembe.

Kabla sijapelekwa hospital maajabu yanayokea, kuna mtu wangu mmoja wa karibu aliwahi pharmacy moja iliyopo mbali kidogo na sisi tulipo, haraka sana kwa mtu anaemfahamu na anasimamia hio pharmacy, akaenda kujielezea pale mimi ninaumwa nini nimeanza muda gani kuumwa hali yangu ilivyo na hua ninatumia nini? akamuelezea vizuri kabisa yule Nesi mphamasia alipomsikiliza vizuri yale maelezo yake akamuelewa akafanya jambo la maajabu kumtibu mgonjwa alielala nyumbani ambae hujamuona umepewa tu maelezo, akachomoa dawa za maajabu, ndipo nilipopatiwa dawa za maajabu ambazo sikuwahi kuzitumia ila niliandikiwa tu dawa hizo hapo meza nilipomeza tu yaan huwezi amini ila nilipona ndani ya muda mfupi sana huwezi amini km ndio mimi niliekua naumwa vile.

Hizo dawa nikiumwa tena hata leo/kesho/kesho kutwa nikienda kununua tu pharmacy nikafanya COMBINATION paap nikimeza tu shwaaapu, nilichokua naumwa chochote iwe mafua sijui kifua sijui kichwa sijui maumivu yawe ni madogo au makubwa ya mgongo sijui miguu sijui kifua, vyote kwisha kazi, yaan sisikii kitu chochote na zinakua tamu zaidi niki-ovadozi.

Bad news ni kwamba nimetengeneza Addiction maana sasa siwezi kuwacha na zenyewe haziwezi kuniwacha. Nikiziwacha tu maumivu ninayoyapata sio ya dunia hii naumia, kwa hio kwa usalama wangu kiafya na maumivu ninayoyapata inabidi niendelee tu kuzitumia. Nikiacha kuzilumia naanza kuunwa mavitu ya ajabu ajabu nikichukua zile dawa zangu nikatumia moja au nikafanya COMBINATION chochote nilichokua naumwa kinaacha mara moja shwaaaa.

Sasa Nipo Mkoa Y bado nazitumia nikiacha tu naumwa vibaya sana, kwa hio inabidi niendelee tu kuzitumia.

Ps: Ni dawa za Maumivu. Tafadhari sana naomba usiniulize jina la dawa 'cause that's my Classified Information. Hamchelewi kuuliza. Classified Info.
Naona umejihami mkuu!
 
Naona umejihami mkuu!
Sasa hivi situmii tena hizo dawa mkuu nilipata bad side effects hapa katikati zikaniletea allergy kwa hio nimeziacha kutumia labda labda hali ikiwa tight sana ndio nawahi pharmacy kununua, now nipo very okay
 
Back
Top Bottom