Niliposema tena kwa Kujiamini 100% kuwa Kocha Nabi atafukuzwa Yanga SC nilikuwa ninamaanisha

Niliposema tena kwa Kujiamini 100% kuwa Kocha Nabi atafukuzwa Yanga SC nilikuwa ninamaanisha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nilisema kuwa akikoswakoswa katika Derby ya Kariakoo (Simba na Yanga) basi atanasa katika Matokeo ya Mechi ya awali ya Club Africaine kama akifungwa au akitoka Sare na asiponaswa hapo anaenda Kuchinjiwa mazima kwa Matokeo ambayo anaenda kuyapata Jijini Tunis nchini Tunisia katika Mechi ya Marudiano.

Yaani niseme Jambo lisitokee? Kaeni tayari kwa Breaking News yoyote kumhusu Kocha Mkuu Nabi kuanzia Leo Alhamisi tarehe 3 Novemba hadi tarehe 9 au 10 Novemba kwani tokea Jana Moto Mkali umewaka huko Avic Town na Nabi Kamtukana Mtu huku Wachezaji Morisson na Aucho Wakitukanana.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The Great!!!
 
Haya yote kayataka Simba, Wanasimba ndio wakulaumiwa. Kila klabu ya Tanzania inayachukulia mashindano ya kimataifa rahisi sana sababu wanacheza na Simba daily na wanamfunga.

Kwa niaba ya Wanasimba nawaomba msamaha Uto na vilabu vingine kwa kuwaaminisha kama hii michuano simple ambapo sio kweli.
 
Nabi haondoki yanga na jana amepewa uhakika wa kuendelea na kibarua chake.
 
You are wasting your time nothing kwa kuisemasema yanga vibaya
 
Nilisema kuwa akikoswakoswa katika Derby ya Kariakoo ( Simba na Yanga ) basi atanasa katika Matokeo ya Mechi...
Sijaona chochote cha maana katika andishi lako. Ni speculations tu ambazo yeyote aweza kuwa nazo kutokana na pressure ya mashabiki na kiu ya kusonga mbele ktk mashindano ya kimataifa.

Nakuona kama mtu mwenye kiherehere tu ili jambo likitokea ujipatie credits za bure. Hakuna ambaye hajui au hahisi kuwa lolote laweza kutokea kwa Nabi kutokana na hali ilivyo ndani ya Yanga.

Hivyo usijifanye mjuaji saaaana wa mambo.
 
Tulia dogo yanga yupo sana atazidi kukupa mimba
 
Hilo lazima litokee maana utopolo wanalazimisha wafanane na SIMBA wakati utopolo ni mchicha simba ni mbuyu....
 
Sijaona chochote cha maana katika andishi lako. Ni speculations tu ambazo yeyote aweza kuwa nazo kutokana na pressure ya mashabiki na kiu ya kusonga mbele ktk mashindano ya kimataifa...
Sasa hapo hujaelewa nini? Yeye kasema kwa maoni yake ametabiri kufurushwa Nabi kutokana na Pressure ya mashabiki kuhusu mwendo wa timu hasa mechi za Kimataifa.

Mbona ulichoandika wewe na hizo hisia za mashabiki ni kitu kimoja ambacho ameandika mtoa mada..!
 
Nilisema kuwa akikoswakoswa katika Derby ya Kariakoo (Simba na Yanga) basi atanasa katika Matokeo ya Mechi ya awali ya Club Africaine kama...
Pick the exact date unachofanya ni ramli bwana kolo
 
Nilisema kuwa akikoswakoswa katika Derby ya Kariakoo (Simba na Yanga) basi atanasa katika Matokeo ya Mechi ya awali ...
Ngoma haipoi wala haitulii

Mwaka kongwa huu kwa watopolo😀
 
Back
Top Bottom