The Transporter
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 3,580
- 7,203
Nakumbuka mwaka 2015 Mwezi 9 baada ya kujichanga changa kidogo nikawa nimesave pesa kiasi nikasema hizi hizi Boxer BM 150 wakati huo ndio zimeanza kushika kasi nikaenda niaenda kuinunua pale mitaa ya Tazara.
Kwa mjini hapa matumizi yake nilikiwa naogopa kidogo maana wakati huo kulikuwa na ajari nyingi za pikipiki hivyo nimpelekee mtu mkoa ambae atafanya biashara itazalisha faida, japo kwa kipindi kile pikipiki za kichina zilikuwa zimetawala ila kwangu nialiangalia utulivu barabarani,
baada ya kuinunua nilienda kuuliza namna ya kuisafirisha pale ubungo kwenye mabasi gharama nilizoambiwa zilikuwa zinakaribia laki 2 nikasema hapana halafu kulikuwa na mambo ya kufungua steringi nilichofanya niliipeleka kwa fundi akaifanyia check up japo ilikuwa mpya nikatoa ile oil iliyokuja nayo nikaweka nyingine 20w50 Bp akapitia pitia na baadhi ya nati kukaza kaza , nikaomba likizo fupi job nikasema nitakomaa, safari ilianza saa 10 alfajiri hapo nipo full koti la kuzuia upepo na kikinga upepo kifuani buti ya kazi mikononi glavi.
Nilibeba na baadhi ya spana za kuajasti cheni na oil lita moja ya akiba mwendo wastani hakuna raha ya safari kama kutumia pikipiki kikubwa iwe imara maana hakuna tochi wala nini Dom nilitimba saa tano asubuhi nikapiga breakfast ya nguvu kidogo nikaongeza mafuta nikaajust cheni saa saba niakaanza safari ikaanza saa 9 nipo Manyoni nikabadiri oil faster maana na kufanya marekebisho yote madogo madogo maana nilikiwa naingia njia ya itigi ile ni karibu kilometa 300 ni pori tu mpk unaingia Tabora by saa kumi nikaianza safari ya lala salama kumaliza safari yangu ya kilometa zaidi ya 850.
Ila Mungu alisaidia saa mbili kasoro naingia Tabora aka Mboka nipo hoi, changamoto kubwa ilikuwa porini mule lile pori linatisha na hapo ndio boxer niliikubari kuna vijiji nilikuwa napita wanakijii wapo waliokuwa wanataka ligi na michina ya ila waliishia kuona vumbi tu maana nilikuwa nawahi giza nene lisinikute mule changamoto nyingine baada ya kufika safari yangu kwanza nililala kuja kuamka kesho saa saba mchana mwili wote hoi na sikutaka kabisa kushika pikipiki.
Mwaka huu panapo majaaliwa hili janga la covid19 likiisha nataka nijaribu hii ya Boxer ya Mo japo siziamini wengi wanazilalamikia na ile barabara ya vumbi sasa hivi ni lami nadhani nitawahi zaidi kufika.