Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
Mkuu ukiwa unaendesha pikipiki hasa masafa marefu kama hivyo cha kwanza lazima uwe na speed ambayo umejiwekea, Kingine sio high way tu ndio kunatisha na kwa magari kutomthamini wa pikipiki humu mijini ndio wamejaa sana hasa dsm sehemu yeyote ukiwa unaendesha pikipiki kipengele cha kwanza ni kutumia sheria ya udereva wa kujihami kwa maana haijarishi upo upande wako au sio vipi ila muda wote tahadhari usijaribu kushinda na wamagari kabisa nipo bora hata upark umpishe apite kabisa
 
Sasa hapo ungekua na baja 250 au xlr. Sikupatii picha

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ile barabara ya pori kutoka Manyoni kwa wakati ule haikuwa na lami huko ndio ilifikia kipindi nikaanza kujuta maana ni pori tupu halafu unajiuliza nikipata break down hapa itakuwaje maana speed sikulegeza na kuwa mwangalifu ila baada ya kufika maendeo ya tabora mjini nilijiona bonge shujaa na ile pikipiki kaibatiza jina la black horse
 

Wakati mwingine lala hata Singida, Usi tembee usiku maana sio sawa!
 
Boxer umetoka Dar saa 10 Alfajili ukaingia Dodoma Saa 5. Mkuu ebu tuache basi ndugu yangu. Ulikuwa unatembea mwendo wa kilometa ngapi kwa saa? Boxer kumbuka ni pikipiki fupi sana. Ungekuwa na unaendesha XL 250 na kuendelea zile honda ningekuelewa ama ENDURO YAMAHA. Kuna mtu katoa angalizo kuwa hakuna mtu wa kusoma kakosea angesema hakuna mtu wa kukuelewa.Scania ama hizi Youtong zinakoma na Dar Tabora. Ebu njoo ufafanue vyema . Mimi napinga kbs.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdingi alikua na paris dakar honda miaka hiyo,ye kwenda lusaka na kurudi kwake ilikua km kwenda dukani.siku kanipita mbalizi pale nasubiri daladala nilichoka hiyo spidi.

Alafu jamaa wampigia miluzi tu kapita fyaa.honi nyiingi. Namkuta home kakaauka sijamwambia km nimekuona pale maana angeuliza ulikua unafanya nini kule viboko vingeanza.mi nilikua mzururaji tu sina issue nikichanga pesa mawazo yangu nipande mwailubi ama mbembela nitembee tu nauli fala tu sh 5 miaka hiyo.

Ilimuua badae hiyo pikipiki.
RIP dingi 😔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…