Poleni Wanayanga, hakika huko SUDAN kuchomoa ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
Hii ni international games, hatuchezi mpira kama tunacheza na Singida Big Stars . Kuna nidhamu zake, tahadhari na hekima.
Hutetemi temi tu kama mgonjwa wa Akili. Ni full discipline, tactical na Experience.
Inawapasa kuendelea kuiheshimu Simba Sc Daima Kwenye hizi anga za kimataifa.
Kwa michezo ya kimataifa, ni lazima ushinde nyumbani ili ufike makundi na robo fainali, na ndio mnaonaga SSC nayo ikifika kwenye knock out , nayo inatoka..... huko mbele mlima unakuwa ni mkubwa zaidi.
Nilishawahi kusema Yanga hamjawahi kuwa tested na maneno yangu yanaenda kuwa ya kweli, mara hii mnaenda kuwa tested for the first time since 1998.
Tusipeane moyo, kuitoa Al Hilal pale Khartoum sio rahisi hivo. Mtapumua pumzi ya moto kama Injinia Hersi alipotoa pumzi nzito pale Kwa Mkapa. Maisha sio simple simple kihivyo. Great things are never easy , they also need time.
Mara ya mwisho nyie kucheza nje ya nchi ugenini ni lini ? Mechi za stage one mlichezea hapo Hapo Tanzania, mkachukulia maisha poa. Mlitakiwa kustuka na hizo goli 9. za mchongo.
Kazi mnayo kweli kweli , Halafu kumbukeni mwaka ni mrefu sana, mkitolewa sasa hivi ni hadi mwakani , parefu sana .
Nipo hapa Angola nasubiria game za wabishi.