Nilishindwa kulala usiku baada ya kusoma 'Sheria mpya ya Usalama wa Taifa'. Nimeumia sana kama mwananchi wa kawaida

Sio hii. Deep state nawafahamu. Ni kikundi cha watu hata hawazidi 5 wakifika 10 wengine ni bosheni tu sio kundi kubwa kiasi hiki
Kiongozi hao wa5 wanaounda deep state ya nchi hii unawafahamu utuwekee majina yao hapa
 
Kwa nchi za wenzetu.. Vitengo vya usalama kidogo wana utu.. Kisha hata wakifanya kazi za hatari ikiwepo kueliminate mtu kunakuwa na mashiko..

Shida ni kwetu siasa ni nyingi...

Atakuja kuondolewa mtu wa kisiasa na sababu zisizo na kichwa wala miguu...

Raia wajiandae.. Yaani unapotezwa kiintelegensia.. Majibu yanatoka kwa usalama wa nchi... Afisa aliyehusika analindwa kisheria..

Wengi wa maafisa hawa wapo kichama na kishabiki na sio weledi wa kazi... Wataumiza watu wengi... Tusubiri
 
Tunapaswa kufanya maamuzi kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia ktk kila nyanja..

Ni tatizo kubwa sana kuwa na wananchi walio juu ya sheria ikiwemo wenye mamlaka yeyote..

Kila mmoja wetu anapaswa kuwa chini ya sheria ikiwemo viongozi wakuu..

Muhimili wa mahakama pamoja na mapungufu una umahili na mfumo thabiti ktk utoaji haki kijinai hata madai..

Mfumo wa uendeshaji Mashitaka,Mfumo wa na sheria ya ushahidi vipo wazi katika kufanya upembuzi wa hatia ama kutokua na hatia kwa mshitakiwa yeyote awe mkubwa ama mdogo..

Kubwa zaidi ni mhimili wa mahakama kuwa huru zaidi hasa ktk uteuzi wa Jaji mkuu,Wasajiri,majaji,Mfuko huru wa fedha ktk kufanikisha mipango na mikakati yake pasipo kuingiliwa na Serikali..Hili litawaweka huru wasimamia haki kutoshurutishwa na wenye mamlaka juu ya hatima zao pindi wakifanya maamuzi kwa kuzingatia haki na si misukumo ya kisiasa,ubinafsi wa wenye mamlaka.

Kuweka kinga ni ruhusa ya uovu,uasi,uharibifu na machukizo makuu ktk amani,utulivu,usalama na ustahimilivu ktk taifa..

No one should be above the Law..No matter what is needed to be done,Should be done in accordance to the country Constitution and Laws..

Ktk hili ninaamini hata watumishi watiifu wa idara ni watiifu kwa Katiba yetu na sheria zetu hivyo hawawezi support mabadiriko yanayolawiti haki,utu,ubinadamu,Usawa na undugu..

Mwisho,Maafisa ni wajukuu zetu,Watoto zetu na ni binadamu kama wengine..wana mapungufu,mihemuko,udhaifu na changamoto (Ktk Elimu,Mapenzi,Siasa,jamii,Biashara,Sayansi,etc)…In a sense kwamba wapo kila sehemu ktk maisha yetu ya kila siku..Wapo Jeshini,Polisi,uhamiaji,Vyuoni,Mashuleni,Wafanyabiashara,Madaktari,Injinia’s,Bodaboda,wauza mchicha,machangudoa,wauza bar,wasafisha viatu,Makuri,Mafundi garage,Waiters…Wachungaji,Maaskofu..Masheikh..Ma house girls,N.k

Hatupaswi kuwapa mamlaka na nguvu isiozibitika kwa mifumo ya wazi kisheria..Hata wanajeshi Ambao ni wapiganaji kwa niaba ya wananchi wote wana mfumo wa utoaji haki kijashi (Mahakama za kijeshi)..Hii yote ni kudhibiti matumizi mabaya ya vyeo,mamlaka,madaraka na mafunzo au ujuzi..

Tanzania tunayoijenga tuijenge iwe ya neema na si majanga,hofu na wasiwasi considering bad perspective na experience juu ya wasiojulikana…

Nawapongeza maafisa wetu wa usalama wa taifa kwa kazi ngumu na kujitoa kwa viapo vigumu ili kuhakikisha nchi inakuwa salama kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama..Checks and balance is innevitable📌
 
Ni makada wa CCM wote
 
Ni vizuri wenye washkaji huko watambe 🤣 ukizingua nakutia nyavuni mkulungwa anamaliza show.

Glock45 click cluck muthafuqa😀
 
Mlisema jiwe ni DIKTETA sio!

Kula chuma hicho.
Watu walikuwa busy kueleza mabaya ya dikteta Jiwe kwa madai ya kwamba viongozi waliyopo sasa wajifunze wasirudie tena makosa kama ya Jiwe, ila kinachoendelea ni wazi viongozi waliyopo hakuna walicho jifunza.
 
Hapa kuna shida kubwa ya kiungozi katika taifa letu. hii mbegu inayopandwa sasa kuna siku huko mbeleni tutaivuna wote pamoja kwa madhara sawa, na hao wanaodhani watakuwa salama baada ya kutungwa kwa sheria hizi. ikumbukwe hata Rwanda na Burundi hapo mwanzo mambo yalikuwa hivi hivi yaani kundi moja la watu kuona lina haki zaidi katika Taifa kuliko wengine na kujitungia sheria kedekede za kujilinda na hata ikibidi kuzima uhai wa wengine ili kubaki madarakani, lakini mwisho siku maangamizi yakatokea ambapo kila upande ulipoteza watu wengi kutokana na kuchukulia mambo for granted kama yanayoendelea hapa kwetu sasa hivi. Kuna watu wanadhani hii nchi ni ya kwao na kwamba pasipo wao kuwa madarakani bora nchi iwake moto. Kuna siku hizi sheria zitashindwa kuwalinda hata hao waliyozitunga na kuzibariki zitumike.
 
Sheria haifai kama ni kweli
Yaani mtu anaweza kukuua tu kwa wivu wa mapenzi kwa mfano,halafu aka fabricate ulikuwa unahatarisha usalama wa taifa na hawezi kushitakiwa kwa mauaji?
Ni hatari sana hii
Tatizo lipo hapo, ni vipi tutajua hakua kwenye majukumu yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…