SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kutokana na sintofahamu na tetesi zinazoendelea kuhusiana na Denis Kibu (mpaka leo sielewi kwa nini watu wanamuita Kibu Denis badala ya Denis Kibu lakini hilo tuliache kwa leo), nimekumbuka kauli yangu niliyowahi kuitoa kuhusu future yake. Niliwahi kusema kuweni na akiba ya maneno, kuna siku mtamkuta Kibu anacheza Ulaya.
Ni kweli Kibu siyo mchezaji mwenye ile unaita kipaji asili cha kina Chama au Aziz Ki ila kitu kimoja ambacho atakupa kila siku atakayoingia uwanjani ni juhudi za asilimia 100. Katika mpira wa sasa ambao mbinu za mchezo na nguvu zina nafasi kubwa kuliko umahiri binafsi wa mchezaji, Kibu ana nafasi kubwa ya kucheza. Kibu anacheza vizuri tu EPL hata kama siyo katika timu kubwa.
Nimalizie kwa kusema, kama kachukua pesa ya Simba akatoweka atakuwa kazingua sana na hapo inaonyesha jinsi management za wachezaji wa Kitanzania zinavyokosa weledi. Kiufupi alikosa washauri wazuri.
Huu uzi umebadili direction sana naona hadi watu wamechanganyikiwa 🤣😂🤣 Siku mkisikia Kibu ameuzwa Belgium uzi utafufuka tena.