Nilitaka kumpiga makofi Afisa wa uhamiaji


Halafu usikute wakati anaongea na wewe alikuwa anatafuna karanga hovyo hovyo bila utaratibu.

Hapo alikuwa anatengeneza mazingira ya rushwa.

Kama tumeamua kufanya vitu mitandaoni sioni sababu ya kufanya nusu mtandaoni halafu tumalizie ana kwa ana. Ni kwanini uhamiaji wasiweke utaratibu wa kumaliza mambo yote mtandaoni?

Njia pekee ya kumaliza rushwa kwenye ofisi za umma ni kuweka utaratibu huduma zote zifanyike kwa njia ya mtandao.
 
Ona huyu naye, hopeless folk.
Uhamiaji njaa tupu, tumewahonga sana wanapokea tu hawana aibu wala haya.

Ukimpa laki anakenua mpaka koromeo linaonekana. Atajichekesha chekesha huku anakuita majina yote, boss, muheshimiwa, mtukufu!

Hata kama huna vigezo ukitoa hela unapewa vibali vyote kiulaini sana.

Kibali cha kazi na cha ukaazi vyote unapewaaaa bwerereee bila vigezo, mradi umetoa tu pesa.
 
Umeongea neno 👍🏾
 
Uko sawa kabisa mkuu. Technology inaweza kupunguza rushwa kwa kiwango kikubwa sana maana inapunguza kuonana ana kwa ana na watendaji.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
nilidhani ni waha tu kumbe mpaka masai wanabaguliwa?
 
usipende kurusha rusha ngumi,ni dalili ya usela mavi na kukosa kujisimamia katika maisha.

hapo kilichokupeleka ni kitu kingine cha msingi sana katika maisha,unaamua kumsugua ndosi afisa,unakamatwa,unawekwa mahabusu,kesi mahakamani,hutoboi unalipa fine au kifungo.
umeshavuruga mipango yako.

NB,wewe ni msimamizi wa mipango yako,ukikubali mtu aivuruge,umekubali akutawale.
 
Raha yao kujaza watu upepo tu na usipokuwa makini utajaa kweli.

Swali langu ni kuwa hata wale ngozi nyeupe (Indian&Arabs) wanafanyiwa hivi kweli? Au sisi wamatumbi tu.
Tena hao utawaonea huruma kama hawana hela,mie mzee wangu alisumbuliwa sana na hapo alikuwa ana renew na kuwaombea wadogo zangu alisumbuliwa sana akaambiwa atoe milioni 10 akagoma, wakati kazaliwa tanzania na wazazi wake hawajazaliwa Tanzania lakini walikuwa na uraia wa Tanzania na nyaraka zote aliwapa, mwisho wa siku wadogo zangu wakaamua kwenda kuomba za kenya wakapata fasta bila usumbufu.
 
Duh kumbe! Basi ni tatizo kubwa!
 
Duh kumbe! Basi ni tatizo kubwa!
hapo ilikuwa kipindi cha magu, ila awamu ya sasa watu wengi nawafahamu wameomba na wamepata tena haraka wiki mbili tuu bila kutoa chochote, tena kuna mmoja dom alienda akaambiwa bado hichi akaenda kuleta, akaambiwa tena bado hichi yule afisa akamwambia hiyo document unitumie tuu kwenye wasap nijiridhishe twende ukapige picha na kuweka finger print na after 3 weeks akapata passport yake bila kujuana na mtu au kutoa chochote. sasa hivi kama huna connection na umekamilisha documents zote (alafu vizia ile foleni ya mchana ufike wakiwa wanakaribia kutoka)passport ni wiki mbili ila unapata,ukiwa na connection passport ni siku tatu tuu umepata 😀.
 
Mkuu ulikua unatengenezewa mazingira ya rushwa sema na wwe umekamilika kila kitu ndiyo maana afisa akakasirika!!
 
Uko sawa kabisa mkuu. Technology inaweza kupunguza rushwa kwa kiwango kikubwa sana maana inapunguza kuonana ana kwa ana na watendaji.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Na Watumishi wengi hawapendi.hiyo Technology maana inawanyima kula, lazima.watai sabotage tu kama wale wa Mwendokasi na zile kadi zilivyo yeyuka, na sasa wana furahi wamerudi kwe vi risit vyao vya karatasi hadi sasa wanaamua kuzulumu zile change 50 50 za.wateja, wakati kipindi cha kadi kulikua hakuna hata mambo ya usumbufu wa change!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…