Nilitaka kusafirisha mzigo kwa njia ya reli nikakuta gharama ni kubwa kuliko malori

Nilitaka kusafirisha mzigo kwa njia ya reli nikakuta gharama ni kubwa kuliko malori

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Labda sielewi au nasikiliza vibaya pindi wataalam na viongozi wetu wanapo zungumzia usafiri wa reli kua eti ni usafiri wa gharama nafuu ukilinganisha na barabara.

Majuzi nilikua na tani 30 za mahindi ili nisafirishe kutoka Mbeya kuja Dar es Salam nilipoenda kuuliza bei nikaambiwa kilo moja itasafirishwa kwa shs 220 uongeze na gharama za Porter's.

Nilipoamua kutafuta malory nilipata malory tofauti tofauti ambapo nikilinganisha bei zao nilipata wastani wa sh 80 kwa kilo.

Kutokana na ukweli huo nikajiuliza huo unafuu unaotajwa kusafirisha mizigo kwa njia ya reli ni kwa muktadha gani?
 
Na uzuri zaidi au ubaya ni kwamba Lori linafwata mzigo sehemu nzuri ulipo na kama unakofikisha dar panaeleweka pia unashusha mlangoni kabisa kwahiyo unakazi yq kupakia mara moja na kushusha mara moja.

Ila kwa treni utapaswa upakie ghala lako upeleke mpaka stesheni na pia ushushe stesheni kupeleka ghala la Dar. Kwa mantiki hiyo gharama za usafiri kwa reli ilipaswa iwe chini sana (labda kama sh 30) kwa kilo ili iweze kushindana na usafir wa gari.

Ila hawajui haya wamekaa tu pale wanakula mishahara hawana ubunifu wowote.
 
Hapana haiwezi ikawa kweli, labda kama ulusikia vibaya!!mfano kutoka MPANDA(KATAVI) hadi dar mzigo wa tani 40, kwa tren kilo moja ni tsh.55, wakati kwa lori ni kati ys 110-120?!!kawaida usafiri wa treni lazima uwe pungufu kati ya 30-40% kulinganisha na wa gari.
 
Pengine ndiyo maana watu hawatumii huu usafiri. Ni ushenzi. Zamani watu walikuwa wanasafirisha mafuta kwa treni, treni moja inakokota matank ya kutosha. Wakaanza ubabaishaji, mara wanaiba mafuta nk.

Treni zetu hizi wangewapa wataalamu binafsi waziendeshe kibiashara na si kizembe hivi. Ila wawe makini wasije kuwapa kama wale wahindi wapigaji na wahuni.
 
Kuna wengine wa posta, siku hizi wana huduma za kusafirisha mizigo kwenda mikoani lakini namna ya ku advertise ndio hawajui, mpaka ukiwaambia watu mtaani wasafirishe kwa njia ya posta wasitumie mabasi wanabaki wanakushangaa maana hawajui kama posta pia wanasafirisha mizigo kama mabasi
 
Kama TTCL. Hii nchi mashirika ya umma ni tatizo sana. Yaani swala la kujiongeza ili kuvutia wateja ni kama hakuna kabisa.
 
Kama TTCL. Hii nchi mashirika ya umma ni tatizo sana. Yaani swala la kujiongeza ili kuvutia wateja ni kama hakuna kabisa.
Ni shida tupu haya mashirika

Kuna sehemu huwa nachukua mzigo nautuma kwa posta

Sasa afisa masoko akaniambia nimsaidie kutangazia wengine wawe wanatumia mizigo posta

Nilipoenda kuwaambia watu wakawa wananishangaa, maana wao wanajua posta ni kutuma bahasha na barua tu

Nilirudi nikamwambia waende wao wakatoe elimu kwa hao wafanyabiashara maana lile eneo watu wengi wanatuma mizigo mikoani kwa njia ya mabasi

Sasa nilicholiza Mimi, wanashindwa nini kufatilia sehemu kama hizo zenye biashara zinazotumwa mikoani wakawapa elimu hao wanaotuma ili watumie huduma ya posta

Mpaka wanasubiri Sisi wengine tusiohusika tuwaambie vya kufanya utasema sisi tunafaidika na lolote
 
Ni shida tupu haya mashirika

Kuna sehemu huwa nachukua mzigo nautuma kwa posta....
Shida ni kwamba hausianishi mshahara wake na huduma anayotoa. Yaani hajui kuwa mizigo ikisafirishwa mingi kupitia kampuni yake ndo anakuwa na uhakika zaidi wa mshahara.

Kusema ukweli hata mi leo ndo nimejua kuwa posta wanasafirisha mizigo
 
Naomba kijuzwa,kutuma mzigo kwa njia ya reli kuna bima inafidia hasara pale mzigo unapopotea au kuharibika pale reli au gari moshi linapopata hitilafu na mzigo kushindwa kufika kwa wakati na kuharibila?
 
Kwanza wanaongoza kwa wizi. Hukawii kukuta gunia zimepungua.

Mimi waliniibia kompresa ya kwenye friji wakati wa kuhama sina hamu nao mpaka leo.
Naomba kijuzwa,kutuma mzigo kwa njia ya reli kuna bima inafidia hasara pale mzigo unapopotea au kuharibika pale reli au gari moshi linapopata hitilafu na mzigo kushindwa kufika kwa wakati na kuharibila?
 
Shida ni kwamba hausianishi mshahara wake na huduma anayotoa. Yaani hajui kuwa mizigo ikisafirishwa mingi kupitia kampuni yake ndo anakuwa na uhakika zaidi wa mshahara.

Kusema ukweli hata mi leo ndo nimejua kuwa posta wanasafirisha mizigo

Hata mimi ndio nimejua leo posta wanasafirisha mizigo. Ahsante ndugu melibam kwa taarifa.
 
Wanatuma mkuu, tena mimi naona ni njia salama kutumia kwao maana mzigo unatunzwa sehemu nzuri kabla haujasafirishwa na ukishafika unawekwa sehemu nzuri

Tofauti na mabasi mengi yenye vi ofisi vidogo unakuta mizigo inabananishwa au wakati mwingine ukienda kupokea au kutuma mzigo unafikishiwa nje kwenye jua

Na pia gharama zao ni nafuu sana, mfano ukiwa na ki parcel kidogo chini ya kilo kumi wanachaji kama shilingi elfu 5 compare na mabasi ambayo wao parcel yoyote ni elfu 10 kwenda juu

Pia mzigo unafika kwa wakati, mfano ukiupeleka mzigo wako wanaanza safari saa 10 jioni ndio utaratibu wao wa kila siku so kama ni karibu unakopeleka unaweza kuupokea kesho mapema tu, kama ni mbali unaupokea keshokutwa yake asubui ambayo ni sawa na mabasi tu

Tatizo lao ni hawajui namna ya kujitangaza ty,
 
Hata mimi ndio nimejua leo posta wanasafirisha mizigo. Ahsante ndugu melibam kwa taarifa.
Wanasafirisha mkuu, sema tatizo ni hawajui namna ya kujitangaza tu, na nk affordable compare na mabasi na ni safe sana pia

Ukipata nafasi watembelee matawi yao watakupa utaratibu
 
Miaka kama kumi iliyopita nilisafirisha kitanda, godoro na jiko kutoka Moro hadi Mbeya kwa posta na vikafika vizuri ila ni mpaka mtu akuambie. Sijui kwanini hawajitangazi?
Wana shida ya kujitangaza, ila ni usafiri mzuri sana kutumia posta, mimi ninaupenda sana kwa kweli, tatizo ni watu wa masoko waliowekwa pale ndio hawajui kazi yao
 
Hapana haiwezi ikawa kweli, labda kama ulusikia vibaya!!mfano kutoka MPANDA(KATAVI) hadi dar mzigo wa tani 40, kwa tren kilo moja ni tsh.55, wakati kwa lori ni kati ys 110-120?!!kawaida usafiri wa treni lazima uwe pungufu kati ya 30-40% kulinganisha na wa gari.
Bei ulizosema NI mamlaka tofauti, kutoka mbeya unatumia train ya tazara inamilikiwa na Tanzania na Zambia. Kutoka kigoma unatumia reli ya Kati -TRC. Sasa usilinganishe Bei ya hizo njia.
 
Bei ulizosema NI mamlaka tofauti, kutoka mbeya unatumia train ya tazara inamilikiwa na Tanzania na Zambia. Kutoka kigoma unatumia reli ya Kati -TRC. Sasa usilinganishe Bei ya hizo njia.
Hata kama ni njia mbili tofauti haiwezi ikawa kwa kiasi hicho anachokisema!!na cjawahi kuona popote duniani usafiri wa treni ukawa juu kuliko wa gari, hasa kwa mizigo hii ya kawaida labda kama ni mzigo unaohitaji uangalizi maalum.
 
Back
Top Bottom