Nilitaka kusafirisha mzigo kwa njia ya reli nikakuta gharama ni kubwa kuliko malori

Nilitaka kusafirisha mzigo kwa njia ya reli nikakuta gharama ni kubwa kuliko malori

Shida ni kwamba hausianishi mshahara wake na huduma anayotoa. Yaani hajui kuwa mizigo ikisafirishwa mingi kupitia kampuni yake ndo anakuwa na uhakika zaidi wa mshahara.

Kusema ukweli hata mi leo ndo nimejua kuwa posta wanasafirisha mizigo
Ndio tatizo la kumuajiri mtu ajira ya kudumu,akifanya kzi ambayo hata ya kuingizia shirika fedha nyingi bado yeye mshahara wake unabaki palepale
 
Nimejifunza kuwa,

Posta ni njia nzuri ya kusafirisha mizigo kwa bei nafuu ( mizigo mikubwa hata meza, vitanda nk).

Kuhusu gharama za Treni kwenye kusafirisha mizigo nitafuatilia kwani inaonekana kuna maelezo hayapo sawa
 
Na uzuri zaidi au ubaya ni kwamba Lori linafwata mzigo sehemu nzuri ulipo na kama unakofikisha dar panaeleweka pia unashusha mlangoni kabisa kwahiyo unakazi yq kupakia mara moja na kushusha mara moja...
nmepata shule🤔🤔🤔
 
Hapana haiwezi ikawa kweli, labda kama ulusikia vibaya!!mfano kutoka MPANDA(KATAVI) hadi dar mzigo wa tani 40, kwa tren kilo moja ni tsh.55, wakati kwa lori ni kati ys 110-120?!!kawaida usafiri wa treni lazima uwe pungufu kati ya 30-40% kulinganisha na wa gari.
bado usafiri wa gali utakuofa mahali fulan tofauti na tren
 
Taasisi nyingi za Tz hazijui kazi zinazotakiwa fanya, na hii ni sababu wana uhakika wa mishahara na kazi hawafukuzwi...

Sheria ibadilishwe wafanyakazi wa UMMA wawe wanafukuzwa kutokana na kutokidhi mahitaji ya wakati husika
 
bado usafiri wa gali utakuofa mahali fulan tofauti na tren
Sasa mkuu mimi kwa treni nasafirisha tani 40, kwa milioni 2.2, kutoka katavi hadi dar, kwa mzigo huo kama ni gari nitatumia milioni 4.4 , hiyo tofauti ya karibia 2.2 hata kama nitatakiwa kufikisha sokoni toka station hadi tandika, hata laki tano haitakwisha!!
 
Sasa mkuu mimi kwa treni nasafirisha tani 40, kwa milioni 2.2, kutoka katavi hadi dar, kwa mzigo huo kama ni gari nitatumia milioni 4.4 , hiyo tofauti ya karibia 2.2 hata kama nitatakiwa kufikisha sokoni toka station hadi tandika, hata laki tano haitakwisha!!
Wewe ndio umeeleza uhalisia, inawezekana huyo jamaa kakutana na vishoka. Usafiri wa treni ni rahisi Sana kuliko magari, nimesafirisha sana mahindi.
Gari unalipia kwenda na kurudi, wakati treni unalipia kwenda tu. Gharama ya treni ni nusu ya gharama ya gari.
 
nmepata shule🤔🤔🤔
Shukrani mkuu

Ndivyo ilivyo unaposafirisha kwa "bulk" lazima gharama ziwe chini ili kufidia gharama za kufaulisha na kusambaza tena kwenye chain mpaka mwisho.

Hivyo hivyo kwa meli inayosafirisha mzigo mkubwa kwa pamoja gharama ni chini kuliko kusafirisha kwa semi itakayokwenda kufaulisha kwenye meli kupeleka ambapo meli haifiki

Sasa hii ya gharama kuwa juu kuliko chombo kidogo ni maajabu ya Tanzania tu
 
Kuna wengine wa posta, siku hizi wana huduma za kusafirisha mizigo kwenda mikoani lakini namna ya ku advertise ndio hawajui, mpaka ukiwaambia watu mtaani wasafirishe kwa njia ya posta wasitumie mabasi wanabaki wanakushangaa maana hawajui kama posta pia wanasafirisha mizigo kama mabasi
Kama TTCL. Hii nchi mashirika ya umma ni tatizo sana. Yaani swala la kujiongeza ili kuvutia wateja ni kama hakuna kabisa.
Hizi taasisi za serikali, wafanyakazi wana uhakika wa mshahara so hawawezi kutia nguvu ili iweje?.

Mfano, watu kama tigo, voda m, zantel nka au DHL nk hawa wanategemea matangazo na watu ndiyo waweze kuishi, no ruzuku.
 
Labda sielewi au nasikiliza vibaya pindi wataalam na viongozi wetu wanapo zungumzia usafiri wa reli kua eti ni usafiri wa gharama nafuu ukilinganisha na barabara.

Majuzi nilikua na tani 30 za mahindi ili nisafirishe kutoka Mbeya kuja Dar es Salam nilipoenda kuuliza bei nikaambiwa kilo moja itasafirishwa kwa shs 220 uongeze na gharama za Porter's.

Nilipoamua kutafuta malory nilipata malory tofauti tofauti ambapo nikilinganisha bei zao nilipata wastani wa sh 80 kwa kilo.

Kutokana na ukweli huo nikajiuliza huo unafuu unaotajwa kusafirisha mizigo kwa njia ya reli ni kwa muktadha gani?
Hapo bado hujaibiwa angalau magunia mawili hapo Kisaki
 
Na Mzigo wako ukiibiwa au ukilowa Reli huwa hawalipi fidia kwaivo inakua kwako
 
Back
Top Bottom