Ndio tatizo la kumuajiri mtu ajira ya kudumu,akifanya kzi ambayo hata ya kuingizia shirika fedha nyingi bado yeye mshahara wake unabaki palepaleShida ni kwamba hausianishi mshahara wake na huduma anayotoa. Yaani hajui kuwa mizigo ikisafirishwa mingi kupitia kampuni yake ndo anakuwa na uhakika zaidi wa mshahara.
Kusema ukweli hata mi leo ndo nimejua kuwa posta wanasafirisha mizigo
nmepata shule🤔🤔🤔Na uzuri zaidi au ubaya ni kwamba Lori linafwata mzigo sehemu nzuri ulipo na kama unakofikisha dar panaeleweka pia unashusha mlangoni kabisa kwahiyo unakazi yq kupakia mara moja na kushusha mara moja...
bado usafiri wa gali utakuofa mahali fulan tofauti na trenHapana haiwezi ikawa kweli, labda kama ulusikia vibaya!!mfano kutoka MPANDA(KATAVI) hadi dar mzigo wa tani 40, kwa tren kilo moja ni tsh.55, wakati kwa lori ni kati ys 110-120?!!kawaida usafiri wa treni lazima uwe pungufu kati ya 30-40% kulinganisha na wa gari.
Sasa mkuu mimi kwa treni nasafirisha tani 40, kwa milioni 2.2, kutoka katavi hadi dar, kwa mzigo huo kama ni gari nitatumia milioni 4.4 , hiyo tofauti ya karibia 2.2 hata kama nitatakiwa kufikisha sokoni toka station hadi tandika, hata laki tano haitakwisha!!bado usafiri wa gali utakuofa mahali fulan tofauti na tren
Wewe ndio umeeleza uhalisia, inawezekana huyo jamaa kakutana na vishoka. Usafiri wa treni ni rahisi Sana kuliko magari, nimesafirisha sana mahindi.Sasa mkuu mimi kwa treni nasafirisha tani 40, kwa milioni 2.2, kutoka katavi hadi dar, kwa mzigo huo kama ni gari nitatumia milioni 4.4 , hiyo tofauti ya karibia 2.2 hata kama nitatakiwa kufikisha sokoni toka station hadi tandika, hata laki tano haitakwisha!!
Shukrani mkuunmepata shule🤔🤔🤔
Kuna wengine wa posta, siku hizi wana huduma za kusafirisha mizigo kwenda mikoani lakini namna ya ku advertise ndio hawajui, mpaka ukiwaambia watu mtaani wasafirishe kwa njia ya posta wasitumie mabasi wanabaki wanakushangaa maana hawajui kama posta pia wanasafirisha mizigo kama mabasi
Hizi taasisi za serikali, wafanyakazi wana uhakika wa mshahara so hawawezi kutia nguvu ili iweje?.Kama TTCL. Hii nchi mashirika ya umma ni tatizo sana. Yaani swala la kujiongeza ili kuvutia wateja ni kama hakuna kabisa.
Hapo bado hujaibiwa angalau magunia mawili hapo KisakiLabda sielewi au nasikiliza vibaya pindi wataalam na viongozi wetu wanapo zungumzia usafiri wa reli kua eti ni usafiri wa gharama nafuu ukilinganisha na barabara.
Majuzi nilikua na tani 30 za mahindi ili nisafirishe kutoka Mbeya kuja Dar es Salam nilipoenda kuuliza bei nikaambiwa kilo moja itasafirishwa kwa shs 220 uongeze na gharama za Porter's.
Nilipoamua kutafuta malory nilipata malory tofauti tofauti ambapo nikilinganisha bei zao nilipata wastani wa sh 80 kwa kilo.
Kutokana na ukweli huo nikajiuliza huo unafuu unaotajwa kusafirisha mizigo kwa njia ya reli ni kwa muktadha gani?