Nilitegemea kipindi kama hiki viongozi washauri baadhi ya Watanzania kutumia gesi asilia badala ya petrol kwenye magari

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Ili kupunguza gharama za maisha nilitegemea kipindi kama hichi viongozi washauri baadhi ya watanzania kutumia gesi asilia badala ya petrol kwenye magari.

Gesi asilia (CNG) ni nishati ambayo hutumiwa kama mbadala wa petroli kwenye magari. Vilevile hutumiwa kama mbadala wa dizeli pia.

Mfano kwenye hizi gari za mwendokasi, huu ndio ulikuwa wakati wa hizo gari kutumia gesi asilia ili nauli zisipande na kuwaongezea adhaa wanainchi wa Dar es Salaam.

Tumeona jinsi Dangote alivyobadilisha magari yake makubwa yanatumia gesi asilia.

Kama tumekua tumejipanga tangu zamani leo tusingelia na huu mfumko wa bei.

Habari, ukitumia mfumo wa gesi kwenye magari unapunguza gharama kwa 60%, yaan ni 150-200km kwa 15500/- na gari inakuwa na nguvu ile ile Ukitumia gesi asilia kwenye magari unapunguza gharama kwa 60%, ambayo ni kilometa150 hadi 200 kwa Sh. 15500.

FB_IMG_16187517303317800.jpg
 
wataalamu wetu bado wamelala usingizi fofofo.
huwa najiuliza hivi kweli tunao wataalamu/watafaiti na wabunifu wenye elimu zao?
 
Mama anacho jua ni kufanya teuzi,kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu na kusema vitu vitapanda badala ya kutatua kero
 
Tatizo kubwa ni gharama ya kuufunga mfumo. Iwapo serikali ingekuwa na viongozi wanajiongeza leo hii gari zote Dar kama sio za nchi nzima zingekuwa zimefungwa huo mfumo. Hili la magari kutumia gesi lipo wazi sana na klimezungumzwa miaka na miaka lakini nafikiri kikwazo kikubwa na wadau wa mafuta maana siku akitokea kiongozi mweledi akalifanyia kazi vizuri basi vituo vingi vya mafuta vitakuwa magofu.

Suala ni rahisi sana serikali ingeilipa DIT ili iwafungie wenye magari huo mfumo bure halafu yenyewe iongeze shilingi 100 tu kwenye kila kipimo cha gesi sawa na lita moja ya mafuta mpaka gharama zao zirudi kwa kila gari.

Na hili limewahi kufanyika kwenye maji miaka ya nyuma walikuwa wanakuunganisha maji bure halafu wakati unalipa bili ya mwezi wanaweka ongezeko kidogo kulipia gharama za uunganishaji mpaka ziishe unaendelea kulipa bili kawaida. Lakini pia vituo vya kujazia gesi vinatakiwa viongezwe kwani kwa sasa vipo vichache sana.
 
Tatizo kubwa ni gharama ya kuufunga mfumo. Iwapo serikali ingekuwa na viongozi wanajiongeza leo hii gari zote Dar kama sio za nchi nzima zingekuwa zimefungwa huo mfumo. Hili la magari kutumia gesi lipo wazi sana na klimezungumzwa miaka na miaka lakini nafikiri kikwazo kikubwa na wadau wa mafuta maana siku akitokea kiongozi mweledi akalifanyia kazi vizuri basi vituo vingi vya mafuta vitakuwa magofu.

Suala ni rahisi sana serikali ingeilipa DIT ili iwafungie wenye magari huo mfumo bure halafu yenyewe iongeze shilingi 100 tu kwenye kila kipimo cha gesi sawa na lita moja ya mafuta mpaka gharama zao zirudi kwa kila gari. Na hili limewahi kufanyika kwenye maji miaka ya nyuma walikuwa wanakuunganisha maji bure halafu wakati unalipa bili ya mwezi wanaweka ongezeko kidogo kulipia gharama za uunganishaji mpaka ziishe unaendelea kulipa bili kawaida. Lakini pia vituo vya kujazia gesi vinatakiwa viongezwe kwani kwa sasa vipo vichache sana.
Mbona wengine wanatumia
 
Mbona Dangote anatumia
 
Back
Top Bottom