fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 6,699
- 9,323
SEHEMU YA KWANZA:NAREJEA TZ KUTOKEA MASOMONI.
Paa,natua Dar kutoka nje ya nchi nilipokuwa nasoma shahada ya kwanza.Nilifikia nyumbani kwa kaka yangu ambae alikuwa mtu mzima sana yaani umri ulikuwa mkubwa sana tu.
Yeye na mkewe walinipokea kwa furaha kubwa sana.Akaniuliza kuhusu mipango yangu,nikamjibu kuwa nitakuwepo nchini kwa miezi 9 tu,baada ya hapo ntarejea kusoma shahada ya pili.Akanijibu sawa.Nikawa namsaidia kazi zake kila siku,maana mimi ni hodari sana kwa kazi.
Kaka yangu alinipenda sana,kwani saa 11 asubuhi nishaamka,naoga nakunywa chai,navaa na naondoka na dereva kwenda ofisi kuu ya kaka maeneo ya ilala sharif shamba,ambapo namuandalia kazi kaka ambae hufika kila siku saa 4 sharp.Akifika nampa repoti ya kazi na ndipo naenda kukagua vituo vya mafuta 7 sehemu mbalimbali jijini dar.Nikitoka kukagua vituo vya mafuta,naenda kwenye duka lake la hardwares mtaa wa jamhuri na narejea ofisini saa 10,ambapo huwa tunakunywa kahawa pamoja na wafanyakazi wake,wa kike na kiume.
Nampa taarifa ya kazi,ambayo huwa nishaiandaa kiufundi sana,na alikuwa anafurahi mno na bahati naye ni msomi wa shahada ya kwanza ya uinjinia wa majengo.
Kila siku huwa tunatoka usiku saa 1 kurejea nyumbani maeneo ya mikocheni.
Namuacha hapo home,mimi naenda kutembea sehemu sehemu na saa 6 narudi home but sio kila siku huwa nafanya hivyo.
Siku moja kaka akaniambia,dada yangu mmoja ambae kaolewa Mwanza anataka niende kumtembelea maana mie nilikuwa namwita mama maana amenilea sana.
Basi nikajiandaa kwa safari,kaka aliniuliza lini ntaondoka kwenda na nitasafiri kwa njia ipi,nikamjibu ntasafiri j3 ijayo,na siku hiyo ilikuwa ni ijumaa,na nikachagua kusafiri kwa treni.Nitaendelea baadae