SEHEMU YA PILI:KUKURU KAKARA ZA MWANZA
Nilifika Mwanza mida ya saa 8 hivi mchana na nilimkuta dada yangu kaja kunipokea.Ilikuwa furaha kubwa sana na nilimkuta akiwa mja mzito,basi akaniambia tupitie tilapia hotel shemeji yako yuko hapo na kikao na rafiki zake.Dah nikafurahi sana.Tukafika tilapia,tukakaa baa ya juu na msosi ukaagizwa na vinywaji.Baada ya dakika 20 shemeji akaja,akanisalimia,tukafurahiana sana wakabusiana na mkewe,mie nikabaki kimya.Tukala na tukanywa sana na baada ya saa 2 hivi tukaondoka kwenda isamilo nyumbani.
Basi nikapewa room yangu ambayo ni ki detachment cha nyumba ya one bedroom,self contained,ina sitting room,ina kitchen yaani nipo kwenye ufalme wangu kabisa.Nilifikia kuoga na kulala hadi saa 2 usiku nikaamka,nikaenda main house nikamkuta dada na mme wake wakiangalia tv.Tukasalimiana,tukacheka sana,basi mida ya saa 3 usiku tukala vey light meal na nikaenda kulala.
Kesho yake nimeamka saa 3 asb nikamkuta dada ananiandalia chai,nikanywa vizuri tu.Dada akawa anajiandaa kwenda dukani kwake,huku namuona mimba ikimuendesha sawasawa,akaniambia nijiandae leo niwe dereva wake,nikamjibu sawa.Jamani mimba inamfanya mwanamke anawiri mno,dada alikuwa kapendeza mno na huo mtumbo,na shemeji alikuwa anauchezea huo mtumbo kila siku mie natazama,mfyuuuuu nasema ngoja muda wangu ufike.
Paaaa,hao mpaka shop kwa dada maeneo ya nyerere road,duka la nguo na vifaa vya urembo wa kina mama.
Dada akaniambia naweza kukaa kidogo na niwe huru kwenda kutembea na gari akanipa niwe natumia na nikapewa na pesa juu.
Mida ya saa 9 mchana nikaenda dukani kumchukua dada nimrejeshe home,by the way dada yangu aliolewa na mholanzi mmoja,ambae kwa sasa wanezeeka wakiishi ujerumani.
Wee basi hiyo wiki ya kwanza nilikula mademu 2 moto kweli kweli,mmoja alikuwa best ya dadangu,yena alikuwa ana kamimba kachanga,sijui ka nani maana mie sikumuuliza nilikuwa napakua tu mzigo.
Demu mwingine alikuwa mwalimu lake sekondari,nilimpata kimkandamkanda tu,naye nikala.
Baada ya wiki 2 dada yangu aliniita sebuleni,akanidodosa maswali mengi na alikuwa anajua kuwa mie ni mtu wa adivencha sana na alikuwa anajua sana kuwa nakula mademu sana.
Akaniuliza lini nategemea kurudi nje kwa masomo digirii ya pili,nikamjibu baada ya miezi 9 hivi maana natamani kupumzika,akaniambia anitafutie kibarua cha muda,nikamjibu sawa tu.Aisee kesho yake akanipeleka kwa muhindi mmoja wana duka mtaa wa uhuru,wanauza vifaa vya majumbani,na wote,yaani yeye na mkewe wanakuwa dukani pamoja.
Hao wahindi wakanipokea kwa furaha mno na wakanipa chai ya maziwa nikanywa,basi dada akanitambulisha kwao na wakaniuliza kama niliwahi kufanya kazi,nikawapa experience yangu ya nkansi na kirando so wakanipenda na kuniomba nianze kazi siku hiyohiyo