Nilivyokuwa najiona mjanja, nikaishia kutapeliwa Milioni 42

Maisha yako tofauti sana, unachopitia wewe usilazimishe na wenzako wawe wamepitia hiko hiko, natoa mfano kipindi naanza 1st year nilipewa laki 6 ya kuanzia maisha chuo maana mzazi alikua anajua Nina mkopo

Ila kuna jamaa nimesoma nae, chuo mwaka wa kwanza kwao alipangiwa nyumba nzima na alipewa gari Prado ya kutembelea, sasa akija huyo wa Prado kuelezea maisha yake ntatokea Mimi niliyepewa laki sita kuanza kubisha kua haiwezekani 1st year apewe Prado au haiwezekani 1st year apangiwe nyumba nzima, maisha yanatofautiana sana Kuna watu Wana pesa acheni kabisa!!

Mwaka Jana Twitter Kule Kuna mtoto wa kigogo mmoja alikua anawatukana watanzania kua wanaibiwa sana, akasema kwao kulikua na hela hawajui hata wapeleke wapi, anakwambia walikua wanatembea na milioni 20 kwenye buti za matumizi tu, hao ni watoto tu!!

Ukiona una maisha magumu au umepitia magumu usilazimishe Kila mtu awe ameishi kama wewe
 
Yes au hujawahi kununua wali sh 200 mwanzoni mwa miaka ya 2000..? Au isije ikawa naongea ma mtoto uliyezaliwa mwaka 2000!
Mwanzoni wa miaka ya 2000 ni kuazia lini hadi lini?

Anyway hii story sio kuwa ni ya uongo kwa sababu ya bei ya chakula pekee, kukopesha wanafunzi 5000 wakulipe 15000 ndio niliposema uongo umekithiri, ila unaweza kuamua kuamini kama unataka sio kesi
 
Pamoja na kusokotwa itoshe kusema biashara ipo damuni kwako, maarifa na uwezo wa kuzalisha faida kutokana na mtaji unao, kama uliweza kugraduate ukiwa na 50m basi uko vizuri, kuna watu hizo wanazishika baada ya kuvuja jasho kwa miaka isiyopungua 30
Umeiamini hii stori ya uongo?
 
Nilikuwa najiona mimi ndiye nilikuwa smart kutafuta pesa kipindi niko shule kumbe watu mlikuwa smart zaidi 😂😂😂.. Hii ya kukodisha simu kuangalia X sikuwahi kuiwaza kabisa..

Respect the hustle aisee!!
Umeiamini hii stori ya uongo?
 
Kuna walokuja kuja mjini na gari la kura enzi za magu basi ndo wenye kubisha na kujifanya wajuvi wa kila kitu humu jf umeona ya kutunga ,sijui uongo haya unafanya nini huku Tajiri ,,tuondoleeeni ugumu wenu wa fikra kwa kulazimisha yasowahusu ,haya tungeni yenu basi woiiiii
 
sawa mzee. Ngoja nianze kujikita kwenye sanaa hii ya utunzi wa nakala mbalimbali nikibobea nitakutafuta unaipe mkuu wa kike moja akiwa na bikra yake
 
Kwa hiyo tukubali tu jamaa alikuwa na simu nne shuleni na alifanya biashara ya kuonyesha porn bila kushtukiwa kwa miaka yote aliyosoma?
 
Kwanza nikupongeze kwa juhudi za kutafuta pesa toka O-Level,
Pili,ningependa kujua mwaka ulioingia chuoni na jina la Chuo ulichosoma ambacho kilikua na utaratibu kwa wanafunzi kwenda kuchukua Pesa za Boom kwa muhasibu badala ya kuwekewa kwenye account.
 
Ngoja nikupe elimu kidogo, miaka ya nyuma kidogo wanafunzi wakifika 1st year wengi walikua hawana account, hii ikapelekea boom la kwanza+ pesa za stationary kua mnapewa kwa utaratibu wa kupanga foleni na kuchukua pesa kwa mhasibu mkononi, hii ilikua boom la kwanza tu, la pili lazima uwe ushafungua akaunti linaingia huko....baada ya 1st year wengi kua wanapoteza na kuibiana hizi pesa ikaja sheria miaka ya mbele kidogo kua lazima ufungue akaunti kwanza ndo unawekewa pesa zako huu utaratibu ukafia hapo!

Nadhani waliopitia vyuoni miaka Hio kama Mkono Mmoja huu utaratibu sio mgeni kwao
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu,ndio maana niliuliza mwaka na jina la chuo nilikua sijui kama zamani boom lilikua linapokelewa kwa muhasibu.
 
kwa hiyo mwamba inawezekana ulikuwa bingwa wa kuibia wenzako...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…