Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,973
- 2,239
Interested
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh [emoji23][emoji23][emoji23]Saaana!!!
Rate ni kama 3000 kwa dakika 15
kwa dhaman ya hela leo
Kwamba story yake toka akiwa tumboniStory inaweza kuwa chai lakini ukikosoanuwe na uhakika na hiyo taarifa unayoikosoa.
Halafu pasaka hii wacha watu wafurahi kidogo...
Anyway, kuna watu huwa wana mastory yao ya hivi kumbe wanataka kupiga watu nakumbuka story za forex za yule wa kudownload noti alianzia story zake tangu yupo tumboni hajazaliwa, vidudu, primary o level advance, jeshini chuo kumbe dah....majanga pia kuna wengine wanataka kushare experience.... mtu akipigwa si atajijua mwenyewe tuuu....
Kama yako kiongoziSikujui kijana nieleze status yako..
Watanzania shida ni moja ujuajiMaisha yako tofauti sana, unachopitia wewe usilazimishe na wenzako wawe wamepitia hiko hiko, natoa mfano kipindi naanza 1st year nilipewa laki 6 ya kuanzia maisha chuo maana mzazi alikua anajua Nina mkopo
Ila kuna jamaa nimesoma nae, chuo mwaka wa kwanza kwao alipangiwa nyumba nzima na alipewa gari Prado ya kutembelea, sasa akija huyo wa Prado kuelezea maisha yake ntatokea Mimi niliyepewa laki sita kuanza kubisha kua haiwezekani 1st year apewe Prado au haiwezekani 1st year apangiwe nyumba nzima, maisha yanatofautiana sana Kuna watu Wana pesa acheni kabisa!!
Mwaka Jana Twitter Kule Kuna mtoto wa kigogo mmoja alikua anawatukana watanzania kua wanaibiwa sana, akasema kwao kulikua na hela hawajui hata wapeleke wapi, anakwambia walikua wanatembea na milioni 20 kwenye buti za matumizi tu, hao ni watoto tu!!
Ukiona una maisha magumu au umepitia magumu usilazimishe Kila mtu awe ameishi kama wewe
Kipindi hicho L7 unyama mwingiMoto L7 2006 hiyo. Nilinunua Uhindini mbeya 230,000. Simu ilikuwa inabamba ile mbaya!
Kuna siku nilikoswa koswa kungongwa gari pale pile jamaa ndo kala kona junction ya mafiati anaitafuta st francis mimi niko zangu busy nakula good music kwa earphone ngoma ya Rihanna "pon-de-reply" nimepakua kwa internet kupitia waptrick...!
umeulizwa mengine umejibu mengine.Ngoja nikupe elimu kidogo, miaka ya nyuma kidogo wanafunzi wakifika 1st year wengi walikua hawana account, hii ikapelekea boom la kwanza+ pesa za stationary kua mnapewa kwa utaratibu wa kupanga foleni na kuchukua pesa kwa mhasibu mkononi, hii ilikua boom la kwanza tu, la pili lazima uwe ushafungua akaunti linaingia huko....baada ya 1st year wengi kua wanapoteza na kuibiana hizi pesa ikaja sheria miaka ya mbele kidogo kua lazima ufungue akaunti kwanza ndo unawekewa pesa zako huu utaratibu ukafia hapo!
Nadhani waliopitia vyuoni miaka Hio kama Mkono Mmoja huu utaratibu sio mgeni kwao
benki vipi??Am waiting ila mwendo uliumaliza mara baada ya kujihusisha na biashara ya kidhalimu ya kukopesha kwa riba!! Riba haijawahi kumuacha mtu salama .
Ule Uzi wa forex ulikuwa noma. Hadi ma vyeti ya shule yaliwekwa kumbe dah.....Kwamba story yake toka akiwa tumboni
😅😅😅 Ila kuna watu mnaubongo mzito sana. Halafu hamjuagi kujificha.Kwa mamlaka niliyojipa ninautangazia umma kuwa huu uzi ni chai... tuusome kwa kujifurahisha tu hakuna uhalisia wowote hapa.
1. Form one alienda akiwa hajui kama shule haina wanafunzi wa kike. Wasichana kutokuwa admitted ni badiliko kubwa sana ambalo huwa sio la siri. Chai no. 1
2. Chakula Tsh 200 canteen. Kama alisoma wakati wa iPad zinatoka ni kwamba sio miaka mingi iliyopita. Kukadiria ni kama 2010 kuendelea. Vyuoni misosi ilikua Tsh 1000 na zaidi. Hakukuwa na uwezekano upate kwa Tsh 200 wali maharage hata kwa shule za sekondari. Au ilikuwa ni Ihefu sec school? Chai no.2
3. Biashara ya mkopo kwenda smoothly bila mgogoro wowote ni Chai no.3 kwenye biashara ya mikopo lazima watokee wasumbufu. Labda kama wateja ni malaika.
4. Kumiliki simu 4 maalum kwa kutazama porn shuleni ni Chai no.4 hii isingeweza kuwa siri kwa vyovyote vile lazima lingemfikia mwalimu wa nidhamu. Katika wanafunzi kuna wenye maadili wasingelifumbia macho. Kuna wenye wivu na pesa unazopiga wasingekaa kimya. Kimsingi hustles za ndugu mwandishi wakati wa secondary zimetawaliwa na chai.
Kwa hustles za Chuo sina tatizo nazo maana angalau zinawezekana.