Muuza Viat
JF-Expert Member
- Dec 23, 2022
- 2,826
- 7,388
Uzur wa askar wanakamua pande zoteHongera sana mkuu kwa upambanaji maana umenikumbusha miaka ya nyuma kidogo nikiwa chalii mdogo kuna bro wangu alikuwa South Africa alikuwa ananitumia mzigo wa simu used kama vile Blackberry, Soni Xperia, Nokia, Samsung na iphone.
Ikumbukwe kwamba hizi simu nilizooredhesha hapa ni matoleo ya mwanzo kabisa kipindi zinaingilia tu lakini zilikuwa za moto kwa wakati wake.
Nilikuwa naweza kuuza simu moja nikapata faida hadi 150k baada ya kutoa gharama na faida ya bro aliyokuwa anahitaji.
Sasa hapo unakuta kaleta mzigo mkubwa na mzigo haukai ni oda za watu yaani ukifika tu ushaisha naweka changu mfukoni namtumia pesa yake kupitia Western Union ama Money gram.
Baadae biashara ikakuwa akawa ananitumia hadi laptop na ps kipindi zimeingilia tu huku kwetu Bongo bado ni wachache wanamiliki.
Nilikuwa napiga hela hadi najisemea imependelewa na Mungu aise maana watu wanakukabidhi pesa kabla mzigo haujaja na mzigo ukitua tu nawapigia simu wanafata home kwetu.
Matapeli wa Sinza wakataka kuniingiza mjini lakini namshukuru Mungu walirudisha mzigo baada ya kuchukua askari nakuanza msaka maana nilipewa details zao mwisho wa siku mmoja wao aliingia 18 za polisi maeneo ya Mlimani City akakamatwa ndo akatupeleka kwa wenzie bahati nzuri walikuwa hawajauza mzigo nikaukagua nikabaini ni wenyewe askari wakasema hawa matapeli tuachie sisi tutawakamua ipasavyo.
Ww wamekukamua na hao wezi na wamekamuliwa