Nilivyokuwa najiona mjanja, nikaishia kutapeliwa Milioni 42

Nilivyokuwa najiona mjanja, nikaishia kutapeliwa Milioni 42

Hongera sana mkuu kwa upambanaji maana umenikumbusha miaka ya nyuma kidogo nikiwa chalii mdogo kuna bro wangu alikuwa South Africa alikuwa ananitumia mzigo wa simu used kama vile Blackberry, Soni Xperia, Nokia, Samsung na iphone.

Ikumbukwe kwamba hizi simu nilizooredhesha hapa ni matoleo ya mwanzo kabisa kipindi zinaingilia tu lakini zilikuwa za moto kwa wakati wake.

Nilikuwa naweza kuuza simu moja nikapata faida hadi 150k baada ya kutoa gharama na faida ya bro aliyokuwa anahitaji.

Sasa hapo unakuta kaleta mzigo mkubwa na mzigo haukai ni oda za watu yaani ukifika tu ushaisha naweka changu mfukoni namtumia pesa yake kupitia Western Union ama Money gram.

Baadae biashara ikakuwa akawa ananitumia hadi laptop na ps kipindi zimeingilia tu huku kwetu Bongo bado ni wachache wanamiliki.

Nilikuwa napiga hela hadi najisemea imependelewa na Mungu aise maana watu wanakukabidhi pesa kabla mzigo haujaja na mzigo ukitua tu nawapigia simu wanafata home kwetu.

Matapeli wa Sinza wakataka kuniingiza mjini lakini namshukuru Mungu walirudisha mzigo baada ya kuchukua askari nakuanza msaka maana nilipewa details zao mwisho wa siku mmoja wao aliingia 18 za polisi maeneo ya Mlimani City akakamatwa ndo akatupeleka kwa wenzie bahati nzuri walikuwa hawajauza mzigo nikaukagua nikabaini ni wenyewe askari wakasema hawa matapeli tuachie sisi tutawakamua ipasavyo.
Uzur wa askar wanakamua pande zote

Ww wamekukamua na hao wezi na wamekamuliwa
 
Enzi hizo ku "deep" (ku beep imekuja juzi tu)ilikuwa sh. 100 kupiga unahesabiwa dakika aisee
Na ikatoka kamba unaning'iniza simu shingoni ilikuwa unyama sana,[emoji1787],, mkuu shusha uzi wahenga tunakuelewa hawa watt waloveshwa "pampasi" hawawezi kuelewa vitabisha tu
 
Enzi hizo.kijijini unawatumia vocha ya buku 5.
Then.wanaenda.kuiuza
Hakukuwa cha mpesa Wala tigo pesa
 
Kwa mamlaka niliyojipa ninautangazia umma kuwa huu uzi ni chai... tuusome kwa kujifurahisha tu hakuna uhalisia wowote hapa.

1. Form one alienda akiwa hajui kama shule haina wanafunzi wa kike. Wasichana kutokuwa admitted ni badiliko kubwa sana ambalo huwa sio la siri. Chai no. 1
2. Chakula Tsh 200 canteen. Kama alisoma wakati wa iPad zinatoka ni kwamba sio miaka mingi iliyopita. Kukadiria ni kama 2010 kuendelea. Vyuoni misosi ilikua Tsh 1000 na zaidi. Hakukuwa na uwezekano upate kwa Tsh 200 wali maharage hata kwa shule za sekondari. Au ilikuwa ni Ihefu sec school? Chai no.2
3. Biashara ya mkopo kwenda smoothly bila mgogoro wowote ni Chai no.3 kwenye biashara ya mikopo lazima watokee wasumbufu. Labda kama wateja ni malaika.
4. Kumiliki simu 4 maalum kwa kutazama porn shuleni ni Chai no.4 hii isingeweza kuwa siri kwa vyovyote vile lazima lingemfikia mwalimu wa nidhamu. Katika wanafunzi kuna wenye maadili wasingelifumbia macho. Kuna wenye wivu na pesa unazopiga wasingekaa kimya. Kimsingi hustles za ndugu mwandishi wakati wa secondary zimetawaliwa na chai.

Kwa hustles za Chuo sina tatizo nazo maana angalau zinawezekana.
Labda sio Azania ,pugu na shule zinazofanana na hizo sisi simu ikiibwa hakuna ku report popote utajua namna ya kuitafuta,Kila mwanafunzi wa advance ruksa kuwa na simu,ikiita darasani teacher anachukua weka simu silence ,na o level waliokuwa hostel wanapitia mwanya huo kuwa na simu,hakuna kuhesabiwa,darasani kuingia ni hiari,pared wanahuhuria form six na form four wakiwa kwenye mitihani,Kila mwanafunzi utamkuta kwenye chimbo anapiga msuli(soma Kwa bidii),unapishana na teacher unaenda tution yeye anaingia shuleni ,Kuna wanafunzi wanakuja na magari wakitoka nyumbani haswa week end na wanayapaki karibu na gari la mkuu wa shule,naongelea 2000-2006
 
Mwanzoni wa miaka ya 2000 ni kuazia lini hadi lini?

Anyway hii story sio kuwa ni ya uongo kwa sababu ya bei ya chakula pekee, kukopesha wanafunzi 5000 wakulipe 15000 ndio niliposema uongo umekithiri, ila unaweza kuamua kuamini kama unataka sio kesi
Mwanafunzi anayekopeshwa yeye hafanyi biashara akirudi baada ya likizo analipa mbona ni jambo la kawaida
 
Umesema kipindi hicho ilikuwa sahani ya wali unanunua 200, so 5k ya kipindi hicho ni kama 50k ya sasa

Halafu unamkopesha mtu elfu 5 (50k ya sasa) wakawa wanakulipa 15k (150k ya sasa) na biashara ikawa kubwa?

Yaani hapa ndipo nilipoishia kusoma hii story, hii ni chai ambayo haina sukari,.😂😂😂 Hiyo biashara ungefilisika baada ya muhula mmoja tu
Naongea haya kwa sababu nina experience na biashara ya kukopesha pia

Ukikoesha watu hela tena kwa riba kubwa bila kuwa na dhamana inayoweza kuuzwa kirahisi hapo jiandikishie kufilisika

Haya mnaoamini hii ni kweli nitoleeni povu
Kwel man anatuzungusha na kistory kisicho na maana ili tumuone mjanja tusahau yy n mshamba na wajanja walmchapa mil 40£
 
Boss nimesoma Govt kuanzia msingi hadi chuo. Form 1 & 6 nimesoma bweni shule tofauti 3 zote za serikali. Hakuna utakachoniambia kuhusu shule za serikali. Niko Form one mwaka 1999 shule nzima hakuna mwenye simu. Mimi nitaendelea tu kusoma uzi wako mwingine kama burudani tu ila sio kuamini ulichoandika.
shule nzima uliwezaje kuhakikisha Kila mwanafunzi Hana simu? Mtandao kwenye kijiji ilipo shule yenu ulikuwepo? Mimi Form one 2000 na nilikua na simu, simu zilikuwepo Ila chache sana
 
shule nzima uliwezaje kuhakikisha Kila mwanafunzi Hana simu? Mtandao kwenye kijiji ilipo shule yenu ulikuwepo? Mimi Form one 2000 na nilikua na simu, simu zilikuwepo Ila chache sana
Sema wenzetu wengine mlikuwa wakishua unajua hii miaka unanunua simu unaweka ndani unatafuta hela kununua line(simu card) nakumbuka nilikuwa primary shule nzima simu alikuwa nayo mwalimu mmoja tu limche la sabuni lilikuwa likaa kwenye gari tunaenda kulichungulia tu kwenye vioo
Sasa akaja kuibiwa sijui ni pupils ndio waliipiga staff wenzie shule nzima tuliitwa assembly tukatangaziwa hiyo mikwala yake sasa yaani uuuuwiiiiii mixer kutishia kwa mganga lkn aliambulia hamna!!!
 
Umesema kipindi hicho ilikuwa sahani ya wali unanunua 200, so 5k ya kipindi hicho ni kama 50k ya sasa

Halafu unamkopesha mtu elfu 5 (50k ya sasa) wakawa wanakulipa 15k (150k ya sasa) na biashara ikawa kubwa?

Yaani hapa ndipo nilipoishia kusoma hii story, hii ni chai ambayo haina sukari,.😂😂😂 Hiyo biashara ungefilisika baada ya muhula mmoja tu
Naongea haya kwa sababu nina experience na biashara ya kukopesha pia

Ukikoesha watu hela tena kwa riba kubwa bila kuwa na dhamana inayoweza kuuzwa kirahisi hapo jiandikishie kufilisika

Haya mnaoamini hii ni kweli nitoleeni povu
nawaomba asilaumiwe huyu ndo uwezo wake kufikiria umeishia hpa
 
Na ilikuwa haiitwi vocha iliitwa "dola" [emoji1787] ...nikikumbuka zile shiva jero jero nachoka zaidi enzi za buzz ni bomba , ...simu iliitwa longa longa ......
Airtel sijui walikuwa na jina gani aisee, kabla hawajatulia na jina lao hili walikuwa wanabadili badili majina ya brand zao kila mara. Mambo ya buzz ni bomba aisee [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
shule nzima uliwezaje kuhakikisha Kila mwanafunzi Hana simu? Mtandao kwenye kijiji ilipo shule yenu ulikuwepo? Mimi Form one 2000 na nilikua na simu, simu zilikuwepo Ila chache sana
Ht mm mwaka huo form one na nilikuwa namiliki simu na nimedumu nayo mpk chuo ndio nikabadilisha. Na hiyo simu nilipewa na mzazi.
 
Na ilikuwa haiitwi vocha iliitwa "dola" [emoji1787] ...nikikumbuka zile shiva jero jero nachoka zaidi enzi za buzz ni bomba , ...simu iliitwa longa longa ......
Airtel enzi hizo ni celtel jamani hahahhahahaha
 
Boss nimesoma Govt kuanzia msingi hadi chuo. Form 1 & 6 nimesoma bweni shule tofauti 3 zote za serikali. Hakuna utakachoniambia kuhusu shule za serikali. Niko Form one mwaka 1999 shule nzima hakuna mwenye simu. Mimi nitaendelea tu kusoma uzi wako mwingine kama burudani tu ila sio kuamini ulichoandika.
Punguza ubishi we jamaa, walimu tumeona vingi
 
Boss nimesoma Govt kuanzia msingi hadi chuo. Form 1 & 6 nimesoma bweni shule tofauti 3 zote za serikali. Hakuna utakachoniambia kuhusu shule za serikali. Niko Form one mwaka 1999 shule nzima hakuna mwenye simu. Mimi nitaendelea tu kusoma uzi wako mwingine kama burudani tu ila sio kuamini ulichoandika.
Mleta uzi km angesoma shule yenu pengine hu uzi tusingeufaidi
 
Back
Top Bottom