Pesa inatengenezwa pale ambapo wengine hawawezi kudhani inawezekana.
Hivi unadhani kwa akili ya kawaida tu ile over invoice ya ATCL kwenye uhalisia wa kawaida unaweza kudhani mtu/watu anaweza/wanaweza kuyafanya yale??
Nimeona hoja yako hapo juu labda nisaidie kumjibia mleta uzi.
2. Hiyo miaka ya 2010 alivyokuwa anauza Ipad kama wali ulikuwa 1,000 tena chuoni, unashindwaje kuamini miaka 7 au 8 nyuma wali kuwa 200 kwenye canteen za shule za sekondari??
4. Mimi nimesoma Private School, tena hapahapa Dar yenye kila aina ya usimamizi na nidhamu. Lakini nilifanya biashara ya kuuza pipi (Ivory) na vyakula kama Sambusa na Chipsi kwa miaka mitatu kuanzia Form Two mpaka Form Four bila hata kushtukiwa. Ile shule ilikuwa ukiruka tu ukuta uingie mtaani wale wa mtaani iwe raia au hata walinzi wa shule wakikukamata na wakakupeleka shuleni wanalipwa laki moja cash (kwa kulisema hili nadhani waliosoma ile shule kama wapo hapa watakuwa wameijua) ila kwa mazingira hayohayo magumu mimi na biashara yangu ilisurvive kwa miaka mitatu na ilikuwa lazima hii mizigo ifuatwe nje na ije kuuzwa shuleni. Kuna mbinu nyingi sana nilikuwa natumia, nilinunua viongozi wa dormitories pamoja na maprefects ikiwemo Head Boy, nilijenga urafiki na Patrons ingawa hawakujua ninachofanya. Nilifanya hivyo makusudi ili wale spies directly wasiweze kuwa threat kwangu sababu walijua wakienda either kwa maprefects au Patrons kunichongea lazima habari zitanifikia. So kwa upande wa jamaa tena shule za serikali ambazo walimu wapo busy na mambo yao sidhani kama inashindikana jamaa alichokifanya.
Kitu kinachotenganisha utajiri na umaskini ni UTHUBUTU tu. Maskini wamekariri njia rahisi na salama kupata pesa ila matajiri ni tofauti. Maskini ni muoga, anaogopa kupoteza alichonacho, tajiri yeye plan yake anaangalia atachopata kwanza sio alichonacho mkononi.