Kwa mamlaka niliyojipa ninautangazia umma kuwa huu uzi ni chai... tuusome kwa kujifurahisha tu hakuna uhalisia wowote hapa.
1. Form one alienda akiwa hajui kama shule haina wanafunzi wa kike. Wasichana kutokuwa admitted ni badiliko kubwa sana ambalo huwa sio la siri. Chai no. 1
2. Chakula Tsh 200 canteen. Kama alisoma wakati wa iPad zinatoka ni kwamba sio miaka mingi iliyopita. Kukadiria ni kama 2010 kuendelea. Vyuoni misosi ilikua Tsh 1000 na zaidi. Hakukuwa na uwezekano upate kwa Tsh 200 wali maharage hata kwa shule za sekondari. Au ilikuwa ni Ihefu sec school? Chai no.2
3. Biashara ya mkopo kwenda smoothly bila mgogoro wowote ni Chai no.3 kwenye biashara ya mikopo lazima watokee wasumbufu. Labda kama wateja ni malaika.
4. Kumiliki simu 4 maalum kwa kutazama porn shuleni ni Chai no.4 hii isingeweza kuwa siri kwa vyovyote vile lazima lingemfikia mwalimu wa nidhamu. Katika wanafunzi kuna wenye maadili wasingelifumbia macho. Kuna wenye wivu na pesa unazopiga wasingekaa kimya. Kimsingi hustles za ndugu mwandishi wakati wa secondary zimetawaliwa na chai.
Kwa hustles za Chuo sina tatizo nazo maana angalau zinawezekana.