Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Ukapelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali hahahahaha! Kuna mshikaji wangu alikuwa anajiita mkemia. Yaani jinsi alivyokuwa mzoefu wa kupima kete kwenye mzani alikuwa anajiita mkemia. Akikaa pale sebleni na boxer tu huku akiwa kifua wazi na savana yake pembeni na kuanza kupima sembe kwenye mzani, utasikia anakuambia "mkemia nipo kazini"
Unfortunately wengi wao huwa wanaishia kuwa mateja

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona unanishambulia, Bwanga ukiacha kuelekea chato, unaenda katoro Buseresere/ katoro geita, sengerema, mwanza, mwanza unaweza kuamua uende Musoma then upite mbugani serengeti ili utokee geneva of africa, au urudi utokee Bariadi/simiyu uingie Arusha kupitia loriondo. Bado unaswali? Kule juu nimetaja njia ya Runzewe lakini unaweza kukatisha njia ya vumbi ushirombo kutokea katoro ukaendelea na safari zako
Mkuu lakini si nilisema tunataniana tu mkuu? Kumbe mwenzangu umeni-mind kihivyo? Nikashangaa na jomba mwingine naye kaingia kichwa kichwa kuniita mbwiga nikabaki namshangaa! Mimi nikichokataa mkuu ni hiyo route yako, maana ulivyokuwa unaidadavua ulikuwa inaonesha kabisa unaenda mpaka ukatokezee Mtukula, sasa ulivyofika Bwanga ukala kona kwenda Geita nikabaki nashangaa huo mzunguko wa nini?
 
Hahahaha tunajilipua ila ndo kivingine wanawake wengi wamefika huko kwa kutumia (mahusiano), hivyo njia yao huwa rahisi kidogo, tumeumbwa kwa udongo laini Sana kuhimili hiyo mikiki ndugu yangu
Honestly siwezi kurisk maisha yangu hivyo, (labda maisha hayajanichapa sawasawa, ama mazingira niliyokulia no)

Wewe jilipue ili ututoe kimasomaso🤩🤩
Mie nilishajilipua..nadhani nna damu hiyo kwakweli..
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Niliishi pale kwa jamaa kama Wiki mbili hivi, Story zao zote ni kuhusu Dawa tu. Aisee nilichoka. Nikasema hapa lazima nitoke. Sijajilipua kuja South kuja kuuza Dawa, Nikasema hata nyumbani wakisikia nimekamatwa kwa kesi ya dawa watanishangaa sana. Kama nimeweza kutoka Bongo mpaka South, Sasa nishindwe nini kutoka hapa kwa Washkaji kwenda sehemu nyengine.

Basi taratibu nilipanga kutafuta Marafiki wengine ambao sio wabongo. Niliona labda nikibadilisha watu nitasikia story nyengine tofauti na Madawa. Nikawa muda mwingi najichanganya na watu wengine. Ukiwa South halafu ukianza kufanya mambo tofauti na wengine lazima wabongo wenzio watachukia. Lakini nilijilipua tena kwa Mara ya pili. Liwalo na Liwe, wakichukia poa tu.

Niseme ukweli wakati natoka Bongo, Kichwani nilikuwa na Mipango miwili ya namna ya kupata Mchongo kwa urahisi. Mpango wa kwanza lilikuwa endapo nitachelewa kupata Mchongo basi niende nikajisalimishe kwenye Kanisa lolote. Ukweli nilipanga kwamba endapo nitakosa watu sahihi wa kunisaidia kufikia malengo yangu basi niwe mtu wa kwenda sana Kanisani ili kupata watu sahihi huko. Nilipanga kujisogeza kwa washua wale wa Makanisani. Nilijua washua wengi wenye Biashara zao Halali au Taasisi zao nitawapata huko.

Mpango wangu wa Pili ilikuwa kama nitachelewa kupata Mchongo basi nitafute Mrembo mwenye Kazi yake, nimpe mapenzi kama yote mpaka anipende na kunisaidia kupata Mchongo. Mjumbe hauwawi ndo yalikuwa mawazo yangu.

Nikaanza na hili la Kwanza la kutafuta Kanisa la Washua. Kumbuka Safari hii nilifanya Karibia na Sherehe za X-Mass na Mwaka Mpya, Nilifanya Karibia tarehe hizo Makusudi. Nilijua kwenye Mikesha ya Kanisani, Mkesha wa X-Mass na Mwaka Mpya lazima nitapata mtu wa kunisaidia. Basi tarehe zikasogea mpaka X-Mass ikafika. Niliwaaga wale jamaa zangu kuwa naenda kwenye Mkesha. Jamaa walinishangaa sana kwa sababu wao hawanaga mambo hayo. Tena siku niliyowaambia kuwa nakwenda kwenye Mkesha tulikuwa tumetoka wote kutembea Mitaa ya Midrand Gauteng. Midrand ipo Katikati ya Pretoria na Joberg. Ni kama dakika 20 kutoka Pretoria. Kuna Umbali kidogo sema wenzetu kwa kuwa Barabara zao nzuri ndo unatumia dakika hizi 20, Ingekuwa hapa kwetu ni umbali wa Kama kutoka Tegeta mpaka Magomeni.

Tukiwa huko Midrand ndo niliwaambia hivyo, Wakati wakuondoka wenyewe wakaondoka Mimi wakaniacha pale Midrand. Nikaanza kuzurura zangu Mitaani nauliza watu wapi nitapata Kanisa kubwa. Nilikuwa natafuta Kanisa ambalo ukiliona tu kwa nje unajua hili ni Kanisa la Washua. Sikutaka haya Makanisa Madogo Madogo.

Nilifanya yote haya ili kujiepusha na Biashara ya Dawa, ilibidi niangaike sana pale. Unajua Wabongo wengi wanajikuta wakiingia kwenye Biashara za Dawa kwa Mtindo kama huu, Yan ukifika ukakutana na Wabongo wenzio hawakupi nafasi ya kujipambania zaidi. Sasa kama wewe ni kichwa panzi basi unaishia kwenye biashara hiyo.

Mimi nilisema nitapambana mpaka dakika ya mwisho, swala la Kibali cha Kazi nitajua mbele kwa Mbele.

Basi nikafika mpaka pale Kanisani. Kuliona tu kwa nje nikajisemea hili ndo nilikuwa nalitafuta. Parking ilikuwa na Gari za Kifahari Kibao. Nikauliza Muda wa kuanza Ibada ya Mkesha wakaniambia kuwa ni saa moja usiku watu ndo wanaanza kuingia Kanisani. Washua Kibao walikuwa wamewahi pale, wamesimama kwa nje wakipiga story zao. Mimi nikasoma mazingira kisha nikatoka, nikazunguka zunguka pale Mitaani mpaka saa moja jioni ilivyofika nikarudi tena. Nikatimba zangu ndani.

Kama ilivyokawaida ya Makanisa mengi, mtu ukifika kwa Mara ya kwanza inabidi ujitambulishe. Tulisimama pale Kanisani kama wageni 50 hivi ndo ilikuwa Mara etu ya kwanza kufika pale. Baada ya kusimama na kujitambulisha kisha tulikaa. Wahudumu wa Kanisa wakawa wanapita kwenye kila Mstari kuchukua maelezo yetu. Nakumbuka kwangu alipita Msichana Mrembo hivi. Nilipomwambia kuwa Mimi ni Mtanzania na ndo nimefika south kwa Mara ya kwanza, alifurahi. Kwenye ile form yao nilijaza namba yangu ya simu. Wakuu kwa upande wa Lugha ya Kizungu siko vibaya sana. Naweza kujitetea kiasi chake.

Utaratibu mwengine wa lile Kanisa kwa mtu aliyefika Mara ya kwanza, wakati unajaza ile form yao wanakuuliza "Je kwenye hili Kanisa letu wewe utatusaidia upande upi?" Wakiwa na Maana Kama utaweza kujitolea mfano kufanya upande wa Media, Yan walikuwa wana Camera za kutosha mle ndani, Kanisa lilikuwa linaruka LIVE kwenye Mitandao ya Kijamii. Pia walikuwa wanataka kujua kama utajitolea kwenye upande wa Muziki sababu walikuwa na Kwaya yao na vyombo vyote vya Mziki. Kama wewe ulikuwa mtaalamu wa Maswala hayo ya Mziki basi utapangiwa huko.

Kwa hiyo ndani ya Kanisa Idara zilikuwa nyingi. Nikaona hapa nitumie fursa vizuri, Kwa kuwa Mimi nina taaluma Fulani ya Mambo ya Camera nikasema Mimi nitajitolea kwenye eneo hili. Yule Mrembo alifurahi kusikia hivyo. Akaniandikisha pale kisha akaondoka.

Ukweli Kanisa lilikuwa la Kishua na limechangamka sana. Kanisa lilikuwa na Gari la kwenda kuwachukua na kuwarudisha waumini wake.
 
Jamaa anakuambia Dubai alikuwa gym trainer,bouncer club, errand boy,Kuwadi, Mwizi ..walevi wakilewa club wakileta vurugu time anawatoa nje anawasachi ...Ukuwadi Ni pale washkaji watakapotaka mademu wa kiafrica wenye Mizigo ya kuvunja chaga.. Anaongea na manzi kuwa jamaa atakupa 150 dollars wewe si huwa unachukua 100 dollars 50 Ni yangu.
Hahaha ngoja nikawe gym trainer Dubai au Qatar Mkuu... au unashaurije , wengi tunatamani kusafiri nchi za mbali....
 
Ukapelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali hahahahaha! Kuna mshikaji wangu alikuwa anajiita mkemia. Yaani jinsi alivyokuwa mzoefu wa kupima kete kwenye mzani alikuwa anajiita mkemia. Akikaa pale sebleni na boxer tu huku akiwa kifua wazi na savana yake pembeni na kuanza kupima sembe kwenye mzani, utasikia anakuambia "mkemia nipo kazini"
[emoji3][emoji3][emoji119][emoji119]
 
🤣🤣 nilijipua hapa hapa tz...huko karibubna kwenu
Itabidi utoke nje ya tz Sasa, km huko south nk ila nasikia usalama Ni mdogo Sana

Nasubiri corona ipoe nami nikasafishe nyota sio kwa gundu hili, ila yangu siwezi kuiweka Kama kujilipua Ni safari ya kawaida tu japo Ni ya kwenda kuanza maisha mapya kwenye dunia za watu huko
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Niliishi pale kwa jamaa kama Wiki mbili hivi, Story zao zote ni kuhusu Dawa tu. Aisee nilichoka. Nikasema hapa lazima nitoke. Sijajilipua kuja South kuja kuuza Dawa, Nikasema hata nyumbani wakisikia nimekamatwa kwa kesi ya dawa watanishangaa sana. Kama nimeweza kutoka Bongo mpaka South, Sasa nishindwe nini kutoka hapa kwa Washkaji kwenda sehemu nyengine.

Basi taratibu nilipanga kutafuta Marafiki wengine ambao sio wabongo. Niliona labda nikibadilisha watu nitasikia story nyengine tofauti na Madawa. Nikawa muda mwingi najichanganya na watu wengine. Ukiwa South halafu ukianza kufanya mambo tofauti na wengine lazima wabongo wenzio watachukia. Lakini nilijilipua tena kwa Mara ya pili. Liwalo na Liwe, wakichukia poa tu.

Niseme ukweli wakati natoka Bongo, Kichwani nilikuwa na Mipango miwili ya namna ya kupata Mchongo kwa urahisi. Mpango wa kwanza lilikuwa endapo nitachelewa kupata Mchongo basi niende nikajisalimishe kwenye Kanisa lolote. Ukweli nilipanga kwamba endapo nitakosa watu sahihi wa kunisaidia kufikia malengo yangu basi niwe mtu wa kwenda sana Kanisani ili kupata watu sahihi huko. Nilipanga kujisogeza kwa washua wale wa Makanisani. Nilijua washua wengi wenye Biashara zao Halali au Taasisi zao nitawapata huko.

Mpango wangu wa Pili ilikuwa kama nitachelewa kupata Mchongo basi nitafute Mrembo mwenye Kazi yake, nimpe mapenzi kama yote mpaka anipende na kunisaidia kupata Mchongo. Mjumbe hauwawi ndo yalikuwa mawazo yangu.

Nikaanza na hili la Kwanza la kutafuta Kanisa la Washua. Kumbuka Safari hii nilifanya Karibia na Sherehe za X-Mass na Mwaka Mpya, Nilifanya Karibia tarehe hizo Makusudi. Nilijua kwenye Mikesha ya Kanisani, Mkesha wa X-Mass na Mwaka Mpya lazima nitapata mtu wa kunisaidia. Basi tarehe zikasogea mpaka X-Mass ikafika. Niliwaaga wale jamaa zangu kuwa naenda kwenye Mkesha. Jamaa walinishangaa sana kwa sababu wao hawanaga mambo hayo. Tena siku niliyowaambia kuwa nakwenda kwenye Mkesha tulikuwa tumetoka wote kutembea Mitaa ya Midrand Gauteng. Midrand ipo Katikati ya Pretoria na Joberg. Ni kama dakika 20 kutoka Pretoria. Kuna Umbali kidogo sema wenzetu kwa kuwa Barabara zao nzuri ndo unatumia dakika hizi 20, Ingekuwa hapa kwetu ni umbali wa Kama kutoka Tegeta mpaka Magomeni.

Tukiwa huko Midrand ndo niliwaambia hivyo, Wakati wakuondoka wenyewe wakaondoka Mimi wakaniacha pale Midrand. Nikaanza kuzurura zangu Mitaani nauliza watu wapi nitapata Kanisa kubwa. Nilikuwa natafuta Kanisa ambalo ukiliona tu kwa nje unajua hili ni Kanisa la Washua. Sikutaka haya Makanisa Madogo Madogo.

Nilifanya yote haya ili kujiepusha na Biashara ya Dawa, ilibidi niangaike sana pale. Unajua Wabongo wengi wanajikuta wakiingia kwenye Biashara za Dawa kwa Mtindo kama huu, Yan ukifika ukakutana na Wabongo wenzio hawakupi nafasi ya kujipambania zaidi. Sasa kama wewe ni kichwa panzi basi unaishia kwenye biashara hiyo.

Mimi nilisema nitapambana mpaka dakika ya mwisho, swala la Kibali cha Kazi nitajua mbele kwa Mbele.

Basi nikafika mpaka pale Kanisani. Kuliona tu kwa nje nikajisemea hili ndo nilikuwa nalitafuta. Parking ilikuwa na Gari za Kifahari Kibao. Nikauliza Muda wa kuanza Ibada ya Mkesha wakaniambia kuwa ni saa moja usiku watu ndo wanaanza kuingia Kanisani. Washua Kibao walikuwa wamewahi pale, wamesimama kwa nje wakipiga story zao. Mimi nikasoma mazingira kisha nikatoka, nikazunguka zunguka pale Mitaani mpaka saa moja jioni ilivyofika nikarudi tena. Nikatimba zangu ndani.

Kama ilivyokawaida ya Makanisa mengi, mtu ukifika kwa Mara ya kwanza inabidi ujitambulishe. Tulisimama pale Kanisani kama wageni 50 hivi ndo ilikuwa Mara etu ya kwanza kufika pale. Baada ya kusimama na kujitambulisha kisha tulikaa. Wahudumu wa Kanisa wakawa wanapita kwenye kila Mstari kuchukua maelezo yetu. Nakumbuka kwangu alipita Msichana Mrembo hivi. Nilipomwambia kuwa Mimi ni Mtanzania na ndo nimefika south kwa Mara ya kwanza, alifurahi. Kwenye ile form yao nilijaza namba yangu ya simu. Wakuu kwa upande wa Lugha ya Kizungu siko vibaya sana. Naweza kujitetea kiasi chake.

Utaratibu mwengine wa lile Kanisa kwa mtu aliyefika Mara ya kwanza, wakati unajaza ile form yao wanakuuliza "Je kwenye hili Kanisa letu wewe utatusaidia upande upi?" Wakiwa na Maana Kama utaweza kujitolea mfano kufanya upande wa Media, Yan walikuwa wana Camera za kutosha mle ndani, Kanisa lilikuwa linaruka LIVE kwenye Mitandao ya Kijamii. Pia walikuwa wanataka kujua kama utajitolea kwenye upande wa Muziki sababu walikuwa na Kwaya yao na vyombo vyote vya Mziki. Kama wewe ulikuwa mtaalamu wa Maswala hayo ya Mziki basi utapangiwa huko.

Kwa hiyo ndani ya Kanisa Idara zilikuwa nyingi. Nikaona hapa nitumie fursa vizuri, Kwa kuwa Mimi nina taaluma Fulani ya Mambo ya Camera nikasema Mimi nitajitolea kwenye eneo hili. Yule Mrembo alifurahi kusikia hivyo. Akaniandikisha pale kisha akaondoka.

Ukweli Kanisa lilikuwa la Kishua na limechangamka sana. Kanisa lilikuwa na Gari la kwenda kuwachukua na kuwarudisha waumini wake.
Hii stori tamu sana....mi mtunzi wa movie naiba vitu hapa 🤣
 
Back
Top Bottom