Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Aisee kuwa na skills fulani fulani ni salaha nzuri kweli kwenye kujilipua, NOTED
 
Ndo kwanza asubuhi jana nimesinzia, leo Niko na fuko la ivori naendelea kupitia uzi, wa moto sana huu, nasoma kila kitu (wadhamini na episodes zenyewe), wadhamini natambua uwepo wenu unachangamsha uzi, wakati keagan Makonda Christian akiendelea kutuletea simulizi hii adhimu na azizi
 
Hongera Sana ukisikia wenye nyota ndo wewe Sasa, unatumia kile ulichonacho japo na wewe ulikuwa na uthubutu tu na wanao ukawabeba, ktk nchi za watu, Mungu mkuu njia zikafunguka,,


Watakuja wapiga debe hapa kusema wanawake tunapenda wenye pesa sijui Ni Nini!! Wakati hata kwenye biblia tunawasoma kina Easter alitumia uanamke kukomboa ndugu zake, nk
 
Upo sahihi mkuu
 
Wapuuzi Sana wanafanya passport ionekane Kama anasa kuwa nayo Yani wakati ni haki ya kila raia mwenye uhitaji kuipata pasipo mbwembwe zote hizo
@Noelia unajua huwa tunakosea sana sisi wabongo...

Passport ni hati au kibali cha kusafiria na tena kukutambulisha wewe kwa taifa jingine kama ni Mtanzania...

Sasa tujiulize wote tu, kama hauna mpango wa kwenda nchi nyingine, kwa nini uhitaji passport?

Halafu pia restrictions zinakuwa nyingi sababu kuna watu wanatumia passport kufanikisha shughuli zao za kiharamia kama kupitisha madawa ya kulevya n.k, sasa kama taifa huwezi tu kuwa unatoa passport ili kufanikisha mauharamia...

Mfano kipindi tulipokuwa na passport ya zamani (ile ya gamba la kijani), passport ya bongo ilikuwa shamba la bibi, watu wa mataifa mengine waliitumia sana kufanya mambo yao especially kwa zile nchi ambazo mbongo anaingia kwa kupata entry visa airport...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…