Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Dubai UAE pesa still upo ukiwa na mtaji , Connection na uaminifu..
Biashara ya magari used,manunuzi ya scrap cars kukata na kuuza vipuri bado yanalipa bongo /Africa.
Kuna bidhaa nyingi Sana kule Abc ninazo ninasubiri kujilipua tuuuu...
Naomba details za hii biashara inbox ndugu, kama hutajali sana. Natamani sana kuifanya
 
Huu Uzi ushaanza Mambo ya kutinduana Basi kwa akili za ndugu zangu watz Yan zishahama kwenda kupambana nje ya nchi saiz wanaanza kuvuta picha wa mtako wa kanya wakimlinganisha yule Mdada mkali anekuja na chuma kikali kanisani Yan sie wajinga Sana Yan tunafia kwenye kidonda Kama inzi.

Kuna stori ya Mayotte humu wengi tuliapa tutakwenda kabla ya hapo Kuna ya Botswana walewale wa Mayotte ndo haohao wanaocoment wanataka waingie Botswana hao hao Leo S.A sie wengi humu hatujielewi ndomana wakenya wanafurah wakikuta wanacompit na mtanzania.

Tujipange kufanikiwa kwa vitendo sio maneno moyoni yaan kuzania
 
Mkuu Keagan Paul ukimaliza yako, nami nitasimulia mkasa ulionikuta kule Arabuni nilipopelekwa na waarabu kwenda kucheza shoo kwenye kumbi zao.
Sitasahau....[emoji3064][emoji22][emoji17][emoji3064][emoji22][emoji17][emoji3064][emoji22][emoji17]
Unitag
 
Mkuu Keagan Paul ukimaliza yako, nami nitasimulia mkasa ulionikuta kule Arabuni nilipopelekwa na waarabu kwenda kucheza shoo kwenye kumbi zao.
Sitasahau....[emoji3064][emoji22][emoji17][emoji3064][emoji22][emoji17][emoji3064][emoji22][emoji17]
Hahahahahahah si uanzishe Uzi tu mkuu tuje na huko
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafanya hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Hakuna tabu kama kuishi na mtu ambae asubuhi anaamka amenuna bila sababu. Mtapiga story pale atakapojisikia yeye kuongea. Alikuwa Mjinga kweli yule jamaa. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. South Africa chakula bei rahisi. Kule gharama kubwa ipo kwenye Kodi za Nyumba na Nauli kwenye vyombo vya Usafiri. Kule Umbali wa Makumbusho mpaka Posta, Kwa Taxi zao, Kule ukisema Taxi ndio Daladala, unaweza kulipia hata Elfu 2 mpaka 3 za Kitanzania. Hiyo ni nauli ya kwenda tu.

Sasa Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi kula nyumbani. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
Lakini Kanya aliniganda kinyama.
Haya maisha kila MTU ana taka kuwa mzigo wenye manufaa... Ungewachngamkia wote... Ukiteleza nao unapata nafuu hata ukikosa sehemu ingine fresh utarejea kujibebisha na madevu yako *****... Maisha nyoso sana
 
Kama unavyojua hakuna kipindi bila wadhini. Embu tuonyeshe huo mtako tuoone... Umenifanya niwaze mengi mno. (Show us your ass I know you got pictures... Explore your gallery)

Astaqhafirullah .
Sheikh swaum tusije tengua.
 
Hizo picha unani PM tu hakuna sgida
Kama unavyojua hakuna kipindi bila wadhini. Embu tuonyeshe huo mtako tuoone... Umenifanya niwaze mengi mno. (Show us your ass I know you got pictures... Explore your gallery)

Astaqhafirullah .
Sio makubwa bi mdada ni Mapenzi yangu kwako tu[emoji120]
Maombi yenu yamefika.
Nawatangulizia picha Pm.
Asa ole wenu mzisambaze...mtakula Ban wenyewe.
 
Back
Top Bottom