Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Asante sana shoga huu mchezo una mbinu zake, yani nilikuwa naingia youtube, nasoma vitabu kama the art of seductio, natazama shows za wanawake waliopata wanaume wenye pesa walikuwa wanafanyaje plus na mbinu zangu za kitanga etc. Hawa wanaume wenye pesa na career zao humpati tu kizembe zembe lazima uwe na game plan. Wanakutana na wanawake wazuri na warembo wenye career zao daily...
Hahaaa ashera umeua..uahaa u made my day....ila umeandika maneno mazuri...kila kitu kizuri lazima ukihangaikie kukipata...iwe kazi au biashara lazima ujikunje...all the best
 
Heheheheeee pele limepata mkunaji, Asante mpenzi kwa msisitizo nimescreeshot hii comment yako manake si mchezo hao watu kama usemavyo ushindani Ni mkubwa hudanganyi hebu nijisogeze piemuni rasmi😍😍
Kale madesa dogo...ukikomaa nipe na mm...
 
Hahaaa ashera umeua..uahaa u made my day....ila umeandika maneno mazuri...kila kitu kizuri lazima ukihangaikie kukipata...iwe kazi au biashara lazima ujikunje...all the best
Sio wote wenye roho hizo, kuna jamaa pale Buzwagi alikuwa yupo vizuri sana, akaamua kuvuta lisimbe la Tabora likamuua na kujitwalia mali yote ya Marehemu Gold diggers wengi ni hatari.
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafanya hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Hakuna tabu kama kuishi na mtu ambae asubuhi anaamka amenuna bila sababu. Mtapiga story pale atakapojisikia yeye kuongea. Alikuwa Mjinga kweli yule jamaa. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. South Africa chakula bei rahisi. Kule gharama kubwa ipo kwenye Kodi za Nyumba na Nauli kwenye vyombo vya Usafiri. Kule Umbali wa Makumbusho mpaka Posta, Kwa Taxi zao, Kule ukisema Taxi ndio Daladala, unaweza kulipia hata Elfu 2 mpaka 3 za Kitanzania. Hiyo ni nauli ya kwenda tu.

Sasa Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi kula nyumbani. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
Lakini Kanya aliniganda kinyama.
Daaah hapo kwenye tako la Kanya najaribu kujenga tathmini
 
Asante sana shoga huu mchezo una mbinu zake, yani nilikuwa naingia youtube, nasoma vitabu kama the art of seductio, natazama shows za wanawake waliopata wanaume wenye pesa walikuwa wanafanyaje plus na mbinu zangu za kitanga etc. Hawa wanaume wenye pesa na career zao humpati tu kizembe zembe lazima uwe na game plan. Wanakutana na wanawake wazuri na warembo wenye career zao daily...
Aisee!Wanawake
 
Wajuaji ndo hu discourage tellers wengi kuendelea na story wanaishiaga njiani tu make kila mtu anajifanya anajua utafikiri walikua nae, Mtu anataka msimuliaji asimulie mpaka chooni alikua anaenda mara ngapi, saa ngapi kwa siku na aina ya rangi ya kinyc alichokua anatoa [emoji23]


Tupunguzeni ujuaji wakuu..
hahaa utawasikia mletauzi kunapahala umekosea [emoji38][emoji38]au utaskia kunasehem umeparuka hahaaa sasa unajiuliza huyu mjuba alikuanamsimuliaji hichokipindi yakimtokea[emoji849]
 
SEHEMU YA KUMI

Kwa Kifupi ndo nikawa South Africa nimeshaingia ivo bila ya kuwa na Ndugu wala Rafiki wakunipokea. Mambo ya kusubiria kuwa na Ndugu au Rafiki yangenichelewesha sana.

Basi Nilikaa pale nje mpaka saa saba usiku ndo Jamaa akaja kunichukua. Alisema kuna sehemu alikuwepo kuna Harakati alikuwa anafanya. Jamaa akanipokea Begi hao mdogo mdogo mpaka KFC tukapata chakula kisha tukaenda Magetoni kwake. Ilikuwa ni ghorofa. Yeye alikuwa amepanga Ghorofa kama ya tatu hivi. Tulifika na kuingia ndani kwake. Kilikuwa ni chumba kimoja, sebure kubwa, Choo na Jiko. TV Kubwa, Makochi ya Kisasa. Kwa kifupi jamaa alikuwa anaishi vizuri.

Tukawa tunapiga piga story pale, Jamaa alikuwa ananichukua Maelezo ili awe na uhakika kama kweli Mimi ni Mtanzania na Kama kweli natokea Temeke. Wabongo wengi wanafanya hivyo ili kujiridhisha kama kweli wewe ni Mbongo wasije kupokea Mburundi, Mkenya au Mkongoman. Baada ya story kidogo jamaa akaniambia panda kitandani upumzike.

Hapa nitasema kama ilivyokuwa, Juu ya Kile Kitandani jamaa alikuwa ametandaza Dawa za Kulevya Kibao. Ilikuwa ndo Mara yangu ya kwanza kuziona dawa za kulevya vile. Zilikuwa nyingi sana halafu Jamaa haogopi wala nini. Alikuwa anazifunga funga. Nikahisi pengine jamaa alichelewa kuja kunifata labda alikuwa busy kufunga hizi Kete zake. Yan jamaa anafunga bila woga, tena mbele ya Mgeni. Nikajiuliza jamaa anajiamini nini.

Mimi sasa, Usingizi wote wa Safari ulikata. Maana nakumbuka nililala pembeni ya hicho kitanda halafu pembeni yangu ndo kulikuwa na hizo Dawa. Huku tunaendelea kupiga story.

Katika Maisha yangu, Dawa za Kulevya nilikuwa nazisikia tu kwenye Vyombo vya Habari na kuwaona Mateja Mtaani. Lakini ile nafika tu South Afrika ndo kama hivi nilikutana nazo tena ile ile siku ya kwanza. Mara pale ghetto tukasikia Hodi, Kisha Jamaa wawili wakaingia ndani. Nao ni wabongo. Tukasalimiana pale kisha wakaendelea na Mishe zao. Wakafungua mabegi yao na kuanza kutoa Kete zao za Dawa za Kulevya na Pesa, ni kama vile walikuwa wanamkabidhi jamaa mahesabu ya siku hiyo. Kwa haraka haraka nilisikia pale, kila mmoja alimkabidhi jamaa kama Laki Nane za Kitanzania. Moyoni nikasema duh jamaa anatengeneza hela. Laki Nane kila mmoja, Je Jamaa ana vijana wangapi ambao kwa Siku kila mmoja anamletea Laki Nane?

Baada ya mahesabu yao, jamaa aliwapatia tena mzigo mwengine wa kuuza siku inayofuata yaani asubuhi yake. Kisha jamaa akaniambia "Sasa Homeboy utafatana na hawa jamaa utakwenda kuishi wanapoishi wao"

Basi pale nikaamka chap, Nikatoka pale Ghetto na wale jamaa wawili. Hao mtaa kwa Mtaa na Begi langu Mgongoni. Hiyo ni Kama saa Tisa au Kumi hivi usiku. Uchovu wote umekata. Natembea na jamaa ambao najua kabisa kwenye Mabegi yao kuna Dawa za Kulevya kibao.

Yan Mwili wangu ni kama vile ulichanganyikiwa kiasi, kutokana na uchovu wa safari, Mambo ya Dawa za Kulevya na Macho nayo yalikuwa yanashangaa tu uzuri wa ile Mitaa. Mitaa mizuri sana. Basi ilikuwa shida tu. Mchanganyiko wa Hofu na Furaha kwa pamoja.

Hao Hao mpaka kama mtaa wa Saba huko. Tulisimama mbele ya Ghorofa kubwa kama Kama Ghorofa 12 hivi. Pale getini mmoja wao alitoa Kadi ya kufungulia Mlango kisha Mlango ulifunguka wenyewe. Hao mpaka ndani, Tulipanda kwenye Lift mpaka Ghorofa ya 8 au 9 hivi. Walifungua Mlango tukaingia ndani. Kilikuwa chumba kimoja kikubwa, Chini walilaza magodoro kama manne hivi. Kulikuwa na Sebure, Choo na Jiko. Jamaa wakanikaribisha pale, tukapanda kwenye Magodoro tukalala. Kwa jinsi chumba kilivyokuwa nilihisi hawa jamaa humu ndani hawana muda wa kupika, vyombo vilikuwa shagalabagala, Kilikuwa ni chumba cha wao kulala tu.

Basi haikuchukua muda jamaa wengine kama Watatu wakaingia ndani. Ndo walikuwa wametoka kwenye mizunguko yao. Tukasalimiana kidogo kisha wote tukalala.

Baadae nilikuja kuelewa kuwa hawa jamaa wote wanafanya kazi ya kuuza na kusambaza Dawa za Kulevya za yule jamaa wa kwanza niliyekuta ametandaza Dawa Kitandani. Wote ni wabongo. Yule Jamaa Bosi wao, tumpe Jina Y, anawatumia nauli hawa Vijana huku Bongo halafu anakwenda kuwafanyisha hizo Kazi. Wengine ni Rafiki zake, Wengine ni ndugu zake. Wakifika hapo South ndo kama ivo anawapangia jamaa chumba na kuwalipia kodi na mambo mengine. Kwa hiyo hiki nacho ni chumba cha yule jamaa Y. Niliwaza kama hawa jamaa wote humu ndani kila mmoja anapewa mzigo wa Laki nane akauze kwa Siku, Jamaa Y atakuwa na pesa kiasi gani? Kwa hiyo Mimi kujileta mwenyewe kwenye huu mtandao wake jamaa alifurahi sana kuwa amepata mtu wa kumuuzia Dawa zake bila shida. Yaan Mbuzi Kafia kwa Muuza Bucha.
Kwa maana iyo kuanzia yule mshikaji wako na dada yake mpka vaileth na wengineo wa saloon wanajua huu mtandao kwa lugha nyepesi wanajua ulikuwa unapelekwa wapi.... ovaaaaa[emoji850]
 
Back
Top Bottom