Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alikuwa anashughulika na mahafari kwanzaDah yan #Daudi Bashite unatutesa kweli yan siku inaisha hiv hiv. Ebu mwaga wino next epsode
Wewe Ni mtunzi kama kina iron mosenya?Ngoja mimi niendelee wakati tunamsubiri Keagan Paul
Wakati tumemaliza ibada kwenye muda wa saa 3 usiku, ikabidi wanakwaya tuanze safari ya kurudi kwenye hotel soo wakati tunapanda kwenye usafari bahati nzuri Tshespo akaja kukaa pembeni yangu .
Niseme ukweli Tshesipo alikuwa kachangamka sana na kuonesha ukaribu sana na mimi wakati bado tuko kwenye gari akaniomba Camera akawa anaangalia zile picha tulizopiga asubuhi kule mlimani na kuniuliza hii umeipenda?? Hii imetoka vizuri huku akitabasamu
Wakati tumekaribia kufika kwenye zile hotel pembeni kidogo kulikuwa na kama hoteli ambayo njee kulikuwa na restaurant ambayo watu walikuwa wakipata chakula vinywaji na mziki kidogo mara tshespo akasema sehemu nzuri sana kwa kupata chakula imetulia na mimi pia nikadakia nzuri sana akasema basi akasema tukifika kwenye hoteli tugeuze hapo kupata chakula.
Basi tuipofika pale hotelini nilienda room kwangu nikajiandaa fasta nikawa namsubiria Tshesipo huku nikiendelea kuscroll camera mdogo mdogo kuangalia picha za Tshespo. Baada ya dakika chache nikaona sms keagan toto la konda, toka njee
shuka chini hapa parking.
Daa kotoka njee nilivyomuona sikujua kama ndio Tshespo tulietoka nae kanisani maana alikuwa kabadiika haswa, hapa ndio niiona urembo aliokuwa kabarikiwa Tshesipo maana alikuwa kavaa skerti fubi inaishia magotini,,mahips na tako yalivyokuwa yamejaa ndani ya hile sketi plus ule mpasuo ungedhani sketi ile inachanika ndani ya dkk mbili
Nywele zlikuwa zimeangukia mgongoni, chuchu saa sita oclock, guu sasa ndio nilichoka asee, guu nilidhani ni paja la mange kimambi, nikasema hapa keagan lazima leo nimueleze hisia zangu, baada ya kufika pale akesema mbona unaniangalia sana, nikamwambia hapana umependeza sana akacheeka huku tukiongozana kwenda restaurant .
Sio Msimbati ni Kilambo..Ruvuma ni njia ya Mtwara. Ila njia haifai kupita si nchi kavu wala majini.
Ukitaka kupitia njia ya maji nenda kazugie Msimbati ili wakufikishe Palma. Ugumu ni kutoboa kuipata Mocimboua.
Kama una ulazima wa kupitia Msumbiji bora upitie Blantyre hadi Beira malori ni mengi
Wanaume tumeumbiwa mateso
Wabongo kwa ujuji, Mnajifanya wachambuzi sana kumbe makenge tuNakuunga mkono...kuna namna inawezekana konda msafi kaamua kuja na huu uzi kivingine akitumia ID nyingine kongwe....
Sababu kuna flow ya uandishi story inashabihiana pia toka mwandishi wa hii story akate mguu humu..@konda msafi amekua active., kipindi kile mwandishi yuko active konda msafi alikua kimya.
Kuna ka similarity hapa...inaonekana tunachezewa akili.
Kabisa mkuu.. Hii tabia sio nzuri..Mtu unaleta uzi,kwa moyo wako kabisa mweupe tena hatujakuomba wala hata hatujuwi kama una uzi pendwa.
Unashusha episode kadhaa Mungu ni wa wote gafla uzi wako unapendwa watu wanaacha kazi, wanakopa bando, yaani kila dk,wanacheki uzi.
Halafu,gafla speed ya kushusha episode inaanza kupungua mara narudi, mara kesho mara yanapita masaa 24 kimya.
Hii tabia ni ukatali kama yalivyo matendo mengine ya ukatili.
Ukianzisha kitu kimalize kiishe raha ya story,isomwe ikiwa bado ya moto na bando zetu hazijachacha.
Ukileta uzi au,story,hlf usipate watu unajisikia vibaya,watu wakija unapotea mnaoleta uzi mnatuchanganya.
Tunaponunua kubando, tukatenga muda kusoma uzi kati ya hbr kibao zilizo humu JF ni mapenzi na uzi huo.
SAWA TUNAJUWA KUNA DHARULA, SHIDA MATATIZO,,MUDA NA MENGINE, UKIPATA DHARULA UKAHISI HUTAANDIKA KWA MUDA SAHIHI, TOA TAARIFA KUWA WADAU KUNA DHARULA NAOMBA SIKU 2 NIPUMZIKE NIDYO TUTAENDELEA. Huo ndiyo uislamu, na ndiyo ukiristo, na ungwana.
unapoleta kisa chako wazi inamaana kuwa unataka tujifunze jambo na kufurahia pia kulingana na story iliyoletwa.
WANAJF kabla ya kuleta story yako plz kaa tafakari na ufanya maamuzi kuwa naandika hii story,mwanzo mwisho iishe na nimejitolea kwa moyo wangu wote ukimaliza kiapo ndiyo unaanza kuandika.
Ukisubiri sana kitu hata ile radha yake inaanza kuisha.
MLETA UZI,,TUNASHKRU,KWA UZI WAKO, TUNASHKRU,KWA EPISODI 16,
LAKINI kaa tafakari kama tunaendelea basi tuendelee kama imeisha basi sema wazi,,kama una dharula sema wazi pia.
Kutuweka roho juu kama tunaoga njia panda siyo fair kabisa.
NB. wengine pia wenye nia za kuleta story,kabla ya kuleta kaa fanya maamuzi kiwa story hii niwasimulie au nikae nayo daima,, hbr za kusimulia mara mchango wa MB, mara unapotea siyo kitu sahihi.
Mkuu weka weka na uongo kidogo story inoge unaweza kusema ibada tulifanyia mlimani na huo mlima ulikuwa mrefu kuliko Mount Kilimanjaro au sio!SEHEMU YA KUMI NA SITA
Ukweli niseme kitendo nilichokifanya cha kupost zile picha hata mimi nilikijutia sana. Unajua wakati mwengine ukimpenda mtu kuna vitu vingine unajikuta umefanya tu, hata ukiulizwa sababu kwa nini ulifanya hivyo huelewi. Malengo yangu yalikuwa yanamhitaji sana Yule demu mwengine kuliko Kanya. Siku iliyofuata nilienda mpaka alipokuwa anaishi Kanya, Nilijaribu kukaa nae kuzungumzia hii ishu, nilimuomba Msamaha mwishoe alinisamahe, maisha mengine yaliendelea.
Tuliyamaliza lakini Kichwani nilibaki na dukuduku Fulani hivi, nilikuwa nawaza sasa nitafanyaje? Maana Kanya kwangu nilimuona kama mzigo wakati mimi nilipanga kutafuta demu ambae atanisaidia kufikia safari yangu. Namtema vipi Kanya? Yule demu mwengine tukawa tukikutana Kanisani tunasalimiana fresh, kwenye simu tunawasiliana. Ukaribu uliongezeka kiasi chake, Alikuwa hajui chochote kilichokuwa kinaendelea, Baadae nilikuja kujua kuwa huyu demu anaitwa Tshepiso na anafanya kazi Capitec Bank.
Sasa kuna wakati Kanisa lilitangaza kuna Safari ya kwenda kutoa Huduma za Kiroho kwenye Tawi lake lililopo Nchini LESOTHO. Kanisa lilikuwa na Matawi mpaka Marekani na Baadhi ya nchi za Ulaya. Walisema anayetaka kwenda na kama una Passport basi ruksa mtu yeyote kwenda, Usafiri, Chakula, Kulala vyote ni gharama za Kanisa. Nikasema hii ni fursa kwangu ya kuwa karibu zaidi na Mchungaji na Washua zaidi. Mpaka hapa kwa kweli nilianza kukubalika pale Kanisani si kama Mwanzo. Nilikuwa sio mgeni tena kwenye macho yao.
Lesotho ni nchi ndogo, Mfano ni kama Mkoa tu wa Morogoro au Morogoro inaweza kuwa Kubwa pia. Ni nchi ambayo ipo ndani ya nchi ya South Africa. Nchi yote imezungukwa na South Africa. Kama mtu hufahamu unaweza ku google ukaona.
Sasa kwa wasiofahamu, Vijana wengi wazawa wa South Africa hawana Passport za kusafiria, Wengi sio sana watu wa kusafiri safiri, kwa hiyo kigezo cha watu kuwa na Passport kilipunguza waumini wengi sana akiwemo Kanya. Alikuwa hana Passport. Kwenye Upande wa watu wa Camera, Mimi na Max tu ndo tulikuwa na Passport. Nilichofurahi Tshepiso alikuwa na Passport kwa hiyo alikuwepo kwenye hii safari.
Utaratibu wa siku ya Safari tulikuwa tunapewa gari Fulani zina muundo kama wa Toyota Alfad, rangi nyeupe, Mnakuwa mnachaguana wenyewe waumini kama sita, kati yenu anapatikana pia dereva, kisha mnaanza safari. Mimi na Tshepiso tulipanda gari tofauti. Siku ya safari ilikuwa ni jumamosi ila Muda wa safari mnapanga wenyewe wana Kikundi, Mchungaji alisema anachotaka watu wote Jumapili tuwe tumefika Lesotho. Kwa hiyo Kanisa lilitoa gari kama 10 hivi. Watu tukaanza safari. Sisi tulianza safari jumamosi jioni.
Kwenye gari yetu mwanaume nilikuwa peke yangu, wengine wote madem. Wote kati yetu hakuna hata mmoja anaijua njia ya kutufikisha Lesotho. Yan wenzetu wana barabara nyingi kiasi kwamba unaweza kuzaliwa palepale na Baadhi ya barabara za kuelekea baadhi ya nchi huzijui. Na ukikosea tu barabara unaweza kutumia muda mwingi sana kurudi kwenye barabara uliyoikusudia kupita. Nakumbuka tulipotea sana. Mpaka ikabidi tutumie Navigator kwenye simu zetu. Wote ndani ya gari tuliwasha Navigator tunamwelekeza dereva wetu wapi pa kupita.
Tulifika Boda kati ya South Africa na Lesotho usiku wa kama saa Saba hivi. Kwa kuwa nilikuwa na mademu wote, mimi ndo niliwaongoza mpaka mle ndani kwenye Ofisi za Uhamiaji. Kwa kuwa kwenye Passport yangu nilikuwa nimezidisha siku za kuishi mle South Africa, Nilisoma mazingira pale kwenye Passport yangu nikaweka Rand 300, nikagongewa bila shida. Japo Lesotho tulikuwa tunakwenda kukaa siku Tatu tu lakini Uhamiaji upande wa Lesotho walinipa siku Thelathini za kukaa Lesotho. Nilikuwa tayari mzoefu wa kupita kwenye Maboda.
Wale mademu walikuwa wanazinguliwa pale, nikawaambia wekeni Rand 100 kwenye Passport zenu halafu nendeni tena, wakafanya hivyo kisha wakagongewa mihuri kasoro mmoja tu kati yetu ndo hakugongewa huyo demu alikuwa ni Mnaijeria, Kwanza Mnaijeria kuingia Lesotho inabidi alipie visa. Sio kama sisi wengine tunaingia free tu. Pili Yule demu kama mimi tu pale South Africa alikuwa amezidisha siku za kuishi (Ame Overstay). Kwa hiyo wale maafisa uhamiaji walikuwa wanataka pesa ndefu.
Nakumbuka alikuwa anasema “Mbona Mtanzania na yeye ametoka mbali lakini amegongewa bila shida”. Basi pale mmoja wetu akafanya mawasiliano na mchungaji, Mchungaji na baadhi ya waumini walikuwa wameshafika Lesotho tayari. Kwa kuwa sio mbali sana, ule ule usiku, mchungaji ikabidi aje mpaka pale boda. Akaongea nao wale Maafisa Uhamiaji, nadhani aliwapa pesa kidogo ila sina uhakika sana. Hatimae wakatuachia tukaendelea na safari yetu mpka Mji Mkuu wa Lesotho unaitwa Masseru. Masseru pa kawaida sana pengine hata Dodoma pazuri. Huwezi hata kulinganisha na Dar, Arusha au Mwanza. Basi tulienda moja kwa moja kwenye Hostel tulizopangiwa kufikia. Tulilala pale.
Asubuhi mapema sana tuliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kupanda Mlima kwa ajili ya Ibada, Ibada ya kwanza tulienda kufanyia milimani huko. Ibada ya Jioni ndo tulienda kwenye Kanisa lao. Kwa hiyo Hata kupanda huo Mlima nakumbuka ilikuwa ni tabu, Mlima ulikuwa mrefu kiasi chake. Wakati magari yetu yanakusanyika pale chini ya Mlima ndo nilikutana na Tshepiso.
Ukweli Lesotho tuliinjoi sana, kwanza tulikuwa wachache, kwa hiyo tulikuwa kama ndugu Fulani hivi, tulipiga picha kama zote mpka leo hii ninazo kwenye Email yangu. Nikiziangaliaga huwa zinanikumbusha matukio yote haya ninayoyaeleza. Kule Lesotho Mimi na Tshepiso tulikuwa marafiki kinoma yan, ile Camera ya Kanisa niliyokuwa natumia kupiga picha, Picha nyingi nilimpiga yeye. Wakuu zote hizo ni harakati za kutaka kutafuta Mchongo ndani ya nchi ya watu. Naomba nisieleweke kwamba mimi ni Marioo ila mazingira ndo yalikuwa yananilazimisha kufanya nilichokuwa nafanya. Nilijua hapa nikicheza tu Akiba yangu ya Pesa inaisha yote halafu kinachofuta ni maisha magumu na kurudi Bongo, halafu mpango wa Kurudi Bongo nilikuwa sina kabisa.Nilijua nikifanya uzembe nitarudi kuuza Dawa za Kulevya kwa Jamaa Y. Kwa hiyo nilikuwa najaribu kuuwahi muda. Na huyu mwanamke naona kabisa kwa maisha yake anaweza kunifikisha Mahali.
Mkuu hapo ni south Africa au Mabatini Tandika?Kwa sasa nina ofisi mbili. Moja ipo Smit Street na Clein na nyingine ipo Edenvile hapa hapa J'burg. Mtaji wa mtu ni akili yake mwenyew, sio kila aishie kaburu ni muuza bangi au unga. Karibuni mapocho pocho wakubwa
View attachment 1757913
Nijifiche kwani wewe kifo.Ww sio hadhi yangu binti nikisema nikutane na ww utajificha kwa aibu au kuzima simu kabisa ww endelea na hao wanakufata PM huko mm nipo mbali sana na ww
Ww sio hadhi yangu binti nikisema nikutane na ww utajificha kwa aibu au kuzima simu kabisa ww endelea na hao wanakufata PM huko mm nipo mbali sana na ww
hii afu ya moto.