Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu nipatie Link kama kawaida yetu kupeanaUkimaliza story ya kumbu, tafuta story inaitwa "how i met my wife" na story ya HAMIDA, Utanishukuru baadae.
Basi hajaizunguka Tanzania ila ungesema alienda baadhi ya mikoa.Malengo tu mkuu
Basi hajaizunguka Tanzania ila ungesema alienda baadhi ya mikoa.Malengo tu mkuu
@Madame BNijifiche kwani wewe kifo.
Relax, huu mchezo hautaki hasira bro.
Kwanza nishajizoeaga siku nyingi kuhusu nyie viumbe kuanzia insta, fb mpaka huku.
Unadhani utasema wewe wa hadhi ya chini...thubutuuuu!!!!
View attachment 1759830hii afu ya moto.
Mkuu, sijui jinsi ya kuweka link,tuombe wakuu wajuvi watusaidieMkuu nipatie Link kama kawaida yetu kupeana
Naona harufu mbaya hapa unataka kumkimbia jamaa sababu kafukuzwa kazi?I love this....aaaaawwwwww!...mtafute aje atuamshe mavifaduro yetu tuamke mkuu
Aisee! Mumsamehe jamaa, labda atakuja na maelezo kuhusu hili. Binafsi huwa sipendi to jump to conclusion. Tumsubiri kwanza aje huenda akawa na maelezo mazuri ya kujustify hii kitu.Wakuu hii story pigieni mstari ndio imeishia hapa, alishawahi kuisimulia na haikuwa na wachangiaji lakini hakuimaliza. Kwaiyo fanyeni mambo mengine tu...
Uzi maalum wa Harakati za kutafuta maisha nje ya nchi na changamoto ulizokutana nazo
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, Mara yangu ya kwanza kufika Beit Bridge, mpakani mwa Zimbabwe na South Africa, ilikuwa saa nane usiku. Ilikuwa safari ya siku tatu kutoka Dar hadi kufika hapo. Ndani ya bus tulikuwa tumechoka sana. Bus lilikuwa na raia wengi wa Zimbabwe na Zambia, Waburundi...www.jamiiforums.com
Aisee! Mumsamehe jamaa, labda atakuja na maelezo kuhusu hili. Binafsi huwa sipendi to jump to conclusion. Tumsubiri kwanza aje huenda akawa na maelezo mazuri ya kujustify hii kitu.
Katulisha matango pori angalia link hiyoMuulize yeye ameshawahi kuandika story yoyote hapa jukwaani??
Anatufanya Watoto bhana anatunnywesha Chai huku anaringa.Aisee! Mumsamehe jamaa, labda atakuja na maelezo kuhusu hili. Binafsi huwa sipendi to jump to conclusion. Tumsubiri kwanza aje huenda akawa na maelezo mazuri ya kujustify hii kitu.
SEHEMU YA TANO
Wakuu nitajitahidi kuandika kwa urefu na nitajitahidi kuandika kila kitu ili mtu mwengine aweze kujifunza kitu. Hata matukio yangu ya aibu pia nitawaeleza ili mtu ajifunze kitu kupitia story yangu na Kama kuna Makosa nilifanya basi iwe rahisi kwa mtu mwengine kujifunza na kurekebisha.
Nilivyorudi kwa yule Dada wa Uhamiaji, alifungua Passport yangu bila kusema chochote aligonga Mhuri nikaondoka zangu. Nikajua kumbe mwanzoni alisema vile ili kunitengenezea mazingira ya kutoa rushwa.
Nilivyotoka tu pale Kaunta, wale Vishoka wakanifuata ili niwarudishie ile Pesa yao, Kwacha 50. Kumbuka hapo nilikuwa bado sijabadili pesa za Kigeni. Nikawauliza wale Jamaa, Kwacha 50 ni sawa na shilingi ngapi za Kitanzania ili niwarudishie pesa yenu, wakaniambia "Wewe tupe Laki Moja tu"
Nikaona wananiletea Ujinga, nikatoka mpaka nje kwa Jamaa ambae alikuwa anawabadilishia watu fedha, Wale Vishoka wapo nyuma yangu tu. Nikataka kubadilisha Pesa yule Jamaa akakataa akasema "Malizana kwanza na hao Jamaa zako".
Nikamwambia kuhusu hawa Jamaa niachie Mimi, wewe nipe huduma tu ya Kubadilisha Pesa, Jamaa alikataa. Nikamwambia basi niambie Kwacha 50 ni sawa na shilingi ngapi za Kitanzania, Hata hilo nalo alikataa aliendelea kusema " Maliza kwanza na hao Jamaa".
Nikaondoka pale kurudi kwenye Bus ili nimuulize Dereva au Konda, Wale Vishoka wapo tu nyuma yangu. Dereva na Konda nao walikataa kutoa ushirikiano kwa madai ya kwamba nimalizane kwanza na wale Vishoka.
Hapo Vishoka wanatoa maneno yote ya Shombo. Lakini nilijifanya kama Siwasikii vile, mwisho wa siku nikawaambia oya nyie sikilizeni Mimi hiyo Laki Moja sina fanyeni mnachotaka kufanya. Tukaanza kuvutana vutana pale na kurushiana maneno. Abiria wengine wapo kimya wanatusikiliza tu.
Mwisho wa Mabishano nilikubali kuwapatia Elfu 50. Roho iliniuma sana. Nilijua fika hapa nimepigwa. Baadae nilikuja kujua kuwa Kwacha 50 ilikuwa kama Elfu Nane ya Kitanzania. Ndo hivyo nilishapigwa.
Baada ya wale Vishoka kushuka ndani ya Bus niliwauliza Dereva na Konda kwa nini walikataa kunisaidia. Wakaniambia kuwa wao ile njia wanapita kila siku na hao Vishoka wapo hapo Boda ya Tunduma miaka na miaka. Kwa hiyo kama wangenisaidia basi Bus lao lingefanya kazi katika Boda hiyo kwa tabu sana pengine wangeweza kutobolewa matairi kila watakapokuwa wanapita hapo. Kwa kweli niliwaelewa.
Aisee kumbe sikuwa peke yangu niliyepigwa usiku ule. Mara waliingia Abiria wengine na Vishoka wengine wakigombana kama ilivyokuwa kwangu. Moyoni nikasema hapa itakuwa kuna mchezo unachezwa kati ya Maafisa Uhamiaji na hawa Vishoka. Ndo mana wanaruhusiwa kuingia hadi ndani.
Tulilala ndani ya Bus hadi asubuhi ndo tukaendelea na safari ya kuelekea Zambia.
....SEHEMU YA TISA
Kwa ambao hawajafika South Afrika, Umbali kutoka Pretoria mpaka Joberg ni Kama Dakika 45 tu, Lakini Umbali kutoka Pretoria mpaka Capetown ni Masaa 24. Ni Mbali ndo mana Ahamad na Dada yake walitumia ndege.
Sikukaa sana pale kwa Vailet, Vailet aliniambia twende Mitaa wanayokaa Wabongo nikutafutie sehemu ya kuishi.
Kumbuka mpaka nafika hapo Pretoria nimesafiri siku 4, nimechoka sana. Sijawai kusafiri Umbali mrefu hivyo. Halafu mpaka muda huo nipo barabarani nazurura tu na Begi langu mgongoni.
Wakuu hapa ilipofika story yetu, kutokana na Harakati za Maisha na Biashara ambazo nilikuta watu wanafanya ambazo nitazieleza huko mbele, naomba sitotaja watu majina yao ya ukweli.Tukafika mpaka Mitaa fulani kuna Saloon nyingi, Vailet akamuita jamaa mmoja tumpe jina X, Nakumbuka akamwambia "X huyu jamaa ndo ameshuka hapa muda huu, naomba mtafutie sehemu ya kulala" alisema hivyo, wakapiga story kidogo halafu Vailet akasepa. Nikawa chini ya Mikono ya mtu mwengine.
Basi pale X akaanza wenyewe wanasema "Kunichukua Maelezo". Akaanza kuniuliza Dar natokea sehemu gan na maswali mengine mengi. Nikamjibu yote. Nilivyotaja sehemu niliyotokea hapa Dar kuwa ni Temeke, X akasema kuna watu kutoka Temeke kibao wako hapa. Ngoja nimpigie simu Jamaa mmoja wa Temeke akufate tena ndo utaishi kwake.
Alimpigia simu huyo jamaa, Jamaa akasema atanifuata. Mpaka inafika saa mbili usiku X anafunga Saloon yake huyo Jamaa bado alikuwa hajafika. X akafunga akasepa, akaniambia "Msubiri jamaa usiwe na wasiwasi atakuja tu" Nilipigwa na Baridi kwenye nchi ya watu mpaka Saa Sita usiku jamaa bado hajafika. Kumbuka hapo nimechoka ile mbaya. Inaingia siku ya Tano bila kulala Vizuri. Nina Usingizi Kinoma.
Na ametuweza kweliWakuu hii story pigieni mstari ndio imeishia hapa, alishawahi kuisimulia na haikuwa na wachangiaji lakini hakuimaliza. Kwaiyo fanyeni mambo mengine tu...
Uzi maalum wa Harakati za kutafuta maisha nje ya nchi na changamoto ulizokutana nazo
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, Mara yangu ya kwanza kufika Beit Bridge, mpakani mwa Zimbabwe na South Africa, ilikuwa saa nane usiku. Ilikuwa safari ya siku tatu kutoka Dar hadi kufika hapo. Ndani ya bus tulikuwa tumechoka sana. Bus lilikuwa na raia wengi wa Zimbabwe na Zambia, Waburundi...www.jamiiforums.com
Story yenyewe ya kutunga mkuu.tuliza chura wewe, unatuharibia mtiririko wa uzi